Kuongezeka kwa ujenzi wa vituo vya mafuta DSM

Kuongezeka kwa ujenzi wa vituo vya mafuta DSM

Neus

Member
Joined
Jun 24, 2020
Posts
38
Reaction score
60
Habari Watz,

Kuna jambo ambalo Mimi naliona toka tumalize uchaguzi wa 2020 linatokea kila kukicha nikipita barabarani ambalo hatukulizoea kwa kipindi hiki Cha Hayati. Kumekuwa na ongezeko kubwa la ujenzi wa vituo vya mafuta hasa Bagamoyo Road kuanzia maeneo ya Tegeta hadi Bagamoyo ilihali wananchi wengi tupo dhofu bin taabani kiuchumi.

Kinachonifikirisha ujenzi huu haukutokea miaka miwili mitatu iliyopita lakini ghafla kila sehemu wazi watu wanajenga vituo vya mafuta. Kuna hata mmoja pale daraja la mto Mpiji unapovuka toka Bunju kwenda Bagamoyo kajenga usiku na mchana kwa wiki mbili tu. Tunaofahamu mambo ya ujenzi ni gharama kubwa.

Swali fikirishi hizi hela watu wamezitoa wapi ghafla? Ndo kusema hayati alianza kuachia hela baada ya miaka yake mi5 ya Kubana? Au ndo tutarajie mmwagiko wa hela mtaani tena?
 
Balaaaaaaaaa tupu UTAKATISHAJI PESA WA UCHI

TISS NA TAKUKURU YAO

USINGIZI WA PORNO
 
Kiongozi swala la ujenzi wa sheli kwa njia ya bagamoyo linatokana na uhitaji wa njia husika ,tambua magaro mengi sasa yanapitia njia ya bagamoyo, mabasi ya mkoani na malori, ya Tanga, Arusha na moshi hupita huku, soon kutakuwa kama njia ya Kimara.

Kwahiyo hili lisikushangaze ni njia ishakuwa kubwa na watu wenye akili huwekeza kwa kuangalia maslahi ya baadae, hata usishangae pia na hoteli zikianza kunengwa na nyumba za kulala wageni nyingi kwa ajili ya wasafiri.
 
Kiongozi swala la ujenzi wa sheli kwa njia ya bagamoyo linatokana na uhitaji wa njia husika, tambua magaro mengi sasa yanapitia njia ya bagamoyo ,mabasi ya mkoani na malori ,ya tanga arusha na moshi hupita huku ,soon kutakuwa kama njia ya kimara.
kwahiyo hili lisikushangaze ni njia ishakuwa kubwa na watu wenye akili huwekeza kwa kuangalia maslahi ya baadae ,hata usishangae pia na hoteli zikianza kunengwa na nyumba za kulala wageni nyingi kwa ajili ya wasafiri.
Kwani njia hii si imekamilika zaidi ya miaka 3 iliyopita na magari kuongezeka. Mtoa hoja anauliza kwa nini sasa ndio zinajengwa
 
Kwani njia hii si imekamilika zaidi ya miaka 3 iliyopita na magari kuongezeka....mtoa hoja anauliza kwa nini sasa ndio zinajengwa
Hoja yangu hapa kipngozi ni kuanza kutumiwa na mabasi ya abiria ndipo kumeongeza thamani na hadhi ya njia hii na ndomana umeona watu wanajitahidi kujenga vituo vya mafuta ,pia watu wengi wanaokwenda tanga arusha moshi, kwa gari ndogo hupenda kutumia njia hii sababu ni fupi tofauti na ile ya chalinze, na pia mji sasa unakuwa kama ilivyokuwa kimara mbezi na kibamba, now sasa njia ya bagamoyo inaanza kukuwa, na ndomana ukitoka bunju kuja mapinga sasa pana majaji tofauti na mwanzo, hii inaashiria wakazi wameongezeka walojenga mapinga. kerege zinga mpaka kilomo.
 
Siyo Dar tu, ni nchi nzima, njoo Morogoro Msamvu, ATN, Total, Puma, Lake, Bahlaboo, Oilcom, Lake na eneo lilipo katikati ya shule ya msingi Msamvu na Moproco kinajengwa...sidhani kama kuna uhitaji kiasi hiki wa mafuta.

Nenda sasa barabara ya Mikumi-Ifakara, vituo vi3, Ifakara-Malinyi almost NOTHING. Vituo ni Ifakara mjini.

Everyday is Saturday................................😎
 
Vigwaza mpaka Chalinze wajuba ni kama wanashindana vile, ndani ya miezi 4 vituo vya mafuta kama 6 hivi vimenyanyuka, Mount Meru, KSK na vingine kibao vinaendelea kujengwa. Kumekucha
 
Shida ni kwamba kila sehemu sasa ni kituo makazi ya watu hayaheshimiwi tena..wala shule haina maana tena. Hatuwezi kwenda bila mpangilio wa maisha.
Hilo ndiyo tatizo, old Dar Road karibu na makaburi ya Kola, Al-Saedy, kajenga kituo wenye kona fulani, nyuma ya kituo ni nyumba za watu ukuta kituo nyuma watu wanaishi. Aisee!

Wanachotakatisha kitakuja kutakata na roho za watu.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Hata mimi nimeliona hilo tena zaidi huyu tajiri bwana Alii na Lake Oil yake, kazitandaza Dar na vichochoro vyake,
Inafikirisha sana, kwanini ghafla sana vituo vya mafuta vimeota kama uyoga?

Ni jambo jema lakini maana wanyonge tunapata ajira.
 
Hata mimi nimeliona hilo tena zaidi huyu tajiri bwana Alii na Lake Oil yake, kazitandaza Dar na vichochoro vyake,
Inafikirisha sana, kwanini ghafla sana vituo vya mafuta vimeota kama uyoga?

Ni jambo jema lakini maana wanyonge tunapata ajira.
Lake oil kwa hapa Daslam ndio mbabe yan had ndani ndani huko sheli zake zipo kaamua kuteka sokl mtu ukitoka chumban sheli hii hapa
 
wengi wameona kujenga vituo nje ya mkoa unapata eneo kubwa kwa bei nafuu ie milioni 20 kwa acre 20 , inaweza kufanywa kuwa multiple investment kama parking za malori yao, hoteli za wasafiri, haina athari ya kuvunjiwa kupisha upanuzi kama ilivyo ukiwa ndani ya jiji.

aidha wateja wa nje ya mkoa wa dar wananunua mafuta mengi kwa awamu moja sababu ikiwa ni kwa ajili ya safari ndefu tofauti na wa ndani ya mkoa wanaoweka elf 7 kwa elf 9 mpaka magari yanazima.
 
Watu wakibanwa wasiweke pesa benki kwa kuhojiwa hojiwa wanazihamishia mitaani kujenga vitega uchumi wakiachwa free pesa zinajaa kwenye mabenki sababu wanajua huulizwi .Sheria za money laundering zinatakiwa zisiwe kali sana zilinde tu pesa za umma zisiibiwe lakini kama hela zinapigwa sekta binafsi huko wasifuatilie sana mfano kuna wafanyakazi sekta binafsi wanawaibia kampuni zao huko waweza wakuta wana mabilioni wakiweka benki fuatilia tu kama kuna pesa ya umma imeibiwa ukiona haipo kauka

Mwachie pesa zake

Sasa hivi nadani kuna baadhi pesa wanazo ila wanaogopa kuweka benki ndio maana ya huu muibiko wa vituo vya mafuta vingine kila baada ya hatua chache
 
Back
Top Bottom