KWELI Kupakata Laptop husababisha hatari katika uzalishwaji wa mbegu za kiume

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Nimeona sehemu kuwa kupakata laptop kwenye mapaja kunasababisha uzalishwaji wa mbegu za kiume kuwa hatarini na nguvu za kiume zinaweza kupungua.

Je, suala hili lina ukweli?

1708339584883.png

 
Tunachokijua
Kompyuta ni kifaa cha ki elektroniki ambacho kina uwezo wa kufanya kazi ya kupokea, kutunza na kuchakata taarifa au data kulingana na kanuni ya program ya kompyuta inayopewa.

Kifaa hiki pia kina uwezo wa kuchapa nyaraka mbalimbali, kutuma barua pepe, kucheza michezo, kuvinjari mtandaoni, kutumiaka kuweka program za mawasiliano, kuhariri picha, video na mambo mengine mengi.

images
Mbegu za kiume huzalishwa na kukua katika kende (korodani) kuanzia kipindi cha kubaleghe hadi utu uzima wa mwanaume. Mbegu ya kiume iliyokomaa ni seli ndogo ya kizazi ya kiume inayoogelea. Seli hii ina kichwa, mwili na mkia. Kichwa chake kimefunikwa na chepeo na kina kiiniseli cha chembe nzito za kijenetiki.

Kichwa hiki kimeshikishwa kwenye sehemu iliyo na mitokondria, ambayo husambaza nguvu za kuiwezesha mbegu hii kutenda kazi. Mkia wa mbegu hii unaweza kukunjika na kunyooka, hivyo kuifanya isonge kwa mwendo kama wa wimbi.

1708342803387-png.2909022

Takriban mbegu milioni 100 - 400 hutolewa kila wakati. Mbegu hizi hubebwa kwenye kiowevu kilicho na virutubishi (manii), kinachosaidia kuziweka hai. Mbegu za kiume ni ndogo sana. Mbegu moja ndiyo seli ndogo zaidi katika mwili wa mwanamume.

Mbegu hukua hadi kupevuka kwa takriban siku 72. Kutoleshwa kwa mbegu za kiume huhitaji kiwangojoto cha mwili cha nyusi 3 – 5 chini ya kile cha kawaida. Hii ndiyo sababu makende huwa nje ya fumbatio. Makende yanapofikiwa na kiasi kingi cha joto, uzalishaji wa mbegu unaweza kutatizika na kusababisha ugumba.

Je, kupakata Kompyuta( Laptop) husababisha hatari katika uzalishwaji wa mbegu za kiume?
Laptop ni moja kati ya vifaa vya ki- eletroniki vinavyotumiwa kwa wingi sana ulimwenguni, lakini pamoja na mazuri yake mengi yapo pia madhara kadhaa yanayoweza kumpata mtumiaji iwapo hatafuata ushauri wa wataalam wa namna gani sahihi wa kutumia kompyuta, baadhi ya madhara hayo ni kama kupata uoni hafifu au maumivu ya mgongo nk.

Kwa mujibu wa Dk. Yefim Sheynkin, ambaye aliiongoza timu ya utafiti wa Chuo Kikuu cha Jimbo la New York. Utafiti huo, ambao ulijumuisha sampuli ya zaidi ya wanaume wapatao ishirini na tisa wenye umri kati ya miaka 21 hadi 35, uligundua kwamba wakati wa kukaa na kompyuta mpakato ikiwa imewekwa kwenye mapaja, inaweza kuongeza joto kwenye makende kwa hadi digrii 2.1 Celsius.

Ripoti ya CNet inasema kuwa joto kutoka kwenye kompyuta mpakato lenyewe linaweza kuongeza joto kwa digrii 0.7 C, ikileta jumla inayowezekana ya ongezeko hadi 2.8 C. Kuhesabu hilo kwenye mfumo wa Kiingereza, hiyo ni takriban nyuzi 5 Fahrenheit – gadzoinks!
1708357151355-png.2909224

Pia kwenye utafiti uliochapishwa na Fertility and Sterility - Watafiti wa Argentina ulibaini kuwa nyuzi joto linalotolewa na kompyuta mpakato wakati ikiwa inafanya kazi huwa na kiwango kinachoongeza joto kwenye makende ya wanaume, na ikiwa joto hilo litakuwa endelevu kuna uwezekanao kuathirika kwa uzalishaji wa mbegu za kiume.

Pia Jamiicheck, imezungumza na Dkt. Fatma Ahmed, ambaye amethibisha kuwa kupakata laptop kunaweza kusababisha madhara kwenye uzalishaji wa mbegu za kiume kwa sababu laptop hutoa joto ambalo linaogeza joto kwenye makende.

Akizungumza zaidi amesema mwili wa binadamu umeumbwa na nyuzijoto zake ambazo makende hayatakiwi kuwa na nyuzijoto hilo ndio maana imewekwa kwa chini nje ya mwili ili zipate nyuzi joto yenye kiwango kidogo zaidi ndio maana wanaume wanashauriwa wasikae kwenye jakuzi au maji ya moto au kwenye joto kali kwa muda mrefu sana.

Kupakata laptop kutaongeza joto ambalo litaathiri uzalishaji wa mbegu za kiume na hata kusababisha ugumba.

Daktari ameeleza kuwa madhara huweza kutokea ikiwa kitendo hicho kitafanya kwa muda mrefu na si tendo la moja huweza kuleta madhara.


Hivyo, kutokaka na hoja za wataalamu wa afya JamiiCheck inaona kuwa hoja inayodai kuwa kupakata Laptop kwenye mapaja inapelekea kuathirika kwa mbegu za kiume ni ya ukweli

Attachments

  • 1708342803387.png
    1708342803387.png
    116.6 KB · Views: 18
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom