Kupinga wagombea huru, ni uamuzi wa "Kipumbavu"

Kwaminchi,


Mkuu kwanza kumbuka kuwa hapa tunahoji sheria zetu iwe for or against.. ni mawazo ya kila mtu kutokana na utaratibu uliopo au utakao kuja. Kwa hiyo sheria tunaiweka nje kwanza na kutazama kile kinachotokea/kitatokea kwa kujenga hoja zetu..
Hata hivyo naomba kifungu hicho cha sheria (Katiba) kinachosema hivyo..

21.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67
ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya
kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki
katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya
Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa
nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi
waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia
utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
21
(2) Kila raia anayo haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu
katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomhusu yeye, maisha
yake au yanayolihusu Taifa.


Mzee Mkandara Ibara hiyo ndiyo kiini cha kesi ya Mtikila. Ndiyo maana mabadiliko ya baadaye ya sheria yalipoongezwa Mahakama iliyapiga chini mara zote. Tafadhali soma hukumu ya kina Jaji Manento ambayo imepangua hoja hizi kwa kina kwanini sheria ya mabadiliko ya Katiba ya 1994 ilikuwa ni kinyume na Katiiba.

Katiba haiwezi kutambua haki fulani halafu kuifuta ndani ya Katiba hiyo hiyo.
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu huwezi kutenganisha haki ya mtu mmoja mmoja toka haki wa jamii ni kwa sababu haki nzima inahusu jamii hiyo na kwamba matendo hufanywa na mtu mmoja mmoja lakini hiyo right huandikwa kwa ajili ya jamii nzima..

sawa...lakini haki kabla ya kuandikwa kwa ajili ya jamii nzima hutambuliwa kama haki ya kila mwana jamii.

Mfano chukulia haki ya kuishi, inahusu jamii yote lakini wapo baadhi ya watu ambao hukutana na matatizo (individuals) na ndipo tunapotumia kifungu cha sheria hiyo inayohusu jamii..

Hapa unathibitisha ninachosema kuwa kulinda haki ya jamii yote ni lazima ulinde haki ya mtu mmoja mmoja kwenye jamii hiyo. Kwani kuvunja haki ya mtu mmoja ni kuvunja haki ya jamii nzima. NI kwa sababu hiyo hatuwezi kukaa kimya mtu mmoja akiamua kwenda kumtia kisa mtu mwingine kwa kusema ni haki ya mtu mmoja tu imevunjwa hivyo tusubiri hadi jamii nzima ivunjiwe haki hiyo. Jamii isiyoweza kulinda na kutetea haki ya mtu mmoja itaweza vipi kutetea na kulinda haki ya jamii hiyo nzima?

Tukikubali kuwa serikali inaweza kufuta haki ya mtu mmoja kuchaguliwa tutaweza vipi kuhakikisha haki ya watu wengi kuchaguliwa inalindwa?

Nachosema mimi hakuna haki inayoandikwa kwa ajili ya mtu mmoja hivyo jamii nzima waikubali haki ya mtu huyo..Utaratibu huu ndio uliopigwa vita na ujio wa Demokrasia kwa sababu zamani Masultan ndio walikuwa na haki ya kutawala kisheria na kati yao waligombea vile vile within royal family hizo lakini wananchi hawakupewa nafasi ya kumchagua kiongozi. Wakafuatia Madikteta ambao kwa kutumia nguvu ya chama au Jeshi waliteua ama kuchagua kiongozi bila wananchi kuhusishwa pia..

Mzee tunapozungumzia hapa ni kuwa haki inapotambuliwa inatambuliwa kama haki ya mtu mmoja kwanza. Ndiyo maana tunasema "kila mtu ana haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake" na hatusemi "kila jamii au watanzania wote wana haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake". Maana yake, mmachinga na tajiri wote wana haki sawa na usawa huo unatokana wote kuwa moja, binadambu; na mbili raia.

Wafalmee na masultani hawakutambua haki sawa kwa wote; ni wao walijipa haki zaidi kwa minajili ya nasaba zao au "matakwa ya Mungu". Ndio maana Mapinduzi ya Ufaransa yalitokea kudai haki za kila mtu na uwezo wa wao kujichagulia wanayemtaka; ni kwa sababu hiyo mapinduzi ya Marekani yalitokea kupinga "haki ya mfalme" kutawala na kurudisha haki ya watawaliwa kuchagua wanayemtaka; na ni kwa sababu hiyo Mapinduzi ya Zanzibar yalitokea kupinga utawala wa Sultani kwa sababu ulitambua haki ya watu wachache badala ya kila mtu.

Hat ukitazama huko kwenye utawala uliokuja pingwa na Demokrasia utakuta kilichotangulia ni ile executive power kuwa chini ya royal prerogative au tuseme Jeshi na sio individual ambao hawana nguvu ya kutawala kama hawana executive power vested in.
Power zote zinakuwa possessed by the Title na sio individuals pamoja na kwamba ni individuals watakao tawala. Bila shaka kwa mtazamo finyu unaweza kushindwa kuona nachojaribu kusema hapa, lakini mkuu ni rahisi kabisa..

Hapa unachanganya "mtu kuwa na madaraka" na mtu kuwa na haki ya kuweza kupata nafasi ya madaraka hayo. Ni kweli kuwa madaraka (power) yako kwenye cheo na si mtu. Na kwahili unathibitisha jambo lile lile. Mbunge anayetoka kwenye Chama na Mbunge anayechaguliwa kama mgombea huru wote watakuwa na madaraka sawa. Mbunge anayeingia Bungeni kama mgombea huru ataapa kuilinda Katiba ile ile na kule Bungeni ataingia na kuzungumza na kupata kinda na madaraka yote kama Mbunge wa Kuchaguliwa.

Mfano mzuri ni "wabunge wa kuteuliwa" na wa "viti maalumu" Hawa hawakuchaguliwa na wananchi lakini kwanini tunawakubali kama viongozi wakati wananchi hawakuwachagua? Yaani tunakubali Rais atuchagulie kiongozi kuwa mwakilishi lakini tunawanyima watu wa Chunya nafasi ya kumchagua kiongozi wanayemtaka kwa vile chama chake hakikumkubali?

Wabunge huru hawatishii madaraka ya mtu yeyote isipokuwa wanatishia uhuru wa watu wengine kufikiri wao ndio "watawala halali" kwa vile wamependekezwa na chama fulani.

ndio maana nikasema ni haki ya kila mtu kuabudu dini unayotaka ndiyo sheria imetungwa kwa kuitazama jamii nzima ya binadamu lakini individuals ndio wanakutwa na majanga haya kila siku sheria ipo kuwa protect.

Mheshimiwa, hivi Mtanzania akiamua kutengeneza ugiimbi wake, na sadaka yake ya kuku akaenda kwenye mti wa mkwaju kutoa sadaka kwa mababu zake serikali inaweza kumkataza kufanya hivyo kwa sababu hajajiunga na dini fulani iliyoandikishwa vitabuni? Je Mtanzania anayo haki ya kwenda kuabudu ng'ombe wake bila kulazimishwa kumsalia au kumswalia kikristu au Kiislamu? Je serikali inaweza kwenda mahakamani na kusema "tumeona ili kulinda amani na utulivu kila mtu anayetaka kuabudu lazima ajiunge na dhehebu fulani au aanzishe dhehebu lake rasmi?"
Tukirudi ktk uchaguzi nitarudia kusema kwamba haki ya mtu binafsi bado kabisa wakati wake Kantazania kwa sababu hadi sasa hivi siasa zetu zinatupotosha zaidi. Siku tutakapo weza kusimamisha Demokrasia na vyama vikawa vinatazamwa kwa mrengo na sera zake na akachaguliwa kiongozi anayeonekana kuwa mbora ktk kuwasilisha sera hizo kwa wananchi hapo naweza kukubali watu binafsi wanaokuja na hoja tofauti kabisa na vyama hivi..Not now hasa nikiwaona wagombea wenyewe wanaotafuta ULAJI na hawana mpya kisiasa zaidi ya ahadi za kutupa Utajiri!

sasa tumekuwa na wagombea kutoka kwenye vyama hivi miaka karibu hamsini sasa, wametufikisha wapi? Hivi wale waliozembea maofisini, kuiba mali zetu na kuharibu utawala wa sheria si wanatoka kwenye vyama hivyo? Je kwa wao kuwa wanachama wa chama cha kisiasa vimetusaidia vipi sisi? Sera si wanazo, namba si wanazo? Imelisaidiaje Taifa.?

Hakuna haja ya kusubiri kwa muda mrefu kwani kama kimeharibika ni bora tukitengeneze. Wagombea wa vyama vya siasa ambao tunaosasa wanafungia milango walio nje ya vyama hivyo kwa sababu yawezekana wao ndio wanatishiwa zaidi na wagombea huru.

Lakini tunapozungumzia wagombea huru, hatuzungumzii wale wasio na vyama tu na hii ni point naona unairuka. Tunazungumzia hata wale wenye vyama lakini kwa sababu ya ufinyu wa nafasi au uhuru wa aina fulani wanashindwa kugombea kupitia vyama vyao lakini wananchi wanawakubali na wao hawataki ikuvikana vyama vyao.

Hebu fikiria kama Dr. Salim, Dr. Kigoda au Mzee Malecela angeweza kusimama kama mgombea huru kutoka CCM badala ya kulazimika kwenda Chadema au TLP na wananchi wakamkubali na akarudi kutekeleza sera za CCM kuna ubaya gani hapo.

Mfano mzuri ni Seneta Joe Lieberman wa CT ambaye chama chake kilimkana na kumtupa nje kwa sababu anamuunga mkono Rais Bush. Baada ya kutupwa na chama chake akajisimamisha kama mgombea huru (independent candidate) na kushinda kiti cha Useneta. Chama chake kikamuomba radhi na kumhakikishia kuwa wataendelea kumpa seniority yake kama atapiga kura na demokrats. Akakubali na sasa ingawa ni seneta huru lakini yuko aligned na Demokrats.

Kama Njelu Kasaka angeweza kugombea kule Chunya na kurudi Bungeni au Hassy Kitine au wnegin wengi walioenguliwa na vyama vyao si Bunge letu lingekuwa moto moto? Wangeweza kuchagua wapi wanataka kupiga kura chama tawala au upinzani na wangekuwa ndio wale wanaoweza kubadilisha mwelekeo wa upigaji kura Bungeni.

Kugombea huru ni jambo zuri, la Kikatiba na uamuzi wa serikali kuifuta haki hiyo ni uamuzi wa "kipumbavu" kama alivyosema Nyerere. (I know some people flinch when they see that name.. you know I had to do that..)

Mkuu bila kubisha sana ebu turudi nyuma kwenye shina la hii issue.. Nini maana ya KIONGOZI?..
Nauliza hivyo kwa sababu huwezi kujijengea jina la Mheshimiwa (Hon) kuongoza wananchi kwa utaratibu unaoutaka wewe..sheria na utaratibu hutazama the mass population ama title kisha huijengea sheria kuipa kinga ya kutoingia wasiokuwa na haki. Kwa maana hii Diwani , Mbunge na rais hawa wote ni Wa - Heshimiwa, hivyo utaratibu unatakiwa kulinda heshima hii kutolewa ovyo kwa mafisadi...

Kisha bado hujanijibu swali langu mkuu hawa wanaotafuta haki ya individuals kugombea Uheshimiwa wanashindwa kitu gani kujiunga na Upinzani ikiwa matokeo ya matunda ya kujiandikisha kwao hakutakuwa na tofauti kama wakiwa individuals.. Kama hawakubaliani na vyama vilivyopo then kwa nini wasituambie kwanza kile wanacho amini wao tofauti na vyama hivi..
Imean hii ndiyo inayomkuta Field Marshall Es na hata wewe wakati fulani yaani watu wanakupinga kitu lakini wao hawana jibu wala solution isipokuwa wanapinga tu ulichoamdika. Why? ati haikukaa sawa!
Sema basi usawa ni Upi? watu wanazunguka tuuuu, kumbe hata ukweli wa issue nzima hawana isipokuwa wanajaribu kudadisi zaidi upate kuingiwa hasira zaidi..[/QUOTE]
 
Mzee Mwanakijiji,
Hiyo ndio nayoizungumzia haswa kipengele cha mwisho kinachosema KWA KUZINGATIA..
kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania..

