Kupitisha airport cargo yenye nguo za mtu binafsi alizokuwa anazivaa akiwa nje ya nchi

Tripo9

JF-Expert Member
Sep 9, 2009
4,352
3,533
Kupitisha airport cargo yenye nguo za mtu binafsi alizokua anazivaa akiwa huko nje ya nchi alikokua anakaa sasa anarudi nazo bongo. Lakini kama cargo je customs analipia shs ngapi pale airport?

Asante.
 
Kwa kawaida huwa hakuna malipo yoyote kwa personal belongings (kuna jina lake kitaalamu kwenye lugha za kodi ila nimelisahau nadhanai wanasema kitu kama personal effects). Zamani kidgo maafisa wa forodha walikuwa wanapiga mkwara kusudi uwape kitu kidogo. Kuna wakati nilirudi na nguo nyingi sana masanduku manne ya kilo 40 kila moja; nguo zile kulikuwa ni za kwangu na nyingine ambazo nilikuwa nimepata donation kupeleka kwa ndugu na marafiki huko kijijini kwetu.

Maafisa wa forodha walitaka kunipiga mkwara sana na kuna jamaa mmoja alikuwa anasema hiyo ni biashara ya mitumba. Hata hivyo baadaye walinielewa wakaniacha, ingawa walifanya hivyo baada ya kunicheleshewa ndege ya precisionair niliyokuwa naenda nayo Shinyanga. Kwa hiyo nikalala dar es Salaam hadi kesho yake. Gharama ya Kulala na usafiri dar es Salaam ilikuwa ni kubwa kuliko hongo ambayo ningeweza kuwapa. Wakati huo nyumba yangu ilikuwa kule changanyikeni haijaisha, na sikuwa nategemea kusumbumbua ndugu na marafiki hapo jijini.

Mizigo yangu haikuwa Cargo, bali ilikuwa unacompanied luggage ambayo ilikuwa kwenye ndege ile ile niliyoruka nayo; kwa hiyo tulifika pamoja.
 
Kwa kawaida huwa hakuna malipo yoyote kwa personal belongings (kuna jina lake kitaalamu kwenye lugha za kodi ila nimelisahau). Zamani kidgo maafisa wa forodha walikuwa wanapiga mkwara kusudi uwape kitu kidogo. Kuna wakati nilirudi na nguo nyingi sana masanduku manne ya kilo 40 kila moja; nguo zile kulikuwa na za kwangu na nyingine ambazo nilikuwa nimepata donation kupeleka kwa ndugu na marafiki huko kijijini kwetu. Maafisa wa forodha walitaka kunipiga mkwara sana na kuna jamaa mmoja alikuwa anasema hiyo ni biashara ya mitumba. Hata hivyo baadaye walinielewa wakaniacha, ingawa walifanya hivyo baada ya kunicheleshewa ndege ya precisionair niliyokuwa naenda nayo Shinyanga. Kwa hiyo nikalala dar es Salaam hadi kesho yake. Gharama ya Kulala na usafiri dar es Salaam ilikuwa ni kubwa kuliko hongo ambayo ningeweza kuwapa. Wakati huo nyumba yangu ilikuwa kule changanyikeni haijaisha, na sikuwa nategemea kusumbumbua ndugu na marafiki hapo jijini.

Mizigo yangu haikuwa Cargo, bali ilikuwa unacompanied luggage ambayo ilikuwa kwenye ndege ile ile niliyoruka nayo; kwa hiyo tulifika pamoja.
Ooh asante sana kwa mchango wako.
Wewe sasa mizigo yako inaitwa checked in luggage sababu umepanda nayo mumo kwa mumo sema imewekwa kwa buti.

Ya kwangu sasa inaitwa unaccompanied luggage coz inasafiri yenyewe halafu mtu anapokea tu. Tena ni kule sehemu ya cargo.

Pia mchango wako umenifungua macho kua ni suala la kuongea nao tu hapo kuwaelezea bhana hizi ni mijinguo tu.
Ngoja nisubiri na michango mingine.
 
Kupitisha airport cargo yenye nguo za mtu binafsi alizokua anazivaa akiwa huko nje ya nchi alikokua anakaa sasa anarudi nazo bongo. Lakini kama cargo je customs analipia shs ngapi pale airport?

Asante.
Personal effects, hakuna kodi hapo
 
Kuna kiwango cha uzito wa mzigo ambacho kimewekwa ni bure mtu kusafiri nacho ila ikizidi lazima ulipie haitojalisha ni nguo au ni nini!
 
Kuna kiwango cha uzito wa mzigo ambacho kimewekwa ni bure mtu kusafiri nacho ila ikizidi lazima ulipie haitojalisha ni nguo au ni nini!
Mkuu huu mzigo hauji na abiria. Unakuja wenyewe wenyewe kama cargo.
 
Kupitisha airport cargo yenye nguo za mtu binafsi alizokua anazivaa akiwa huko nje ya nchi alikokua anakaa sasa anarudi nazo bongo. Lakini kama cargo je customs analipia shs ngapi pale airport?

Asante.
Inategemea na kilo bwashee pale na aina gani ya mzigo garama /thamani
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom