Ukwasi unaopatikana kwenye Kampuni za kusafirisha mizigo

BM X6

JF-Expert Member
Nov 24, 2020
1,360
4,149
Nitakachoenda kukieleza kitakuwa sio kigeni sana kwa watu waliofuatilia story yangu ambayo ilikuwa ni Live Story/True story ambapo story yenyewe nilianza kuipost humu mwezi kama huu July tarehe 6 mwaka jana 2022. Hatma ya Maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni ndio kichwa Cha story

Story kwasasa imesimama kwa muda ila itaendelea kama nilivyosema ni live story so kinachoendelea ndio ninachoandika kwa muda huo ila kwa tahadhari ya kuchuja matukio coz matukio mengine ni nyeti kidogo

Sasa ndani ya hii story kuna kijana anaitwa BM X6 ambaye anafanya kazi kwenye Kampuni ya kusafirisha mizigo kutoka china kwa kutumia usafiri wa ndege, huyo kijana ni Mimi

Katika story nilikuwa nikidokeza mambo kadhaa yanayohusu hii kazi ambayo najishughulisha nayo na namna ninavyo tengeneza pesa, wengi walikuwa interested na story kwa ujumla lakini wengine wakawa interested kwa upande wangu mimi na kazi ninayoifanya kwasababu Story ilikuwa na matawi mengi, moja kati ya tawi pendwa ni zile sehemu ambazo zitamuhusisha Caryn na Mimi, Sasa ukishaona Jina la Caryn na BM ujue na kazi pia itahusika na ndio wengi wakawa interested zaidi

Sitaeleza sana kuhusu hiyo story, kwa ambaye hujasoma kama ukipata muda utaipitia kwa Wakati wako. acha leo tudili na kilichonifanya nifungue huu Uzi

Kama kichwa kinavyosema Ukwasi unaopatikana kwenye Kampuni za kusafirisha mizigo Kampuni za kusafirisha mizigo zipo za aina nyingi lakini hapa nitazungumzia hizi Kampuni za kusafirisha mizigo kwa Ndege kutoka taifa moja kuja taifa jingine hasa hasa nitazungumzia taifa la China na Tanzania maana ndio eneo nililokuwa nafanyia kazi so nitakachokieleza nitakuwa na ufahamu nacho

Kumbuka Ukwasi/Utajiri unaweza kupatikana kwenye shughuli ya aina yeyote inayokuingizia kipato Cha kutosha ila mimi nimeamua kuelezea upande wa Air Cargo kwasababu ndio eneo ninalishuhudia watu wanavyopiga pesa, sio tu kwa wenye Kampuni bali hata maafisa wa TRA na Ma-Agent

Naomba nikumbushe kitu kabla sijaendelea....Sipo hapa ku motivate mtu, maana katikati ya Uzi kuna namba na mahesabu mazito sana hivyo mtu kama una hela zako unaweza kuhamasika na wewe ufungue Kampuni.

Ushauri wangu kama utataka kufungua Kampuni basi fungua kama ulikuwa na mipango hiyo na isiwe sababu ya huu Uzi, unajua kwanini nasema hivyo? ni kwasababu pengine katika huu Uzi kuna changamoto nitazisahau kuziandika halafu ukaenda kukutana nazo zikuvunje moyo mwisho wa siku uwe umepoteza muda na Pesa

Kwanza kipindi Cha mwanzo hutaiona hela kabisa, inahitaji uvumilivu maana utakuwa unasafirisha kilo chache mno kutokana na upya wa Kampuni na pesa yake utakuwa huioni, halafu katika kipindi hiki inabidi utafute Kampuni nyingine uwe unasafirisha nao ili muweze kushea Airways bill maana ukisema usafirishe kilo mia tatu mwenyewe kwenye ndege utakula tu hasara na kipindi hiki ni kipindi Cha kupata watu wa sales wazuri

Na ili changamoto zisikukwamishe basi unahitaji watu wazoefu ambao wanaweza kuzishinda hizo changamoto, aina ya hizi Kampuni nyingi nimeshuhudia zikiajiri watu wazoefu na sio wenye elimu tu, kwanza hizi Kampuni zinaibiana sana wafanyakazi hasa hawa wa sales, Yani kama kuna mtu wa Sales and Marketing ambaye ni mzoefu hana elimu na yupo mwenye elimu but zero experience mimi binafsi nitakushauri Chukua mzoefu kwasababu anajua njia ya kuwaingia wafanyabiashara hasa wa pale kariakoo.