Mkuu hata Ukisoma Katiba ya China au Guinea Bissau utakuta imetangulia na usemi kama wenu isipokuwa hufungwa mahala na utaratibu. Leo hii China wanaruhusiwa watu waote kuingia uchaguzi/uteuzi lakini karibu kila mtu ni mwanachama wa chama tawala pamoja na kwamba sio lazima uwe mwanachama.
Lakini kulingana na mfumo wa Demokrasia China inayonekana hawana Demokrasia kwa sababu individuals wanaruhusiwa kuingia lakini mrengo wa Chama tawala ndio mrengo na dira ya taifa zima. Kukosekana sheria ya upinzani Kichama ktk mrengo ndicho kinachoondoa demokrasia pamoja na kwamba watu binafsi wanaruhusiwa kuingia chaguzi hizi..It's not who is against the governmet policies. Kwa upeo mkubwa hakuna watu binafsi kwa sababu wanatoka chama kimoja na wao Ubinafsi wameuweka kuwa ni kutokuwa kiongozi ndani ya chama. Hivyo wametenganisha raia kama ni wafuasi na ambao wanaangukia fungu la binafsi na wale walioko kwenye Power tayari (Udikteta) ndio wawakilishi wa chama, yet bado utafunwa na utaratibu na sheria zao.
Nitaruka nje kidogo ya mada hii na kutoa mfano mwingine ambao unahusu mfumo wa kiuchumi - FREE na Open market, kimaandishi utafikiria kwamba serikali haiweki utaratibu ambao bado unawapo control ya kila kinachofanyika. Hata nchi za Kibepari uchumi wa nchi hizo unakuwa controlled na serikali pamoja na kwamba wamiliki ni watu binafsi, policy zake hazijengwi na watu isipokuwa serikali na kitu cha kwanza hawatazami haki ya mtu huyo isipokuwa haki ya Taifa na wafanyabiashara wote hivyo kujenga sheria zinazokinga uvujaji wa haki hiyo.

Hapa unathibitisha ninachosema kuwa kulinda haki ya jamii yote ni lazima ulinde haki ya mtu mmoja mmoja kwenye jamii hiyo. Kwani kuvunja haki ya mtu mmoja ni kuvunja haki ya jamii nzima. NI kwa sababu hiyo hatuwezi kukaa kimya mtu mmoja akiamua kwenda kumtia kisa mtu mwingine kwa kusema ni haki ya mtu mmoja tu imevunjwa hivyo tusubiri hadi jamii nzima ivunjiwe haki hiyo. Jamii isiyoweza kulinda na kutetea haki ya mtu mmoja itaweza vipi kutetea na kulinda haki ya jamii hiyo nzima?
No mkuu sithibitishi usemi wako, kinachogomba hapa ni sheria kuiwezesha haki hiyo ifanye kazi.. Sheria inatazama haki ya jamii haitazami individuals.. Hivyo sheria hutungwa kwa sababu ya Jamii nzima tofauti na hoja yako inayotaka sheria itungwe kwa sababu ya individuals ambao hawaundi jamii..Ni hawa individuals wanaotaka kujiunga na Uheshimiwa, hivyo wanabanwa na taratibu.
Mtikila yupo mahakamani kujenga hoja ya kutafuta sheria ya individuals na sio jamii nzima hivyo ni lazima tuitazame haki hiyo kulingana na mazingira yetu. Haki ya jamii haiombwi ni dhahiri na sheria inapokataa haki hiyo jamii nzima huathirika hata kama imeombwa na mtu mmoja.
 
Mzee Mkandara,

Hiyo "kwa mujibu wa sheria" ndio mahakama ilichofuta kwamba hiyo sheria ni kinyume na Katiba. Serikali haiwezi na haina nguvu ya kufuta haki ya mtu kuongoza kwa sababu hataki kujiunga na chama fulani. Haki ya kuchagua na kuchaguliwa ni haki za msingi za Raia na serikali haina uwezo wa kufuta haki hiyo. Mahakama zetu zimeamua hivyo na hata mahakama ya rufaa tena nakutabiria mapema kuwa hata kusikiliza haitapoteza muda na kuacha uamuzi wa Mahakama kuu usimame.

Serikali haina nguvu au uwezo wa kufuta haki za jamii nzima kwa sababu tu hawazipendi.
 
Mzee mwanakijiji,
Hapa tunazunguka mbuyu mkuu, Utaratibu wa sheria hii unamhitaji mtaka haki kueleza kile anachokileta kwa wananchi..Unaruhusiwa kugombea nafasi yoyote ile isipokuwa kuna Utaratibu na sheria. Hizi taratibu na sheria ndizo msizozikubali kwa sababu mhusika hataki kufuata utaratibu uliopo wa kuwa na chama Title isipokuwa kutumia jina lake bila mwongozo wazi. hawa jamaa wanataka kuleta kitu gani?... hawana jibu isipokuwa right ya kuongoza! come on guys..
Vyama vina Ilani, mrengo sera na kuorodhesha yote wanayokusudia kuyafanya, huyu mgombea binafsi unataka akubaliwe kisheria kuingia uchaguzi bila kufuata taratibu na sheria ambazo zitakuwa wazi kwa wananchi...Tanzania ya leo tunahitaji sana sharia zinazokinga na kulinda demokrasia tunajaribu kuijenga. Mkuu sisi tunaijua KLH news ilosajiliwa pamoja na kwamba mmiliki ni Mwanakijiji na haipotoshi kitu wala sio kazi kubwa inayokukwamisha kuanzisha tovuti yako ama haki zote za uandishi.

Conclusion yangu ktk mada hii ni kwamba mnajaribu kuiondoa kabisa ile haki ya kwanza 21 (1) kuwa haipo kwa sababu ya taratibu na sheria zinazoambatana na kifungu hicho. Yaani mnachotaka ni kutokuwepo na sheria kabisa ama utaratibu ambao unamzuia/ruhusu mtu binafsi kuingia kama vile nchi hii haitakuwa na serikali.
Kwa hoja zenu ni sawa kabisa na kuhoji - Why tuna Political Parties wakati viongozi wetu ni individuals. Kwa nini isiwe mtu anagombea moja kwa moja bila kuwa na chama ambacho kinamfunga mtu ktk mrengo, ilani, sera na kadhalika..kwani upeo wa mtazamo wa haki hii unaishia kwa mtu mmoja.
I mean hata mtu kuzaliwa kuna utaratibu pamoja na kwamba kila mtu ana haki ya kuishi...misingi ya taratibu na sheria za uzazi ndizo hutungwa kumlinda mtoto, mzazi, nurse nahata Hospital hakuna haki inayosema tuache kila kitu wazi maadam kila mtu huzaliwa...
I don't know might be I'm missing a point here!
 
