Kumwaga mbegu za kiume/kike kiholela ni hatari kwa afya

ONJO

JF-Expert Member
Jun 1, 2022
215
261
Habari za mda ndugu zangu.
Moja kwa moja kwenye mada

Kumwaga mbegu za kiume au za kike ni hatari kwa afya.πŸ’ͺπŸ’ͺπŸ’ͺπŸ’ͺπŸ’ͺπŸ’ͺ

Nayaandika haya nikitumia Biblia Kama Mwongozo wa maisha,Kwani kwa kuamini yaliyoandikwa ndipo tunakuwa na maisha marefu.

Maisha marefu Kwasababu kuna ufufuo kwa wale watakaoishi Kama Mungu anavyotaka.
Maisha mafupi Kwasababu ya kutoamini neno la Mungu,

Kumbe urefu wa maisha upo katika kumcha Mungu..Kuishi miaka mingi bila kumjua Mungu Ni hasara.

Naam imeandikwa Mwanzo 38
IMG_20231219_175431.jpg

Ukiendelea hapo chini yake utaona Bwana Mungu akamua huyo Onani.

Jambo hili kwa kizazi chetu limekuwa mazoea kwa vijana wake kwa waume.
πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Kufanya ngono kabla ya mda wa kuoa,
Kijana anajua kabisa kuwa huu si wakati rasmi wa kufanya mapenzi,anachokifanya anavaa kondomu ili asimpatie binti mimba.
Je hiyo sio kumwaga nje?
Na mwingine kupiga punyeto usiku na mchana nayo ni kumwaga mbegu nje kabla ya wakati.

Mfalme sulemani alifundisha akisema"Nawasihini enyi binti za yerusalemu msiyachochee Wala kuyaamsha mapenzi mpaka menyewe yatakapoona kuwa ni vema"Wimbo ulio bora 3:5

Watanzania acheni kuwaka tamaa za kimapenzi.
Kwahiyo mnaweza mkaona kuwa kumwaga mbegu ni dhambi mbele ya Mungu.

Mabinti nao wanakila aina ya vidoge vya kuzuia mimba badala wasubiri mda wa kuolewa wanaona Ni starehe kufanya mapenzi kila siku,

Enyi mabinti aina ya kina Onani, Enyi vijana aina ya kina Onani.Mnajali kutimiza haja za mapenzi kuliko kutunza utu wenu.

Kama Onani hakutaka kumwagia mbengu zake ndani, kwanini alikubali kulala naye?hapa ni hakika kabisa alitaka kuonja utamu wa mke wa ndugu yake ni sio kumzalia.
ACHENI KUFANYA MAPENZI KABLA YA WAKATI
kwanini mnadhubutu kupoteza mbolea adimu Kama hiyo,yapaswa kuihifadhi kwaajili ya mtu mmoja, atakaye furahia kwa upendo wa Kweli.

BASI KUPIGA PUNYETO NA KUMWAGA MBEGU NJE KWA KUVAA KONDOMU NI KOSA AU DHAMBI.
Kwamaana imeandikwa yeye amtazamaye Mwanamke kwa kumtamani amekwisha zini naye moyoni.Bwana Yesu alimaanisha tusifikirie kufanya mapenzi kwenye akili zenu mpaka wakati wa kuoa na kuolewa utakapofika.
πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ‡ΉπŸ‡Ώ

Na ONJO Mpenzi wenu.
 
Je! Mapadri na Masister ambao hata hawaruhusiwi kuoa wanatakiwa kumwaga mbegu zao wapi??

Qur'an inasema nini kuhusu Upadri?

Qur'an 57:27 inasema hivi '...'Tena tukafuatisha nyuma yao Mitume wengine, na tukamfuatisha Isa bin Mariamu, na tukampa Injili. Na tukajaalia katika nyoyo za walio mfuata upole na rehema. Na umonaki (utawa wa mapadri) wameuzua wao. Sisi hatukuwaandikia hayo, ila kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu. Lakini hawakuufuata inavyo takiwa kuufuata. Basi wale walio amini katika wao tuliwapa ujira wao. Na wengi wao ni wapotovu.

Kumbe hapo utaona kwamba upadri na utawa ilikua ni uzushi wala MUNGU hakuwaambia wafanye hivyo, ispokua wao walifanya hivyo kutafuta radhi ya MUNGU, lakini hata hivyo hawakufuata inavyotakiwa na wengi wao walipotoka.
 
Haha haponi mtu
Hata Pope haponii 😁
 
Kama wao walifanya hivyo yawapasa kutomwaga kabisa, Wala kufikiria mapenzi maana ndicho kiapo chao kwa Mungu.
 
Mbegu za kike zipoje mkuu, mbona unanichanganya?

Halafu hilo si agano la kale halizingatiwi....
Mambo ya kale yamepita mkuu!,kwanini Yesu alifundisha usizini,usiibe,usiue, usiseme uogo?Wewe ndiye mwenye fikra zilizokufa.Kumbe upo tayari kufanya mapenzi na mama yako Mzazi?
 
hata kama asipoanza atazini tu aidha kwa mawazo ama kwa nyeto

au hadi mawazo yanafundishwa?
Ndiyo dhambi huanzia ndani ya mawazo ya mtu na kutekelezwa kwa matendo.Je unawezaje kumtaka mtu ufanye naye mapenzi Kama hujawaza kwanza?
 
Mambo hayo ni ya Wayahudi mimi Mwafrika hayanihusu namwaga popote ninapotaka
Familia moja ilizaa Mataifa na Kwasababu hiyo na wewe upo,Kama Mungu aliwezesha hilo kwanini asikutazame wewe mwafrika ambaye Ni Mali yake?
 
Back
Top Bottom