Advantage kubwa zaidi hawa wazoefu tayari wanakuwa na wateja wao, kwahiyo kama unamchukua ujue ni lazima atakuja pamoja na wateja wake aliowatafuta akiwa huko kwenye Kampuni aliyokuwa akifanyia kazi, Japokuwa kuna wateja wengine ni ngumu kuhama hama hasa kama mahali alipo atakuwa anapata huduma bora, ila ukimpata mtu wa sales ambaye ni smart na mzoefu wa hizi kazi anaweza kuondoka na mteja wake,

Mteja nae sio zwazwa kwamba atakuwa anapelekwa pelekwa tu, atakachokifanya yeye atakubali ili kupima ubora na unafuu, Sasa hadi hapa mtu wa sales anakuwa kashafanya kazi yake, kazi inabaki kwa Kampuni ku deliver good service,

Kufikia hatua Kampuni inatakiwa iwe imeshafanya research na kujua madhaifu ya Kampuni ya anayotoka huyu mteja mpya, ukijitahidi kwa kutoa huduma nzuri tu labda inayofanana na mpinzani wako basi ujue mteja ana chance kubwa ya kurudi kule alipotoka kwasababu utakuwa hauna jipya, hivyo jitahidi sana kuwa wa tofauti katika kuboresha huduma na ikiwezekana pia bei zako ziwe tofauti kwa kuzishusha kidogo

Hata mtu ambaye atakuwa anakutolea mzigo Bandarini hakikisha unachukua yule nguli, kwasababu hapa ndio mambo yote, ukikosea hapa hakuna Mahali utafika, ukipata agent ambaye ni smart plus mzoefu na ambaye hana tamaa tayari una asilimia 60 za ushindi, hapa pia usiangalie elimu sana, ushauri wangu ni ule ule, ukimpata mzoefu na mwenye elimu basi pita na mzoefu

Kwenye Kampuni kama hii Muhasibu ni muhimu, hapa sasa angalia mwenye elimu yake ili mahesabu yaende sawa. Mimi Binafsi katika Kampuni natumika katika kutoa mizigo pale Airport pamoja na Bandarini hivyo kazi yangu inaniweka karibu na Muhasibu maana ndio mambo yote ya Mchele mchele anahusika nayo

Kwa muda huu mchache nitakuwa Muhasibu ili kukuonesha watu wanavyopiga pesa kupitia hizi Kampuni za usafirishaji mizigo kwa ndege

Kwa kuanza ni kufahamu namna TRA wanavyocharge mizigo pindi unapoitoa nje ya nchi, Mfano kwa hii mizigo ya kawaida kutoka China au Uturuki kama nguo, hereni viatu nk kwa kawaida huwa wana charge kuanzia Tsh 1,600 hadi 2,000 kwa kilo. itategemea una mzigo gani, kama ni Spea utachajiwa kuanzia Tsh 1,700 hadi 2,000 kwa kifupi utachajiwa kwa namna utakavyoongea nao inaweza kuwa Tsh 1,603 au 1,808

Pia kuna Spea zingine hawachaji kwa kilo, wanaangalia invoice yako, Mfano kama vitu vya network network mara nyingi sana huwa hawachaji kwa kilo lakini pia ukitumia u master wako unaweza kuchajiwa kwa kilo na ndio maana mwanzo nilitoa kipaumbele kwa watu wenye uzoefu dhini ya wenye elimu, kwasababu kwa ninavyojua mwenye elimu bila uzoefu ataenda kwa kukariri mwisho wa siku atapigwa sana, hadi na yeye aje kupata uzoefu maafisa wa TRA washapata vitambi

Hii pia ni moja ya sababu ya hizi Kampuni kucharge bei tofauti tofauti kutokana na aina ya mzigo, wewe uliyesafirishiwa makava ya simu cost zako zitakuwa tofauti na yule aliyesafirishiwa simu, kwa kifupi kama ilivyo kwa TRA pia hizi Kampuni kuna mizigo wanacharge kwa kilo na kuna mizigo wanacharge kwa invoice inavyoongea

Kwa mizigo ya kawaida Kampuni nyingi huwa wanacharge kuanzia Dola 12, 13 hadi 14.5 kwa kilo moja ya mzigo

Tufanye una Kampuni yako ambayo ina charge $12.5 per kilogram halafu umepata kilo elfu moja yani tani moja ya kusafirisha, kwa rate ya jana dollar 12.5 ni sawa na 30,250/= so utapiga hiyo 30,250 × 1000 (ambazo ndio kilo zako) = 30,250,000

Katika hiyo milioni 30 na laki 2 na nusu ndio unatakiwa hapo hapo utoe pesa ya Airways bill, Pesa ya ZBS, Pesa ya ZAT, Pesa ya TRA pamoja na gharama nyingine ili mzigo uweze kutoka china na ukifikie ofisini kwako hapa Dar

Tuanze na gharama ya Airways bill, Kusafirisha mzigo kwenye ndege tu-assume ni elfu 5 kwa kila kilo

(Nimeweka makadirio ya juu kwasababu haya ni mahesabu ya kwenye karatasi ila najua haiwezi kufika au kuzidi hiyo)

Sasa tutapiga 5000 × 1000 = 5,000,000 hivyo mzigo wako wa kilo elfu moja hadi unatua pale Airport ya Zanzibar unakuwa ume cost milioni tano, Mzigo ukishafika Airport kuanzia hapo sasa inakuwa ni kazi ya Agent kuanza process za kuutoa mzigo akiwa na Documents zote mkononi

Agent ataanza ku-Deal na ZAT ambao hawa unakutana nao Airport ya Zanzibar

ZAT wanadeal na Ethiopia Airways na Air Tanzania, mizigo yako ikishatua, wao ndio wanai toa kule uwanjani wanaileta kwenye Godown lao

Na kabla Agent hajaanza kufanya kazi yake kuna makubaliano baina ya Agent na Kampuni ambayo inataka kutolewa mzigo, makubaliano hayo ni ya kipesa

Ma-Agent wengi ili waweze kukutolea mzigo huwa wana charge 4,500 hadi 5,000 per kilo, Sasa Kampuni ikishakubaliana na Agent kwamba itamlipa Elfu 4,500 kwa kila kilo kutoka Zanzibar hadi kuufikisha mzigo Dar, Kampuni itakachofanya itapiga hesabu ya kilo zinazotakiwa kusafirisha kutoka Zanzibar na kufanyiwa clearing, Sisi si tulishasema Kampuni yetu ina kilo elfu 1, so tutachukua 1,000 × 4,500 = 4,500,000. so Kampuni itampatia Agent milioni 4 na nusu baada ya hapo kampuni haitatoa pesa nyingine yeyote hadi mzigo unafika ofisini Kwa maana ya kwamba katika hiyo milioni 4 na laki 5 Agent atalipia kuanzia usharu usafirisha na takataka zote

Kabla hatujajua faida ya Agent anayoipata tuanze na Kampuni kwanza

Katika milioni 30 na laki 2 na nusu ya Kampuni tulitoa milioni tano ya Airways bill na tukatoa milioni 4 na laki 5 ya Agent, hivyo mzigo kutoka china hadi kufika ofisini inakuwa imetugharimu 5,00,000 + 4,500,000 = 9,500,000

Kwahiyo mzigo hadi unakufikia ofisini kwako unakuwa umeugharamikia kwa milioni tisa na nusu. 30,250,000 - 9,500,000 = 20,750,000

Tunapata milioni 20 na laki 7 na nusu, lakini hapo kuna gharama hatujazitoa kwa kule upande wa China, Kuna gharama za kufanyia packaging mizigo hadi kuusafirisha kwenda Airport kwaajili ya kuja Bongo, so kwenye hiyo 20,750,000 tutoe hiyo laki 7 ya juu kwaajili ya shughuli hiyo (makadirio ya juu) inabaki milioni 20 Cash

Katika hiyo milioni 20 tutoe milioni 5 ya emergencies zozote zile tubaki na milioni 15 kama faida ambayo ni uhakika kupata pesa hiyo tena na zaidi kwasababu makadirio niliyoyapigia hapo ni ya juu sana

Na kumbuka hiyo ni hesabu ya tani moja tu kwa wiki, Mimi Binafsi wakati nimeajiriwa nilikuwa nakimbiza hadi tani 5 kwa wiki japo huwa sio Guarantee wiki nyingine nilikuwa nakimbiza tani 2 tu pekee, Sasa tufanye Kampuni yako ina uwezo wa kupata na kusafirisha tani hiyo hiyo moja tu kwa wiki, kwa hesabu ya milioni 15 ukizidisha mara wiki nne yani kwa mwezi total ya Maokoto yako ni milioni 60

Kwenye hiyo Milioni 60 hujalipa tu wafanyakazi pamoja Kodi ya Ofisi zote mbili ya China na ya Tanzania

Unaweza kuanza na wafanyakazi 11 tu, Manager, Accountant, Secretary, 2 Storekeepers na Mfanyakazi mmoja wa China ambaye ataratibu shughuli zote za kule, hao watano waliobaki wawe watu wa Sales

Kwa kuanza watu wa sales utawalipa mshahara kwa miezi mitatu ya mwanzo baada ya hapo utawalipa kama wanavyolipagwa kwa Commissions, Kampuni nyingi huwa wanalipa Tsh 500 per kilogram, Upande wa Clearing utachagua uajiri kabisa mtu au utatumia Agent

Faida anayopata Agent

Wakati nimeajiriwa nilishapiga hesabu huwa mara nyingi natumia 3,000 au 3,200 kwa kilo kuutoa mzigo Airport ya Zanzibar kulipia usafiri hadi kuufikisha mzigo Sealink na kuufikisha Dar Bandarini na kumalizana na TRA gharama zote hizo huwa sizidi Tsh 3,200 kwa kilo

Sasa piga 3,200 mara elfu moja kilo za mzigo 3,200 × 1000 = 3,200,000 then Chukua Ile milioni 4 na nusu toa hiyo milioni 3 na laki 2 (4,500,000 - 3,200,000) inabaki milioni moja na laki tatu, so 1,300,000 hiyo ndio pesa anayobakiwa nayo Agent kama akiweza kusafirisha na kufanya clearing ya kilo moja kwa 3,200, Au kama hiyo hesabu imekuchanganya unaweza kuchukua 4,500 - 3200 = 1,300 so elfu moja mia tatu ndio faida yako kwa kila kilo moja, Utachukua 1,300 utazidisha kwa kilo ulizo zifanyia clearing ambazo ni hizo kilo elfu 1 so itakuwa 1,300 × 1,000 = 1,300,000

Milioni moja na laki tatu ndio anayobaki nayo Agent kama kifuta jasho, lakini inaweza kuwa chini ya hapo au zaidi ya hapo inategemea na namna utakavyo deal na wale majamaa pale Bandarini

Na kwa upande wa kampuni faida yake haiwezi kuwa chini ya Ile milioni 15 tuliyoipata sana sana itakuwa zaidi ya pale kwasababu najua katika mizigo itakayosafirishwa kutakuwa na vitu kama simu, laptop nk (electronics) ambapo mizigo hiyo Charges zake ni tofauti kama nilivyosema hapo awali

Bei za kusafirisha Electronics mara nyingi zinachezea humu

PS - Usd 80
Simu - Usd 20
Tablet - Usd 25
Camera - Usd 35
Kid Tablet - Usd 15
Airpods - Usd 5 to 10
Laptop - Usd 50 to 55
Botton Phones - Usd 5 to 8
Goods with Battery - Usd 14 to 16

Nihitimishe kwa kusema kwamba hizi Air Cargo zinalipa sana sana, kama Ile Kampuni niliyokuwa nafanyia kazi nina uhakika yule Mzee kwa mwezi anakunja zaidi ya Milioni 100 kama faida na hapo tunadeal na China tu, Kuna Kampuni wanasafirisha mizigo kutoka Uturuki, China, Dubai, Europe na Marekani unadhani hawa watakuwa na Ukwasi kiasi gani?

Ukiachana na hawa wenye hizi Kampuni, Raia wengine wanaopiga mkwanja ni watu wa TRA na Maagent, kuna kajamaa nakajua pale Bandarini kana Land cruiser GXR ila kazini anakuja na Premio anajilia mema ya nchi, na hana muda mrefu kazini, hizo ni pesa za Dili,

Mimi mwenyewe kuna mzigo wa kilo 900 nilishautoa pale Bandarini bila kuukagulisha, ule mzigo nilitakiwa kuulipia 2,250,000 uzalendo nikauweka pembeni nikasambaza upendo kwa milioni moja, iliyobaki nikaweka mfuko wa shati, Uzuri mzigo nilitakiwa niupeleke kwa mteja moja kwa moja, so nilichokifanya nilizuga kwamba documents za mzigo nimemuachia mteja, na ubaya wa kuajiriwa ndio huo Documents ni muhimu kuonesha ofisini, Au kama unaelewana na Accountant unaweza kula nae dili

Hizo ni kama umeajiriwa lakini kama ni Agent wa kujitegemea mkishaingia makubaliano na kampuni jambo kubwa huwa wanataka uwafikishie mzigo wao salama na kwa wakati wao hawahitaji Documents za TRA sijui waanze kupitia mchakato mzima ulioufanya hadi unapitisha mzigo Bandarini wao hiyo sio shughuli yao, Sana sana labda utawapa karatasi ya release kwasababu hakuna haja ya kutaka kujua TRA mm nimechajiwa pesa ngapi,

Welcome to the world of $1 a day, if you make it good for you otherwise it's your fucking problems
 
Madini sana haya, kumbe hawa watu wa clearing and forwarding wanapiga hela sana?!

Hebu shusha nondo vizuri kuhusu clearing and forwarding agents company.
 
Back
Top Bottom