Kupinga wagombea huru, ni uamuzi wa "Kipumbavu"

......acha hasira na ma-emotions wewe!! kama ni mawazo yako na yako mwenyewe basi si ungebaki nayo mwenyewe?? nani alikuomba uyalete hapa??
kila mara unapoingiza Nyerere kwenye mazungumzo basi kwa taarifa yako ua una-compromise sana credibility yako!!! si amini kama wewe si mwana sisiemu.....huwezi kuipinga SISIEMU wakati unakumbatia Nyerere. Kama hiyo inawezekana basi haupo smart enuff kufanya hivyo na ndicho kisa hasa Bongo upinzani ni Ziro!!!.

wow! who is emotional now?
 
si ndio maana tuna forum!! kwani mimi nimelialia hapa kukosolewa??? si huyo "sugar daddy" wako ndio anaanza u-mayai hapa!!! kila mara ukitaka kutulazimisha kuwa nyerere ni saint....sisi "wapinzani wa kweli wa sisiemu" tutabisha kwa nguvu zetu zote!!! ipo kwenye damu......

duh! ukichukua muda kusoma utaweka emotions zako pembeni na utatumia kipaji cha rational mind ambacho natumaini unacho. Kuanza kuita watu "sugar daddy" hakufanyi hoja zako kuwa nguvu bali zinathibitisha udhaifu wako katika ulimwengu wa fikra. Na hilo la kubisha kwa sababu iko "kwenye damu" yawezekana ndio tatizo kwamba unabisha alimradi unabisha hata kama huna hoja.

Ili nikusaidie kupata mwelekeo mzuri jaribu kujibu swali hili:

"Je ni uamuzi wa serikali kupinga wagombea huru una msingi wa kikatiba, haki za raia, na haki za binadamu?". Acha emotions pembeni na tumia muda kufikiri swali hili kabla hujajibu. Na yes una uhuru wa kumnukuu mtu yeyote anayekubaliana na mawazo yako.
 
Hata mimi siamini Nyani Ngabu is riding on Mwnkjj's cocktails. He sounds tough some times. Siamini.

Kaka mimi ni equal opportunity defender (and sometimes offender)....hata wewe nitakutetea nikiona unashambuliwa pasipostahili.....
 
KUPINGA WAGOMBEA HURU SI UAMUZI WA KIPUMBAVU. Inategemea unazungumzia hii kwa maslahi ya nani, kutokuwepo kwa mgombea huru ni kwa manufaa ya CCM, once kukiwa na ruhusa kwa watu kuwa wagombea huru, hasa kwenye udiwani na ubunge hiyo ndio itakuwa mwisho wa CCM. Katiba imesha-provide opportunity ya kuiondoa CCM kwa hiyo hao wanaopinga sio wapumbavu wanajua kuwa ile style ya kuwashurutisha wanachama kwa kisingizio cha kusema "uamuzi wa Chama" au "msimamo wa chama" haitakuwepo tena. Sheria hiyo vile vile itauua uwezo wa viongozi au vikao vya CCM vinavyotumia hoja ya nguvu, kama kwenye hatua za kugombea nafasi za kugombea ubunge. Busara ya kuikataa iko hapo tu, serikali haina la kupoteza ispokuwa CCM ndio iko hatarini, hapo zitapigwa danadana zote kuhakikisha haki hii inaminywa.
 
According to the dataz ni kwamba ccm wanashinikizwa na upande wa Zanzibar kuikataa hii ishu ya wagombea binafsi, kwa sababu ni moja ya sharti la msingi la kwanza kuwekwa na Marehemu Karume, kwa Mwalimu, alipokuwa akiunganisha Zanzibar na Bara, na viongozi wa Visiwani huwa mara kwa mara wanawakumbusha viongozi wa juu wa bara!

Leo hii hoja ikisimama tu basi itakuwa ndio mwisho wa Muungano, majuzi Muungano umeponea chupu chupu kufa kule Butiama, kwenye ishu ya muafaka, sasa ccm bara ndio lazima wahahe kuzima ishu hii ya wagombea binafsi! ni kwa sababu ya kuogopa kufa kwa Muungano!
 
Hata kwenye ndoa kuna divorce.Kama muungano is more trouble than its worth then to hell with muungano.

Hii (private candidacy) ni basic human right.Muungano siyo basic human right.

Where are our priorities?
 
Mzee Mwanakijiji,
Mimi ni mmoja wa hao Wapumbavu lakini pamoja na Upumbavu wangu nakuomba unipe somo kidogo pengine huo Upumbavu unaweza kuwa ujanja wa kibongo bongo..

Mkuu kwana nitaanza na kuelewa kwa nini kumekuwepo na mfumo wa vyama vingi duniani.. Swala hilo halitokani na wagombea Binafsi hata kidogo isipokuwa linatokana na itikadi za vyama kutofautiana. Watu ama viongozi hujiunga na vyama hivyo kutokana na kile kinacho simamia..Na ndio maana tuna mrengo wa kushoto, Kulia kati Kulia na kadhalika..Vyma vyote hufunguliwa kwa sababu wana imani tofauti kisiasa na chama ama vyama vilivyopo..Ndi tumekuta vyama kama vya Green Party na kadhalika ambavyo sio mtu anayejitangaza isipokuwa sera za hicho chama kusimamia malengo fulani..
Tatizo langu kubwa kuhusu haki ya wagombea binafsi ni pale wanapojaribu kuendeleza siasa ambazo sisi tunaoishi nje tunafahamu zinawapoteza wananchi...Yaani wananchi kuchagua wagombea kutokana na sifa zao badala ya kutazama nini chama hicho kimekusudia kuwafanyia wananchi..Na kwa bahati mbaya uchaguzi uliopita ulikuwa mfano bora wa uchaguzi wa mgombea kutokana na sura ama mfuko wake..

Kama hawa kina Mtikila wangekuwa wamesimama kutafuta haki ya wagombeaji binafsi ambao watawekewa sheria inayohusiana na kuonyesha sera zao tofauti na vyama vilivyopo bila shaka nadhani inaweza kukubalika lakini tusikubali KUIGA tu ile haki maadam wenzetu Ulaya wanaitumia wakati wao tayari wamekwisha shiba kisiasa na wana upeo mkubwa wa mrengo na sera ambazo vyama vikubwa wameziacha nje..

Ni kweli CCM wanaogopa hili lakini at the same time tusiwataze CCM hofu yao zaidi na kusahau maslahi yetu sisi wenyewe. Haki zote hupokelewa kulingana na mazingira na zipo haki ambazo Ulaya zinakubalika lakini kwetu Afrika inabidi tuzitazame mara mbili mbili kama zinalingana na mazingira yetu hivyo hivyo sisi tunazo haki ambazo hazikubaliwi Ulaya, hii haina maana kuna mtu anakosea.
Kwa mfano, kuna baadhi ya states zinaruhusu ndoa za Wasenge lakini hawakubali ndoa za kiislaam kuoa mke zaidi ya mmoja. Ndoa za Mkeka au kupangiwa na wazazi zinakubalika kisheria India na Asia na ni Haki ya mzazi lakini hazikubaliki nchi hizi hata kama wapo wazazi wanaopanga ndoa hizi..
kwa hiyo, tujaribu kutazama kilke kinachokubalika kwetu badala ya kutazama sheria za wenzetu Kuiga mfumo ambao kwanza haulengi tofauti za kimrengo na sera..
Kama utakumbuka niliwahi sema kuwa hadi leo hii Ukimuuliza Mdanganyika yeyote nini mrengo wa CCM watakwambia hawafahamu, hizo sera zao ndio zinachanganya kabisa maana wao ndio wameshika leo hii dira ya Kitaifa iliyoanzishwa na mwalimu... UJAMAA na KUJITEGEMEA, kisha wao ndio wa kwanza kuzivunja na wananchi ama washabiki wake wanaona poa tu maadam wachezaji wapo..

Kwa hiyo mkuu nitarudia kusema pamoja na Upumbavu wetu mimi nadhani haki ya wagombea binafsi bado muda wake itakuja wakati wake kwanza tujenge demokrasia kwa maana yake halisi.. Vyama vyote ni lazima viwe na mrengo kisheria ili kuwawezesha wananchi wajipanga nyuma ya vyama hivyo badala ya kutazama sura gani zipo chama gani..Lakini kwa hali iliyopo sasa hivi, wananchi tunashabikia vyama kama vile Yanga na Simba, mpira mmoja kiwanjani..Sura za wachezaji, rangi za jezi ndio kielelezo kikubwa cha kushabikia..
Hivyo mkuu binafsi naona kama tutakuwa tunazidi kujifukia ktk kiza kikubwa cha vyama vyetu nchini hata kama kuwepo kwa wagombea binafsi ni moja ya silaha kubwa kuivunja CCM...Kama walivyovunjika KANU ya Kenya halafu watu wale wale waliokuwa KANU wamekimbilia vyama vingine na baadhi (mafisadi) kushika tena madaraka..
 
Mkandara ndugu yangu... kilichoitwa upumbavu siyo watu wanaopinga hoja ya mgombea binafsi; na mimi nitakuwa ninajichumia dhambi kuwaita watu hivyo. Kilichoitwa upumbavu ni UAMUZI wa kufuta haki ya raia kuchaguliwa. Mimi nikitaka kuwa diwani wa eneo letu na sitaki kujiunga na chama chochote kilichopo, na sitaki kuanzisha chama changu, lakini watu wanaamini naweza kuwaongoza baada ya kuwaambia Ilani yangu na wakaipenda na wakataka kunichagua niwaongoze, kwanini wananchi wa eneo langu wanyimwe haki ya kunichagua? Na kwanini mimi ninyimwe haki ya kuchaguliwa wakati kwenye kumchagua kiongozi sitakiwi ni lazima niwe mwanachama?

Unaonaje tuweke pendekezo kuwa kila anayepiga kura lazima awe mwanachama wa chama cha kisiasa ili kura yake ihesabiwe?
 
... kilichoitwa upumbavu siyo watu wanaopinga hoja ya mgombea binafsi; na mimi nitakuwa ninajichumia dhambi kuwaita watu hivyo. Kilichoitwa upumbavu ni UAMUZI wa kufuta haki ya raia kuchaguliwa...

Mtu aliye fanya uamuzi wa kuiba ni mwizi, aliyefanya uamuzi wa kuongopa ni mwongo, aliyefanya uamuzi wa kipumbavu ni mpumbavu. Hakuna 'kugawanya nywele' hapo.

Kama ambaye amefanya upumbavu sio mpumbavu nani mpumbavu, aliyefanya uasherati? Na muasherati atakuwa nani?

Makala yako ilikuwa controversial. Nyerere alisema hivyo bila kubanwa unavyobanwa wewe kwa sababu mwenzako hakuijua Demokrasia kama wewe, na kila mtu alikuwa anamwogopa. Kama kweli hukumaanisha na hupendi dhambi ya kuita watu wapumbavu, kama ulivyo dai, basi omba radhi. Vinginevyo simama na ulicho amini kwamba kufuta haki ya raia kuchaguliwa ni upumbavu, na aliyefanya upumbavu ni mpumbavu.

Lakini huwezi kuuma na kupuliza hapo hapo.

Naamini wewe ni bora kuliko Nyerere inapokuja kwenye kuelewa haki za Demokrasia. Mwalimu Nyerere nisingethubutu kumwambia asicho taka kusikia.

Ahsante.
 
basi seriikali ndiyo mpumbavu! kwani ndiyo iliyofanya uamuzi huo. Naomba radhi kwa mtu yeyote ambaye anadhania kuwa yeye ni sehemu ya serikali iliyofanya uamuzi wa kipumbavu. Ningesema kuwa na maoni ya kupinga ugombea binafsi ni upumbavu basi ningekuwa nimemtukana mtu mwenye maoni hayo.

Hii lugha ninaifahamu vizuri, na nikitaka kusema kitu ambacho nataka kumaanisha sina tatizo hilo. Labda tatizo langu ni kuwa baadhi ya wasomaji wangu wanasoma zaidi ya nilichoandika na kuniwekea maneno kinywani.

Nachagua maneno ninayotumia vizuri sana kama Mwalimu.
 
Kwa kweli inauma sana. Hii yote ni janja ya nyani ya CCM kuundelea kutawala lakini wanajidanganya. Hawa wanyang'anyi wa rasilimali zetu hawaoni mbele hata kidogo. Tutadaii haki yetu kwa kila njia inayowezekana. Tukishindwa tuyaambia Mawe na milima yatazungumza kuipigania mama yatu Tanzania anayebakwa na Mafisadi na CCM bila huruma. Aluta Continua M.M. Mwanakijiji.
Ndugu zetu huko vijijini tunawafikia kweli?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom