Kunasababu kijana mwenye degree kuoa binti mwenye degree

Mbona mimi natafuta mkaka asie na degree na mimi nnayo? Msituharibie sifa bana.

huwezi mpata kirahisi. Wanaume tuna tabia fulani ya kuangalia mwanamke unayeweza kumcontrol kwenye vitu vingi. Sasa nyie dada zetu mliosoma mna kasumba ya kutobabaishwa na mwanaume yeyote kwa sabab unaweza kuzaa na mtu na ukaishi na wanao. Mwisho utaishi kunishikisha mwiko jikoni kisa elimu yangu ndogo. Kuna jama alioa dada mmoja wa chuo na ye mwalimu wa primary alikuwa anaendeshwa mpaka akakimbia ndoa. Mi upande wangu nilishaweka kigezo mke ntakayeoa ni lazima awe na at least diploma. Hivyo relationship yoyote na mtu chini ya hapo huwa naikwepa kabisa. Hata ukiwa na mvuto na tabia nzuri kiasi gani,ntakupotezea tu! Hata waliosoma wapo wenye feature hizo.
 
Jamani kwani kushika mwiko kuna ubaya gani? Mbona wapo waliosoma kibao wanashika mwiko tena kwa kupenda na sio kulazimishwa?

Nwy elimu sio inayooa wala inayoolewa. . . vyeti ni kwaajili ya kazi na sio kuendesha ndoa. Ukishalijua hilo hutosumbuliwa na elimu ya mtu.
 
Tanesco mnaniua,konyagi gizani, kuipata mpaka nipapase mezani mpaka nije nivunje kaglasi kangu nimekanunua bei kubwa, joto nalo limezidi, pulizi rudisheni umeme sina mpango wa kukaa bar leo
 
Wewe hujasoma, mimi nimesoma. Nilivyosema ndivyo.

haahahha Lizz babygal hizi ndo sentensi zinazowakimbiza hahahhaha....usiseme mi nimesoma mwulize kwani we unafikiri inatakiwa iweje sweetie?? kaaz kweli kweli
 
Chonde vijana degree sio soln ya kila jambo....ndoa siyo kuderive formula ngumu za umeme...mahusiano/ndoa yanajengwa na vitu vingi (mapenzi kwanza).....malezi/makuzi yanamuathiri mtu moja kwa moja haijalishi ana kiwango gani cha elimu au la...usomi unatija tu pale unapotumiwa kujitafutia maarifa bora ktk mahusiano(usione vyaelea)...juhudi na maarifa vinahitajika ktk KUJITAMBUA binafsi ili uwe na kitu cha KUTOA ktk mahusiano yako...ktk kila jambo ni vizuri kumtanguliza Mungu..
 
haahahha Lizz babygal hizi ndo sentensi zinazowakimbiza hahahhaha....usiseme mi nimesoma mwulize kwani we unafikiri inatakiwa iweje sweetie?? kaaz kweli kweli

Hahahaha. . . .
Mwanaume shurti abembelezwe eehhhhh? Ntazingatia somo mpenzi, nisije nikakimbiwa kabla hata sijapata.
 
Acheni viburi, dharau na majivuno kisa hizo Elimu za vyuo mlizozipata.Chungeni sana maneno yanayowatoka midomoni usizungumze ili usifiwe na watu ama ili umfurahishe mtu fulani.:embarassed2:
 
Jamani kwani kushika mwiko kuna ubaya gani? Mbona wapo waliosoma kibao wanashika mwiko tena kwa kupenda na sio kulazimishwa?

Nwy elimu sio inayooa wala inayoolewa. . . vyeti ni kwaajili ya kazi na sio kuendesha ndoa. Ukishalijua hilo hutosumbuliwa na elimu ya mtu.

kushika mwiko mwanaume kupo lakini kwa mila zetu no! Huo ni sawa na mkosi kwa mtu ambaye ameoa. Unapooa au kuolewa unategemea kujenga familia imara,yenye kushirikiana kati ya mama na baba. Sasa kila kitu anapotegemewa mwanaume mpaka chupi,vipodozi, chakula, khaa!! Mi ntaweza wapi. Hivo vitu ntanunua kama zawadi au muda wowote nikipenda,lakini visiwe vitu vya lazima kutoka kwangu. Kuna wanawake anaweza kuwa hana elimu ila ni mjasiriamali mpaka we unategemea kwake,mfano wachaga,wakinga. Unaweza kumuanzishia biashara na akaikuza mpaka ikawa ndo tegemeo la familia. Lakini kuna makabila unamwanzishia biashara anakula mtaji na madeni unalipa kwa mshahara wako. Sasa kwa nn nisitafute msomi mwenzangu ambaye tutasaidiana hata kama ni kidogo?
 
haahahha Lizz babygal hizi ndo sentensi zinazowakimbiza hahahhaha....usiseme mi nimesoma mwulize kwani we unafikiri inatakiwa iweje sweetie?? kaaz kweli kweli

hizi ndo kauli tunazopewa ndani ya nyumba. Kwa nn nisikimbie kama sina madesa?
 
kushika mwiko mwanaume kupo lakini kwa mila zetu no! Huo ni sawa na mkosi kwa mtu ambaye ameoa. Unapooa au kuolewa unategemea kujenga familia imara,yenye kushirikiana kati ya mama na baba. Sasa kila kitu anapotegemewa mwanaume mpaka chupi,vipodozi, chakula, khaa!! Mi ntaweza wapi. Hivo vitu ntanunua kama zawadi au muda wowote nikipenda,lakini visiwe vitu vya lazima kutoka kwangu. Kuna wanawake anaweza kuwa hana elimu ila ni mjasiriamali mpaka we unategemea kwake,mfano wachaga,wakinga. Unaweza kumuanzishia biashara na akaikuza mpaka ikawa ndo tegemeo la familia. Lakini kuna makabila unamwanzishia biashara anakula mtaji na madeni unalipa kwa mshahara wako. Sasa kwa nn nisitafute msomi mwenzangu ambaye tutasaidiana hata kama ni kidogo?

Swala la utegemezi halina elimu. Wanawake kibao wana kazi zao ila waume zao hawajui mshahara wao hua unaishia wapi maana mpaka pesa ya lunch bado wanaomba, na matumizi ya nyumbani hawachangii. Kwahiyo wewe ukiingia kichwa kichwa ukidhani kuwa na msomi ndio umepata, utaishia kujikuta umepatikana.

Alafu huo ushirikiano unaoongelea unainclude kumsaidia mke wako pale anapokua amechoka au hajiwezi, sio unajifanya tunashirikiana wakati hata kumsaidia kuondoa kikombe mezani unadai sio kazi yako.
 
unaoa mtu unaoa degree? Mapenzi hayaangalii elimu

hatuoi degree,ila lazima awe anajiweza. Hata kama hako kamshahara atapeleka kwao itapunguza kuchukua na za kwangu. Mi siwezi kuoa mtu ambaye ataniogopa kwa sababu hana elimu. Nahitaji yule ambaye tutaheshimiana na kutambua majukumu ya kila mtu. Mi sipendi yale mambo ya KWA SABABU WEWE UMESEMA. Lazima mkubaliane kwenye mambo ya muhimu. Ila likija suala la kubisha basi tu kwa sababu amesoma,hapo comand inahitajika. Pia jua kuna wakati baba mambo yanaweza kukuendea vibaya baba aafu lifu la watoto likawa ovyo.
 
Kuogopwa sababu ya elimu...hapo nyalotsi mlitongozana au ulikabidhiwa mke...
 
Elimu ni kgezo kimojawapo muhimu na wala :nerd:sii pekee wakati wa kuchagua mwenza
 
kwani cku hizi kuna kutongozana? Mtu mnafahamiana,mnapeana contacts, Mnatembeleana na kila kitu kinamalizika. Mwisho unajikuta upo kwenye uhusiano na mtu ambaye ulimtamani tu ghafla. Ndo maana cku hizi ndoa ni kitu cha bahati mbaya! Watu wanapeana mimba kwa kuviziana baada ya hapo majuto yanaanza.
 
Elimu ni kgezo kimojawapo muhimu na wala :nerd:sii pekee wakati wa kuchagua mwenza

mimi nilianza na elimu,thus ufuatiliaji wa hayo mengine ulijikita kwa waliosoma tu. Hao wengine nilikuwa nakwepa hata kuwa karibu nao.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom