Uongozi Ngome ya Vijana ACT ni mtihani kwa Ndolezi Petro

Mngoreme wa pili

New Member
Feb 22, 2024
4
5
Ngome ya vijana wa Chama cha ACT Wazalendo itafanya mkutano wake kesho wa kuchagua mtu atakayekuwa mwenyekiti kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari wagombea wanne wamejitokeza kuwania nafasi hiyo miongoni mwao akiwemo binti wa mwanasiasa mahiri na mwanadiplomasia Riziki Shahari Mghwali Bi Ruqqaya Nasiri Mahmoud.

Wagombea wengine ni Abdull Nondo anayetaka kutetea nafasi yake na Julius Masabo anayewania nafasi hiyo kwa mara ya pili baada ya uchaguzi uliopita kushindwa

Nimezungumza na watu tofauti tofauti kujua uimara na udhaifu wa wagombea na mitazamo ya wapiga kura kwa wagombea hao wanne.

kwa asilimia kubwa wagombea watatu, Abdull Nondo, Julius Masabo na Ndolezi Petro katika udhaifu wao wa kiuongozi wanatajwa kuwa ni watu wa aina moja, kwamba ni watu wasioshaurika, na wenye ubinafsi na kujikweza (hapa wapiga kura wanataja kuwa kama wataamua kwenda na udhaifu huo mbora wao ni Abdull Nondo linapokuja suaalaa zima la kupigania maslaahi ya vijana na kuwa sauti yao.

Masabo anatajwa kuwa mtu mwenye kufichwa zaidi katika mbawa za viongozi kuliko kusimamia agenda za vijanaa huku Ndolezi akitajwa kutafuta vyeo kwa udi na uvumba kwa ajili ya kufikia malengo binafsi kabla ya malengo ya kitaasisi

kwamba tamaa yake kubwa ni kutaka kuwa mwenyekiti na kuwa na utambulisho huo hata kama masuala ya vijana hayatakuwa yakipata naafaasi nzuri ya kujadiliwa chini ya uongozi wake (kwamba hatoi uongozi).

Udhaifu mwingine wa Ndolezi unatajwa ni ule wa kutoamini kufanya kazi na watu wa visiwani kwa mitazamo kuwa hawana uwezo wa moja kwa moja.

wanaomtaja Ndolezi katika hoja hii wanasema wakati wa kukusanya maoni ya mabadiliko ya katiba hivi karibuni, mhandisi huyo wa maji alikuwa akifanya juu chini kuhakikisha nafasi ya kuwa na mgombea mwenza haipewi nafasi ndani ya chama kwa ngome zake zote.

Inatajwa sababu kubwa aliyokuwa akiitoa kuwa ni ubora wake wa kiuongozi unaweza kufifishwa na mgombea mweza kutokea visiwani kwa kuwa wengi hawana uwezo wa kusimamia maasuala ya bara.

kwamba baada ya hoja yake hii kushindwa kwa waliokuwa wakikusanya maoni ya katiba, alijaribu kuipenyeza kaatika katika vikao vya halmashauri kuu kabla ya viongozi na wajumbe wa kikao hicho kumzima na kumfanya atafute mhombea mwenza kwa shingo upande.

Uamuzi huo unatajwa kuwa umeshamuondolea nafasi ya kushindanaa kwa asilimia 75 kabla ya kuingia kaatika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Februari 29 mwaka huu.
 
Back
Top Bottom