Ili kulinda haki ya raia kugombea ubunge bila sharti la kuwa mwanachama wa chama cha siasa na ili kuhakikisha vyama vya siasa vinabaki kama Asasi muhimu za demokrasia nchini, nimepeleka serikalini mapendekezo ya mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi na hivo kubadili aina za wabunge Bungeni. Mapendekezo ni kama ifuatavyo


• Bunge liwe na aina zifuatazo za Wabunge;

1. Wabunge waliochaguliwa kuwakilisha Mamlaka za Serikali za Mitaa. Mamlaka hizi sasa zitatamkwa na Katiba nazo ni Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji. Hivi sasa nchini kuna Mamlaka za Serikali za Mitaa zipatazo 124 kwa upande wa Tanzania Bara. Hivyo hapa tutapata Wabunge 124 wa kuchaguliwa moja kwa moja na wananchi. Katika kundi hili ni dhahiri wagombea binafsi wataruhusiwa hivyo itabidi Katiba na Sheria ya Uchaguzi ziweke masharti ya ushiriki wao. Rejea barua yangu ya awali kuhusu baadhi ya masharti.

2. Kwa upande wa Zanzibar Wabunge wa kuchaguliwa watokane na Wilaya za kiutawala zilizopo sasa. Hapa tutapata Wabunge 10.

3. Wabunge wa Mikoa ambapo kwa Tanzania Bara watakuwa ni sawa na idadi ya Wabunge wanaotokana na Mamlaka za Halmashauri za Wilaya ambao idadi yao itakuwa 124 kwa sasa. Kwa upande wa Zanzibar, ili kulinda matakwa ya Kikatiba kwamba idadi ya Wabunge wa Zanzibar isipungue 50 kama ilivyo sasa, Wabunge 40 watatokana na kundi hili la Wabunge wa mikoa. Mikoa itagawiwa Wabunge kutokana na uwiano ya wananchi waliojiandikisha kupiga kura katika Mkoa husika na mgawo huu utakuwa unarejewa kila baada ya miaka kumi. Vyama vya siasa vitagawiwa Wabunge hawa wa Mikoa kutokana na uwiano wa kura ambazo kila Chama kimepata katika uchaguzi wa Wabunge ndani ya Mkoa husika na kwamba Chama lazima kipate asilimia 5 ya kura au zaidi ili kugawiwa viti hivi. Katika kundi hili Wabunge wanaume na wanawake watakuwa ni sawa kwa sawa yaani nusu kwa nusu.


4. Wabunge wanawake ambao watakuwa ni asilimia 30 ya Wabunge wanaotokana na makundi matatu hapo juu. Mgawo wa Wabunge hawa utakuwa ni kwa mujibu wa mfumo uliopo sasa.

5. Wabunge 5 kutoka Baraza la wawakilishi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Spika kama si Mbunge.


• Ndugu Rais, kwa mapendekezo haya tutaweza kutoa uhuru kwa raia wa Tanzania mwenye sifa na bila kujali kama ni mwanachama au sio mwanachama wa Chama cha Siasa kugombea Ubunge na hata udiwani.

• Mapendekezo haya yanaangalia umuhimu wa Vyama vya Siasa kubakia nguzo muhimu ya demokrasia nchini. Kugawa viti vya ubunge kwa vyama kutokana na uwiano wa kura ambao Chama kimepata kutafanya Vyama vyetu vijiimarishe zaidi na kutoa sera bora zaidi ili kuwa na ushindani mkubwa wa kisera na kuifanya kila kura kuwana thamani maana kila kura itakuwa na thamani.

• Kwa mapendekezo haya tutakuwa na asilimia 44 ya Wabunge wote wanawake bila kujumlisha Wabunge wanawake watakaochaguliwa kutoka katika Mamlaka za Serikali za Mitaa moja kwa moja kama kina Mheshimiwa Balozi Getrude Mongela, Beatrice Shellukindo, Dkt. Zainab Gama, Jenista Mhagama nk. Hivyo tunaweza kufikia asilimia 50 ya Wabunge wanawake iwapo Vyama vya Siasa vitateua wagombea 24 tu kati ya 124 wa Mamlaka zilizopo sasa na kushinda.

• Kwa mapendekezo haya Tume ya Taifa ya Uchaguzi haitakuwa na kazi ya kugawa mipaka ya majimbo tena bali mipaka itatokana na Tangazo la Rais la kutangaza Mamlaka ya Serikali za Mitaa.

• Mapendekezo haya yanaondoa nafasi ya Rais kuteua Wabunge na badala yake Katiba ifanyiwe marekebisho ili Rais aweze kuteua Baraza la Mawaziri nje ya Wabunge ila wathibitishwe na Bunge.

• Demokrasia ndani ya Vyama vya Siasa itaimarika, hasa katika ngazi za chini na hususan ngazi ya Mikoa. Vyombo vya kidemokrasia ndani ya Mikoa vitakuwa na majukumu sasa ya kuchagua watu watakaopelekwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili wateuliwe kuwa Wabunge kufuatia uwiano wa kura za Chama hicho katika Mkoa husika. Pia Tume ya Taifa ya Uchaguzi itahakikisha kuwa Vyama vinapata wawakilishi wake katika Orodha ya Mikoa kidemokrasia kwa kutunga kanuni maalum kwa ajili hii na pia Tume yenyewe kusimamia chaguzi hizi pale inapobidi

• Ndugu Rais, ninakuomba uziagize mamlaka zinazohusika kuandaa mapendekezo ya mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi na kuita mjadala wa Kitaifa kupitia Asasi kama REDET ili kupata maoni ya Watanzania wengi zaidi na hivyo kuboresha demokrasia.


Ndugu Rais, ninaamini kuwa ni muhimu kufanya mabadiliko ya mfumo wa siasa kwa faida ya demokrasia ya nchi yetu kwa sasa na siku za usoni, hivyo ninaomba Serikali itafakari mawazo yangu haya.
 
Mzee Mwanakijiji, kama kawaida yako, umesema kweli tupu. Umejenga hoja isiyopingika: haki ya ugombea binafsi ni haki ya kikatiba na ya kibinadamu ambayo haikwepeki. Mwalimu Nyerere ambaye viongozi wa CCM wanadai kumuenzi, alishatoa wosia wake kuwa haki hii ya ugombea binafsi ni ya msingi katika demokrasia ya kweli, si ya mjadala ila ya kutekelezwa mara moja. Lazaros
 
Demokrasia inatengenezwa na watu na ukiniuliza mimi yawezekana tulikuwa na demokrasia kubwa katika maeneo wakati wa Nyerere kuliko ilivyo sasa. Kama Nyerere alikubali na kuheshimu matokeo ya Mbulu ambako mgombea huru wa TANU aliyesimama yeye mwenyewe baada ya Kamati ya Tanu kupitisha mtu mwingine kwanini usikubali kuwa hiyo ni Demokrasia? Si wangemuacha Njelu agombee kama mwanaCCM huru? Yaani ya Njelu ni Demokrasia na ya Chifu Swarat siyo?


Ukisoma makala nzima utaona kuwa hakuna mahali ambapo nimesema kuwa CCM au mtu yeyote hana haki ya kwenda Mahakamani kukata rufaa. Kwa vile umeona jina "Nyerere" na mawazo yako yameenda mbali zaidi basi umesoma kuwa nimesema CCM hawana haki ya kwenda mahakamani.

Hoja yangu ni ile ile, uamuzi wa kupinga wagombea huru/binafsi Tanzania ni uamuzi wa kipumbavu, hauna msingi katika Katiba n.k Na mahakama zimeshaamua hivyo kwa karibu miaka 15 sasa! Waende Mahakama ya Rufaa au wafanye uhuni waliofanya mwanzo wa kwenda kubadili sheria wakati kesi iko mahakamani.




Ukiiweka katiba sawa wewe na nani? Kama CCM ingetaka kuwa inatii mahakama ingeshatii zamani sana. Walibadili sheria baada ya kushtakiwa katika kesi ya Chavda ili kufanya serikali iwe vigumu kudaiwa, na walibadili sheria walipotakiwa kuruhusu wagombea huru. CCM hawatobadili Katiba ili watu wengine wanufaike.

tatizo langu ni la watu kutaka kila matatizo yao ya kushindwa kufanikiwa maishani kumtupia Nyerere. Hoja tunayoisimamia wengi ni ile ya kusema Nyerere alikuwa ni muungwana sana kuliko wenzake waliomfuatia katika urais!

Na kama nilimwelewa vizuri kwenye hotuba yake ya Mbeya yeye alisema wao walifuta sheria iliyoruhusu vyama vingi kuwepo na hawakufuta haki ya mtu kugombea binafsi kwenye katiba ya nchi

Kilichomshangaza yeye ni pale kisheria vyama vingi viliporuhusiwa lakini serikali ikatunga sheria ya kuzuia mgombea binafsi. Hapo ndipo alipoona ni jambo la kipumbavu na siyo haki kuondoa haki ya mtu kwenye katiba.

kwa mamneno mengine mwalimu alikuwa anasema kama mtu angeenda kuidai haki yake ya kikatiba ya kusimama kama mgombea binafsi (enzi za mfumo wa chama kimoja) basi mahakama ingempa kwa sababu kwenye katiba ilikuwa haikatazwi mtu kugombea binafsi kwa hiyo sheria ya chama kimoja ilikuwepo lakini katiba ya nchi yetu ilikuwa haikatazi mtu kugombea binafsi kama ilivyo sasa!
 
Mkuu Zitto,
Shukran sana kwa mapendekezo yako pamoja na kwamba binafsi naona kuna vipengele vinavyonipa shida kuwaelewa hasa pale tunapowapa wanawake nafasi sawa na wanaume kama sheria ama utaratibu hali katiba inasema KILA MTU anapewa nafasi sawa..Sioni sababu ya kuweka kifungu kinachotofautisha kati ya wanaume na wanawake ikiwa haki hii ni ya kila raia...
Nikirudi kwenye hoja yangu ndio maana nikasema taratibu na sheria huwekwa ktk kukinga ubadhirifu ama ukiukaji wa haki yenyewe..
Bado, hadi sasa hivi mku hamjanipa shibe ya hoja yangu na labda hapa nitaeleweka vizuri zaidi..
Mathlan, Mzee Mwanakijiji kanipa hoja inayosema hivi:- kila mtu ana haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake" na hatusemi "kila jamii au watanzania wote wana haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake". Maana yake, mmachinga na tajiri wote wana haki sawa na usawa huo unatokana wote kuwa moja, binadamu; na mbili raia.
Nachosema mimi ni kwamba anaipotosha point nzima ya Uchaguzi kwa sababu kutangulia kwa haki inatokana JAMII nzima kama vile unapojaribu kuwapa wanawake nafasi sawa na wanaume. Na ktk mtazamo wangu nimetazama haki hiyo hiyo kwa mtoto ambaye ana kila haki ya kuishi lakini kuna taratibu zinazoambatana na haki hiyo ikiwa ni pamoja Umri, Uzazi wa majira (China na kwingineko) au hata pengine utaratibu wa mtoto kuzaliwa ndani ya ndoa (dini na mila zetu), sioni kama utaratibu na sheria hizo zinaondoa haki ya mtoto kuishi isipokuwa kuboresha ama kukinga haki yenyewe. Nachoogopa mimi ni pale tunapoiga hizi haki hali mazingira yetu ni tofauti kabisa na nchi za wenzetu ambapo wao tayari wameisha boresha mfumo mzima wa wajibu kwa wazazi. Kama utabeba mimba nje ya ndoa bado wazazi watakuwa responsible na mtoto huyo kama vile mko ktk ndoa, mwanamme unayekimbia watoto utakamuliwa hadi mwenyewe uogope kutia mimba lakini mazingira yetu siku zote yamekuwa yakitazama upande mmoja wa wenye nguvu..na ndio maana tumeshindwa kujenga sheria na taratibu zinazoweza kuhakikisha haki ya mtoto badala yake tumejenga taratibu za kimila zaidi ktk mfumo mzima wa sheria zetu..
Binafsi nitarudia kusema kwamba wakati wa wagombea binafsi bado kabisa kwa sababu hata hiyo demokrasia yenyewe haijasimama. Na kama ulivyopendekeza nitapenda kufahamu Nani atalipia gharama za kumsimamisha mgombea binafsi? Kumbuka katika maelezo yako umesema kutakuwa na viti 124 hivyo hapo tunaweza kuwa na wagombea binafsi zaidi ya 124 kwani hakuna limit ya wagombea binafsi na kama itakuwepo basi tutarudi kule kule kwenye kunyima haki watu kugombea uongozi...Why put a limit number!..
Na kama hawa wagombea binafsi watagharamia chaguzi hizi huoni kwamba tunakaribuisha Takrima?.. Mazingira yetu Takrima hutolewa na viongozi kuomba kura za wananchi wakati wenzetu Takrima kwa tafsiri yake hutolewa na wananchi kumwezesha mgombea kumudu matumizi bila kuomba kurejeshewa fadhila yao... wanachotazama ni kile mgombea huyo amesimamia...
Je, katika mazingira hayo kuna utaratibu gani ama sheria zipi zitakazowekwa kulinda haki hii ya wagombea binafsi ambao hawana mrengo...
 
Mzee mwanakijiji,
Hapa tunazunguka mbuyu mkuu, Utaratibu wa sheria hii unamhitaji mtaka haki kueleza kile anachokileta kwa wananchi..Unaruhusiwa kugombea nafasi yoyote ile isipokuwa kuna Utaratibu na sheria. Hizi taratibu na sheria ndizo msizozikubali kwa sababu mhusika hataki kufuata utaratibu uliopo wa kuwa na chama Title isipokuwa kutumia jina lake bila mwongozo wazi
.
[/COLOR][/B]

Mukulu mkandara, Kinachogombewa hapa ni sheria kukutaka kupiga kura bila chama lakini kupigiwa kura chama. Ningekuelewa kama ugekuja na hoja kwamba sheria ibadilishwe kwamba kila anayepiga kura lazima pia awe mwanachama wa chama cha siasa. Isiwe mimi nisiye na chama ninahaki upande mmoja tu na upande mwingine sina haki. Kumbuka sheria hiyo hiyo inazuia kunilazimisha kuwa mwanachama wa chama cha siasa kama sitaki kuwa mwanachama.
Vyama vina Ilani, mrengo sera na kuorodhesha yote wanayokusudia kuyafanya, huyu mgombea binafsi unataka akubaliwe kisheria kuingia uchaguzi bila kufuata taratibu na sheria ambazo zitakuwa wazi kwa wananchi..
.

Kwani hizo ilani na sijui unazoziita sera (ambazo kwanza hazitekelezeki)zinatoka mbinguni? si zinatungwa na watu? nani alikudanganya kuwa nikisimama mimi mchukia fisadi siwezi kuwa na sera zangu? na ilani yangu ya uchaguzi? Si kweli kwamba sera ili iwe sera lazima iandikwe na chadema; ccm; cuf n.k. hata hizo zinazoitwa sera huko kwenye vyama vyenu tunazitunga sisi akina mchukia fisadi. Na hii hoja yako siku zote wameitumia ccm kuzuia upinzani binafsi

Tanzania ya leo tunahitaji sana sharia zinazokinga na kulinda demokrasia tunajaribu kuijenga
.

Kwa hiyo unadhani kwa kuzuia ugombea binafsi ndio unalinda demokrasia? demokrasia maana yake ni hiyo kweli? demokrasia maana yake ni kutoa uhuru wa wengine kutoa mawazo na maamuzi yao yakaheshimiwa.

Yaani mnachotaka ni kutokuwepo na sheria kabisa ama utaratibu ambao unamzuia/ruhusu mtu binafsi kuingia kama vile nchi hii haitakuwa na serikali.

Huu ni upotoshaji ulio dhahili kwani kukiwa na mgombea binafsi kunazuia kusiwe na sheria? Hapa linalopingwa ni kuwalazimisha watu wawe na vyama vyenu hivyo visivyo na tija yoyote vinavyoishia kula ruzuku na kuendeleza ufisadi kwa kutumia ruzuku hiyo hiyo.

Kwa hoja zenu ni sawa kabisa na kuhoji - Why tuna Political Parties wakati viongozi wetu ni individuals. Kwa nini isiwe mtu anagombea moja kwa moja bila kuwa na chama ambacho kinamfunga mtu ktk mrengo, ilani, sera na kadhalika..kwani upeo wa mtazamo wa haki hii unaishia kwa mtu mmoja.

Waitu, hakuna ambaye anazuia vyama vya siasa kaatika hoja hii; sijui kama umeelewa vizuri hoja yenyewe ambayo hata mungekwenda katika mahakama ya mbinguni ruling ingekuwa hiyo hiyo. Hapa ni haki ya mtu kuchaguliwa kuwa kiongozi wa watu bila kulazimishwa kuwa mwanachama wa chama chako ndicho hoja inayozungumzwa. Wewe gombea kwa chama chako; mimi mchukia fisadi nigombee kama mchukia fisadi. Na wote twende kwa wananchi na hizo hoja zetu za ushawishi tunazoziita sera na ilani sijui; na atakayekubaliwa na hao wananchi basi na awe kiongozi wao! BASI. Shida iko wapi???
 
Mkuu Zitto,
Binafsi nitarudia kusema kwamba wakati wa wagombea binafsi bado kabisa kwa sababu hata hiyo demokrasia yenyewe haijasimama. Na kama ulivyopendekeza nitapenda kufahamu Nani atalipia gharama za kumsimamisha mgombea binafsi?
kumbuka kwamba ni lazima sheria zibadilishwe ili kuweka miongozo kama hii. Na kwa kweli itasaidia sana kuainisha jinsi ya kugharimia uchaguzi na hata JMK kesha lizungumzia hili. Maana hata leo tuseme ukweli wagombea wote ni kama wanajigharimikia tu kwa pesa zao wenyewe? hizi pombe na pesa zinazogawiwa huko vijijini na mijini kama karanga wakati wa uchaguzi kwani ni vyama ndiyo hugharimikia?.Na sasa tukae tupange katiba yetu na tuainishe mambo hayo tuyatakayo na si kusema oh demokrasia yetu bado, kwani twasubiri malaika gani kutokea kutufanyia demokrasia uitakayo mkulu? Kwa upande wa Zitto yeye katoa maoni yake tu kama rasimu, na wewe Mukulu Mkandara toa rasimu yako tuchague kilicho bora tukubaliane tuweke sheria nzuri za kutupatia viongozi safi.
Je, katika mazingira hayo kuna utaratibu gani ama sheria zipi zitakazowekwa kulinda haki hii ya wagombea binafsi ambao hawana mrengo...
Maoni hapa yapo hapo juu
 
CCM kweli wamekuwa tambara bovu, kuna umuhimu gani wa kupoteza pesa ya walipa kodi kupinga/kufungua kesi ya mgombea binafsi? Wanaogopa nini? Ukiona chama kinachoongoza kinaanza kuweweseka namna hii basi ujue Dua la kuku limempata Mwewe.
 
Mzee Mwanakijiji,
Duh, hili swali litachukua kurasa nzima kulieleza na binafsi sielewi msingi wake kwa sababu mimi naelewa tunashindwamkuelewana...

Kwa kifupi nitasema kwamba HAKI ni ufunuo wa kuheshimu msingi wa usawa na uvumilivu katika Jamii ambayo kila mtu anapewa uhuru na nafasi kisheria ama kihisia ktk kujenga jamii yenye nguvu.

Hapa naweza jaza kitabu kizima kuilezea haki hiyo isipokuwa vizuri nirudi pale tunapogongana. Binafsi naamini kabisa kwamba lazima kwanza u identify Jamii inayohusika (entitled to) kupewa haki hiyo iwe binadamu wote, wanyama, Wasenge, wanawake, wanaume, watoto na kadhalika..
Kisha kila mhusika (MTU) wa fungu hilo hutegemea kutendewa haki hiyo na kila MTU aliyemo ktk mazingira ya kundi hilo hivyo sheria mara zote huwa zinalenga KILA MTU, nje ya kundi hili kuheshimu uhuru na nafasi ya wahusika ktk kundi hilo, hivyo mara nyingi sheria za haki hizi hutungwa kwa walioko nje ya kundi hili wazifuate na kusiheshimu.

Kwa hiyo kila unaposema kuwa HAKI hutazama kila mtu na haisemi JAMII kama ulivyonukuu huko nyuma, huwa nashindwa kukuelewa wala kukufahamisha vizuri kwa sababu wewe umeegemea sana kwa wale wanaostahili ukasahau kwamba makundi yote mawili yaani wale wanaostahili kupata haki hiyo na wale wasiostahili ama wako nje ya kundi la wastahili sote KILA MMOJA wetu anatakiwa kuzifuata. Aidha iwe kuzipata (obtain) amakukatazwa (refrain)..
Hivyo basi Application ya sheria huwa ni individuals lakini malengo ya haki nzima huwa ni kwa JAMII inayohusika....
Mkuu, hata wale Masultan na Malikia walikuwa na HAKI ya Kutawala kulingana na mtazamo wa enzi hizo na sheria ziliandikwa kuwapa haki hiyo familia za hao Masultan..
Kwa hiyo hili neno haki lina mapana ambayo mimi na wewe hatuwezi kuya cover yote...Muhimu tufahamishane kile tunachozungumzia hapa kwani tukienda nje zaidi ndio tutazidi kujipoteza.
Mimi Kama Muislaam (Jamii Islaam) nina HAKI ya kuoa wake wanne hivyo jamii ya kiislaam ita heshimu haki hiyo kisheria lakini sio lazima Mkristu aikubali haki hiyo kuwa ni haki...
Utata unazidi kujitokeza ktk neno hili HAKI.
Tukimaliza hapo nadhani tutaelewana..
 
Mzee Mkandara unaogopa nini kwenye hoja ya mgombea binafsi? Hizo sera za vyama vyetu vya siasa zinatekelezwa? Maisha Bora kwa kila Mtanzania ni mojawapo ya sera za Chama cha Mafisadi je vinatekelezeka?
Kwani mgombea binafsi hawezi kuja na sera zake. Kwani sera ni lazima itugwe na chama? Hivi wewe mkandara huwezi kutunga sera zako na kuzipeleka kwa wananchi na wakazikubali?
 
Msesewe,
Mkuu labda hujanielewa vizuri, binafsi siogopi wagombea binafsi isipokuwa nimetazama hasara zake kwa taifa changa ambalo halina demokrasia kutaka kuingia maji marefu ya bahari wakati hata ya mtoni yanatushinda..
Labda nipe fursa nizungumze mengi ambayo kama mimi ningekuwa CCM basi bila shaka ningelikubali mfumo huu mara moja...
Kwa nini basi nasema hivyo..
Wagombea binafsi mara nyingi huwepo kuvunja nguvu za vyama na kwa mtazamo wangu muathirika zaidi atakuwa mwananchi, kisha vyama vya Upinzani na mwisho CCM..
Kwa hali ambayo tupo sasa hivi CCM ni King Kong ambaye kuanguka kwake kunategemea nguvu ya ajabu sana. Wagombea binafsi nina hakika watatoka vyama vya Upinzani zaidi ya CCM kwa sababu CCM ni shirika kubwa, mafia wasiokubali kushindwa.. Natazama kama Freeman akisimama Chadema, Dr. Slaa na ChaCha wangwe wanaweza kusimama binafsi. Umoja wa Wapinzani uliotegemewa kujengwa utakosa mshikamano kwa sababu kama mimi nilikuwa nigombee Ukerewe kwa tiketi ya vyama hivi vya Upinzani, nitapambana na mtu yeyote atakaye chaguliwa dhidi yangu na wengie walioachwa watagombea kwa tiketi hii.. Hivyo vita vitakuwa kati yetu kubomoana kwanza. CCM Mkuu tatizo lao kubwa ni hawa Mafisadi na I dare to say hakuna mtu toka CCM (Sio Salim wala Warioba)ataweza kusimama nje peke yake kwanza wazee vijana ndio kabisaaaa hawezi kusimama nje wakashinda bila nguvu ya dola - Mugabe stlye.
Viongozi wao wote wanafahamu hili na hata kama wapo watakao toka na kugombea nje kama wagombea binafsi, mafia ya CCM itawanyima fedha, watakosa UALAJI waliokuwa nao sasa hivi.. Hivyo tunachotegemea ni wale walioshindwa chaguzi za ndani ya chama kujitokeza..
Binafsi siamni kama watajitokeza kwa sababu CCM ni Mafia, wameshindwa kusimama Bungeni against UFISADI kweli wataweza kusimama nje ya CCM hali kisheria Bunge linawapa uwezo mkubwa sana kutoa maoni yao?..
Nguvu ya wagombea binafsi itaondoa umoja wa wananchi kuchagua kiongozi anayefaa chini ya mwongozo (chama) fulani ambacho wengi wetu tunakisubiri na hawa watakuwa responsible na kuwajibika kwa pamoja kuhakikisha mageuzi haya ya Kiuchumi yanapatikana hasa kuondoa Ufisadi.
Binafsi naishi huku na nimeona matatizo ya kuishi kama watu binafsi badala ya kujipanga nyuma ya Community yako. Wapo Watanzania wengi ambao kama ndivyo tulivyo hawapendi kujipanga nyuma ya Community zao na pengine frustration zao zinatokana na kuwa sisi kama viongozi wetu nchini vyama hivi huendeshwa kama serikali yetu..Hivyo hujikata wakaishi nje ya jumuiya zetu lakini tatizo huja pale wanapopata matatizo.. Utasikia la Mgambo kuchangisha fedha na kadhalika, lakini kwa ujumla wake ukitazama maisha ya Watanzania nje ni duni sana ukilinganisha na mataifa mengine ambayo Jumuiya zao zimesimama.
Kwa hiyo, mfuumo mzima wa kila mtu na mzigo wake ni chachu ya maendeleo ya Mtanzania na hakika wagombea binafsi ni moja ya mgawanyiko huo ambao lengo lake ni KUTAWALA sio kupata viongozi wanaostahili kutuongoza.
nachosema mimi ni kwamba TIME will come ambapo tutaweza kufikia kuwa na wagombea binafsi lakini sio leo wala kesho..
 
