Kupata Visa ya kuja Tanzania ni kazi kweli kweli, Uhamiaji na Mambo ya Nje mnamkwamisha Rais

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Nimepata taarifa kwa rafiki yangu mmoja kwamba yeye na wenzake walipanga Tanzania lakini wanatakiwa kulipia Visa, baada ya kufungua mtandao wa Uhamiaji wanashindwa kupata huduma kila wakifanya kuomba wanapata error na muda wao wa likizo unakatika. Mimi mwenyewe nimejaribu kufuatalia nimekwama nadhani website haifanyi kazi au Kuna link ambayo labda wamebadilisha.

Kibaya zaidi mawasiliano yao ni TTCL na ukipiga namba haifanyi kazi, kwa mazingira haya unajiuliza hizi huduma za mtandao Tanzania zinaubora. Website inayotumiwa na watalii inapotezaje mawasiliano kwa muda wa mwezi kila siku inashindwa kufanya kazi hadi umalize kuomba visA. Je wizara ya mambo ya nje kwanini isitoe Tangazo kupitia Ubalozi wetu huko nje kwamba mtandao wao unashida ili watu waombe kwa kufika ubalozini?

Wanaohusika kwanini wanashindwa kutoa public notice pale kunapokuwa n tatizo? Mgeni akijaribu kuomba visA akakwama anajaribu website nyingine ya nchi nyingine je atupotezi watalii? Mimi nimepta taarifa za huyu ndugu zangu je wangapi wanapata shida?

Uhamiaji, mambo ya nje na utalii rekebisheni haya
 
Aliyeturoga watanzania sasa hivi ni marehemu!
Ukute majamaa yao ya IT yapo yanaangalia "ze utamu" huko!
Ndio maana TCRA wamefunga hizo website maana watumiaji wakubwa ni watumishi wetu!
 
Kama kwako siyo mama kwetu siye ni Mama, mzazi na mlezi. Urais si zaidi ya mzazi. Tunajadili kukuza mapato ya nje na hujuma fupifupi wewe unaleta maswali mchundo, tulia huko acha wananchi tujadili hoja

Eti wanaangalia ze utamu....inaweza kukuta hata IT awajui kwamba mtandao unasumbua. Maana mtu unaambiwa amejaribu kuomba VISA zaidi ya wiki sasa anapokelewa na error Hadi anajiuliza hii nchi ni maskini kiasi gani?
 
Kwa VPN inafunguka vizuri, aliegundua vpn noma sana
 
Kimsingi haya mambo yanakera kweli, yaani karne hii ya 21 lakini bado tunaishi na kutoa huduma kijima. Kweli TZ tunasafari ndefu.
 
Kama kwako siyo mama kwetu siye ni Mama, mzazi na mlezi. Urais si zaidi ya mzazi. Tunajadili kukuza mapato ya nje na hujuma fupifupi wewe unaleta maswali mchundo, tulia huko acha wananchi tujadili hoja

Eti wanaangalia ze utamu....inaweza kukuta hata IT awajui kwamba mtandao unasumbua. Maana mtu unaambiwa amejaribu kuomba VISA zaidi ya wiki sasa anapokelewa na error Hadi anajiuliza hii nchi ni maskini kiasi gani?
Tatizo la utumbo mkubwa Ni kubwa Sana nchini.
 
Uhamiaji wanazungua Sana, Toka wamwite mwanangu wa kumzaa SARATONJO ndo niliona kuna binadamu wakivaa uniform wanakuwa wanajiona Kama ulimwengu wa Kwanza. Natafuta maana halisi ya saratonjo siku nikipata maana yake lazima ntawashtaki kwa kumdhalilisha binti yangu kisa ni mweusi na anaomba kwenda kusoma nje. Mbele yangu Kama mzazi wanamtania mwanangu "wewe si saratonjo Kama masaratonjo wengine?" Passport uwezi kupata tafuta shule hapa usome la sivyo tafuta kazi ya kufanya.....binti yangu Hadi leo analalamika kwa udhalilishaji uliofanywa na afisa wa kiume Tena Mwenye nyota mbili ambaye tuliamini ni msimamizi wa wengine.

Kwa mentality zile zakuona watu weusi hatupaswi kusafiri nje naamini Hawa watu hata Mfuno wao visa ukigoma awawezi kushtuka maana wao wanaamini ni mabosi wa nchi hii.

Unaenda na binti kwa huyo anayeitwa mkuu wa pasipoti unamwambia binti yangu ametimiza masharti ya kisheria yakupata pasipoti nayeye anarudia kumtukana binti yangu saratonjo, na yupo ofisini kuhudumia wananchi then ukiwa mkali unaambiwa Waziri kaagiza mabinti wasipewe pasipoti.....unawauliza hivi mabinti wa kihindi mnawaludisha? Wasomali mnawaita saratonjo? Waalabu mnawanyima pasipoti? Au weusi sisi ndani ya nchi yetu ndio mnaona manyani kwa sababu wapole au wajinga?

Ubaguzi ubaguzi, na kwa taaarifa yao nimeshaandaa picha za wale wote waliomdhalilisha mwanangu, nimefanya utafiti wa unyanyasaji wa watoto wa kike wanopata kupata pasipoti ambapo wahindi, waalabu, wasomali na wazungu wao hakuna anayesumbua na awapangi hata foleni wanaenda emergency kwa mkubwa wa pasipoti nakuandikiwa vimemo. Nakamilisha ntamtumia Waziri atuambie anatumia sheria gani kukataza watu wenye ngozi nyeusi wasipate pasipoti?

Lakini pia binti yangu ntamwongoza kwa sababu alirekodi mazungumzo yote ya maafisa hao basi awafungulie mashtaka tukipata maana ya saratonjo even if itakupa code zao.

Nina hasira Sana na wapumbavu wachache wanoacha kusimamia sheria wakaangaika kusumbua Watanzania. Kibaya zaidi unawaambia pokeeni maombi yangu mniandikie kwamba mtoti huyu apati pasipoti kwa sababu anakwenda kujiuza wanakataa hata kupokea maombi eti rudi kakae na mwanao asome hapa huna pesa kwana hata huyu siyo mwanao unazuga tu........majibu mabovu. Viongozi awasikilizi na wadogo hivyohivyo. Hasa subirini tumalize kukusanya tasrifa za mabinti wanaokataliwa tumpe Waziri au hata kurusha hapa jf ndo mtatujua tuone Kama mtapona.

Mnamkatalia binti yangu mnamuita saratonjo lakini nampa elfu hamsini mtu kibandani nje anatumia less than 30mnts binti yuleyule kwa siku inayofuta anapata pasipoti ......huu mfumo wenu tunaendelea kuufanyia kazi posta na kurasini soon ntatupia hapa picha za vishoka mnaowatuma, maafisa wanaotuitia binti zetu saratonjo na wakubwa zaao ambao wanadai wametumwa na Waziri wanyime mabinti weusi pasipoti lakini wawape wenye rangi Tena kwa upendeleo mkubwa wakutopanga foleni.
 
Eti wanaangalia ze utamu....inaweza kukuta hata IT awajui kwamba mtandao unasumbua. Maana mtu unaambiwa amejaribu kuomba VISA zaidi ya wiki sasa anapokelewa na error Hadi anajiuliza hii nchi ni maskini kiasi gani?
Naomba nikuulize swali, na ningependa unijibu kiutulivu, kwa sababu mada yako ni muhimu sana, siyo katika eneo hili pekee, bali ni kama kila sehemu ya utendaji wa serikali yetu.

Kwani hatujawahi kufanya vyema kuliko tunavyofanya sasa katika eneo hili?

Kwa nini tunarudi kinyumenyume katika mambo ambayo tayari tulishajuwa namna ya kuyafanya vizuri?
 
We are not serious. We need to be serious to take this country to the next level
 
Yaani huduma Kwa wateja serikalini ni shida sana. Sio uhamiaji tu. Karibu taasisi zote serikalini customer care ni tatizo. Unapiga namba husika mwezi mzima, haipatikani, ikiita basi haipokelewi. Useme Utume email, ndio kabisa, hamna majibu.
 
Back
Top Bottom