NAMBA MOJA AJAYE NCHINI
JF-Expert Member
- Oct 29, 2019
- 8,526
- 17,432
1. Vyama vyote vya siasa ni mali ya serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo Nchi ina jukumu la kuvilea, kuvilinda na kuvipa nafasi ya kushiriki kazi za kimaendeleo ya nchi kwa ujumla.
2. Baraza la usalama na Deep state Viwe na jukumu la kuweka mfumo wa uongozi wa kila chama na uteuzi wa viongozi kwenye kila chama kabla ya kupigiwa kura na wananchi kwa kuzingatia uzalendo na uwajibikaji wa wateuliwa ili kuepuka mapandikizi na viongozi wasio wazalendo.
3. Iwepo Tume huru ya uchaguzi ili kufanya Demokrasia halisi ambayo itatamalaki nchini Bila hofu ya watawala kwa kuwa wateuliwa kugombea wamekidhi vigezo vya uzalendo kutokana na mchujo uliofanyika kuwapata kutoka namba 2 hapo juu.
4. Raisi aliye madarakani awe chini ya uangallizi wa Baraza la usalama wa taifa na Deep state na sio kua top wa kila kitu. Itasaidia kudhibiti madaraka yake hata kuondolewa madarakani kama atakiuka sheria na maono ya Taifa letu ili kuleta mamlaka ya kumwajibisha Rais aliepo madarakani kuepuka migogoro na kuvuruga umoja wa kitaifa.
Angalau haya yakifanyika yataepusha jeshi letu kutumika ovyo kutishia uhai wa vyama vingine na harakati za siasa nchini kama ilivyo sasa hivi!