Nguvu ya wagombea binafsi itaondoa umoja wa wananchi kuchagua kiongozi anayefaa chini ya mwongozo (chama) fulani ambacho wengi wetu tunakisubiri na hawa watakuwa responsible na kuwajibika kwa pamoja kuhakikisha mageuzi haya ya Kiuchumi yanapatikana hasa kuondoa Ufisadi.
Binafsi naishi huku na nimeona matatizo ya kuishi kama watu binafsi badala ya kujipanga nyuma ya Community yako. Wapo Watanzania wengi ambao kama ndivyo tulivyo hawapendi kujipanga nyuma ya Community zao na pengine frustration zao zinatokana na kuwa sisi kama viongozi wetu nchini vyama hivi huendeshwa kama serikali yetu..

Mkandara, can you confirm to me that we are now united? What makes you think there will be division if private candidates were allowed to run, just thinking or.... Unajua kuwa sasa hivi kuna baadhi ya sehemu ukichagua mgombea wa CCM au ukichagua wa chama kingine unakuwa kama adui? Kwenye situation kama hii, don't you see private candidate ataunganisha watu badala ya kuwagawa?

Tumekuwa nyuma ya community ya CCM kwa miaka mingi, what have we got? Ukitumia experience ya huko uliko sina hakika kama inaweza kuleta matokeo unayodhani inaweza kuleta, realities za hapa ni tofauti kabisa. Na CCM ya 2005 mpaka sasa iko tofauti kabisa na ile ya 1977.

Umeona wazi kabisa issue ya Radar, EPA, Import support, Ndege ya rais, BOT towers etc etc wizi wa wazi umefanyika, where is that collective responsibilty you are talking about. au unazungumzia collective responsibility ya kujilinda kutokana na makosa. Wabunge wa CCM wameburuzwa karibu wote wakubali kuwa EPA iishe kimya kimya. Kisa wanatakiwa kuwa na msimamo wa Chama, don't you see kama zaidi ya nusu ya wabunge wangekuwa private hili lisingepita kiujanjaujanja.
 
2.JPG


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge) Bw. Phillip Marmo (pichani) amesema kuwa serikali haitokaidi uamuzi wa Mahakama kuhusu suala la wagombea binafsi endapo Mahakama ya Rufani itasisitiza kuwa waruhusiwe kwenye uchaguzi mkuu ujao kama ilivyoamuriwa na Mahakama Kuu mwaka 2005. Hata hivyo, Bw. Marmo amesema kuwa kutokana na mchakato wa maandalizi ya uchaguzi mkuu kufikia mbali endapo msimamo wa mahakama utakuwa ni ule ule basi itabidi uchaguzi mkuu uahirishwe ili kuruhusu utaratibu wa kubadili Katiba na kuwezesha wagombe huru na binafsi kushiriki kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu.

Pamoja na hilo Bw. Marmo amedokeza kuwa endapo itabidi Katiba ibadilishwe basi kuna uwezekano kuwa suala la mgombea binafsi litarudishwa kwa wananchi ili liamuliwe kwa kupitia kura za maoni. Akizungumza na KLHN International ambacho ni kituo cha Watanzania kirushacho matango kupitia mtandao wa Intaneti Bw. Marmo alisema kuwa hata hivyo kwa wakati huu suala la kura za maoni halipo “kwani tutavuka huo mto tukiufikia”.

Kuhusu kile ambacho kinaonekana kuwa ni mgongano kati ya serikali na mahakama kuhusu suala la mgombea binafsi Bw. Marmo alisema kuwa hakuna mgongano wowote isipokuwa hivi sasa haupo muda wa kutekeleza uamuzi wa mahakama akidai kuwa rufaa iliyokatwa na serikali ilisababisha uamuzi wa awali usitekelezeke. Bw. Marmo alitumia mfano wa adhabu ya kifo ambapo rufaa ikikatwa basi adhabu ya awali ya kunyongwa haitekelezwi hadi rufaa iamuliwe. Hata hivyo alipoulizwa kwa kutumia mfano wa kesi ya Nalaila Kiula (aliyekuwa Waziri wa Ujenzi) na ile ya kina Nguza Viking ambapo wote licha ya kukata rufaa bado waliendelea kutumia adhabu zao Bw. Marmo alidai kuwa “kesi hizo ni za mazingira tofauti”.


SIKILIZA MAHOJIANO:

INLINE: Bonyeza Play

[mp3]https://www.jamiiforums.com/downloads/mahojianonamarmo.mp3[/mp3]

au

 
Mkuu Mzee Mwanakijiji Thanx for a Qulity Sound! Tunasubiri hayo mahojiano. Big Up
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom