Wanaotajwa tajwa kumrithi Rehema Sombi kiti cha UVCCM Mkoa wa Singida

Kanyunyu

JF-Expert Member
May 2, 2012
335
495
WANAO TAJWA TAJWA KUMRITHI REHEMA SOMBI KITI CHA UVCCM MKOA WA SINGIDA

Na Mwananzengo

Baada ya Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Singida ndugu Rehema Sombi kufanikiwa kushinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi taifa , inatarajiwa kwamba ataachia nafasi Moja ya Uenyekiti wa uvccm Mkoa wa Singida Ili abaki na nafasi ya juu ya Makamu Mwenyekiti uvccm taifa, hilo ni takwa la kanuni kwakuwa nafasi zote mbili ni kazi za muda wote hivyo anapaswa kubaki na kofia Moja .

Kwakuwa ni wazi kwamba uchaguzi wa uvccm Mkoa wa Singida utarudiwa mapema mwaka huu ( January/ February) Ili kumpata mrithi wa Rehema Sombi, joto la siasa limeanza kupanda na kumeibuka mjadala mkali ni nani hasa ataweza kumrithi Rehema Sombi? Wadau mbalimbali na wachambuzi wa siasa za Mkoa wa Singida wametoa mitazamo yao na kuwamulika baadhi ya vijana ambao wanatajwatajwa na wanapewa nafasi kubwa ya kunyakua kiti hicho Cha Mkoa kutokana na sifa zao njema na uwezo wao wa kiuongozi . Kwa kutambua hilo tutawachambua vijana hao kwa ufupi Ili kupanua mjadala wa kisiasa kuelekea kumpata Mwenyekiti mpya wa umoja wa vijana wa CCM Mkoa wa Singida.

Wanaotajwatajwa ni hawa wafuatao,

1. KASSIM MUMBAWA
2. MUFANDII MSAGHAA
3. LAMECK OMARY
4. BARAKA MUSA
5. ALLY YANGA
6. MUNIRA GEORGE
7. SHIGELA MWIGULU
8. MOHAMED MSAGHAA
9.ABDUL ALLY
10. JORAM NKUMBI

ANALYSIS

1. KASSIM MUMBAWA

Huyu ni kijana anatokea Ihanja Wilayani Ikungi Mkoani Singida, Kassim amekuwa kwenye harakati za uongozi wa Uvccm tangu akiwa shuleni na baadae chuoni akijipambanua kwa umahiri wake wa kujenga hoja na kujipambanua katika uwezo mkubwa wa uongozi . Anaonekana ni mtu sahihi atakayeweza kuongoza Jumuiya ya vijana na kuwa sauti ya vijana wa Mkoa wa Singida.
Kassim Mumbawa amehitimu masomo yake katika chuo kikuu Cha Cha Dodoma akisomea degree ya kwanza ya Sociology.

2. MUFANDII MSAGHAA

Huyu ni Binti anatokea Igauri kata ya Ntonge wilaya ya Singida Vijijini Mkoani Singida. Mufandii ni Binti mwenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja na ushawishi kutokana na kuwa na exposure ya masuala ya siasa na uongozi . Mufandii ameshiriki harakati za siasa za UVCCM tangu akiwa chuoni Mzumbe University ambapo alikuwa ni mshiriki mzuri na mwana hamasa wa kukitetea Chama na Jumuiya ya vijana.
Katika uchaguzi Mkuu wa CCM mwaka huu 2022 Mufandii msaghaa alishiriki kikamilifu siasa za Umoja wa vijana wilaya ya Singida Vijijini.
Mufandii ni mwanasheria aliyehitimu masomo ya degree ya kwanza ya sheria katika chuo kikuu Mzumbe na mwaka jana alihitimu Post graduate Diploma in taxation kutoka chuo cha Kodi Dar es salaam.

Mufandii anatazamwa kama kijana sahihi anayeweza kuivusha Jumuiya ya vijana na kutosha kuvaa viatu vya Rehema Sombi kwa ukamilifu .

3. LAMECK OMARY

Lameck Omari ni kijana kutoka Wilayani Manyoni na amewahi kuwa Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Manyoni kwa kipindi cha mwaka 2017- 2022 na hakugombea tena nafasi hiyo katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2022.
Lameck ni mhitimu wa degree ya kwanza ya Elimu kutoka chuo kikuu Tumaini . Kwa Hulka yake ni kijana mwenye misimamo thabiti katika kusimamia mambo na amekuwa na uzoefu wa siasa za UVCCM Mkoa wa Singida. Lameck anatajwa kuwa na nafasi nzuri ya kuweza kurithi mikoba ya Rehema Sombi endapo atazichanga karata vizuri wakati wa uchaguzi wa kuziba nafasi ya Kiti Cha vijana Mkoa wa Singida.

4. BARAKA MUSA

Baraka Musa ni kijana kutokea wilaya ya Singida Vijijini Mkoani Singida, ni msomi mwenye exposure kubwa ya masuala ya siasa na uongozi ndani ya CCM na Jumuiya ya vijana. Baraka ana uwezo mkubwa na sifa za kuongoza Jumuiya ya UVCCM Mkoa endapo atazichanga karata vizuri kuelekea uchaguzi wa kuziba nafasi kiti cha vijana Mkoa wa Singida.
Kwa sasa Baraka Musa ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Singida Vijijini na ni mjumbe wa kamati ya siasa ya Halmashauri ya CCM wilaya ya Singida Vijijini.

5. ALLY YANGA

Huyu ni kijana kutoka Singida mjini, ni mhitimu wa degree ya kwanza kutoka chuo kikuu Cha Sokoine kilichopo Mkoani Morogoro.
Yanga ni kijana mzalendo na mwenye matamanio makubwa ya kisiasa kutokana na ushiriki wake wa siasa za chuoni na siasa za Mkoa wa Singida kwa ujumla. Katika uchaguzi Mkuu wa CCM 2022 Yanga alijitokeza kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Singida na kubahatika kuteuliwa na vikao vya chama na katika uchaguzi huo alishika nafasi ya mshindi wa pili ambapo Rehema Sombi aliongoza kwa kura na kushinda nafasi hiyo kwa kishindo .
Yanga anatazamwa kwa jicho la tatu kwamba ana uwezo na sifa za kuongoza Jumuiya hiyo ya vijana Mkoa wa Singida hivyo anapewa nafasi nzuri ya kuweza kurithi mikoba ya Rehema Sombi.

6. JORAM NKUMBI

Joramu Nkumbi ni kijana kutokea Misuna wilaya ya Singida mjini, huyu ni mwana ulumbi wa misamiati ya lugha ya kiswahili, ni mwana majumui wa Afrika na Mwalimu wa masuala ya uongozi kwa vijana barani Africa kupitia Taasisi ya kuwajenga vijana kiuongozi ya AYLF .
Joramu Nkumbi ni public speaker na motivational speaker wa masuala mbalimbali ya uongozi na kijamii , ni mhitimu wa degree mbili (masters degree) akibobea katika taaluma ya hesabu kutoka chuo kikuu Cha Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Joramu Nkumbi ana uwezo usio na kifani na bongo kali sana linapokuja suala la uongozi na siasa . Anatajwa kuwa na uwezo na nafasi nzuri ya kuweza kurithi mikoba ya Rehema Sombi na kuvaa viatu kwa ukamilifu.

7. MUNIRA GEORGE

Huyu ni kijana kutokea huko Nduguti Wilayani Mkalama , pia ni kiongozi wa Chama ngazi ya wilaya nafasi ya katibu wa siasa na uenezi wa Wilaya, pia ni mjumbe wa kamati ya siasa ya Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Mkalama.

Munira anatajwa kuwa kingunge wa siasa kutokana na uzoefu wake wa siasa za chama Cha Mapinduzi wilaya ya Mkalama, Mkoa na kitaifa kutokana na ushiriki wake wa vikao vya wilaya , Halmashauri kuu ya Mkoa na mkutano Mkuu wa CCM taifa .

Munira anatajwa kuwa na exposure kubwa ya masuala ya siasa hivyo anaweza kumudu kuongoza Jumuiya ya vijana Mkoa wa Singida hivyo inategemeana na atakavyozichanga vizuri karata zake kuelekea uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi ya kiti cha vijana Mkoa wa Singida.

8. ABDUL ALLY

Huyu ni kijana kutokea Mtinko wilaya ya Singida Vijijini, ni mwanaharakati wa kisiasa kwa muda mrefu na aliwahi kugombea udiwani kata ya Mtinko mwaka 2020 kupitia Chadema kabla kurerejea CCM na kuendeleza ushiriki wake wa siasa ndani ya CCM.
Anatajwa kuwa ni kijana mwenye hamasa na siasa akiwa na matamanio ya kushika nafasi za kisiasa kuonyesha maono yake ya muda mrefu.
Abdul Ally anatazamwa kama kijana sahihi anayeweza kuongoza Jumuiya ya vijana Mkoa endapo atazichanga vizuri karata zake kuelekea uchaguzi wa kumpata mrithi wa Rehema Sombi.

9. SHIGELA MWIGULU

Shigella Mwigulu ni kijana kutokea wilaya ya Manyoni , amekuwa kwenye harakati za kugombea nafasi za uongozi ndani ya Jumuiya ya UVCCM wilaya ya Manyoni na Mkoa wa Singida.

Katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2022 Shigella alijitosa kugombea nafasi ya Uenyekiti wa uvccm Mkoa wa Singida na kufanikiwa kupitishwa na vikao vya uteuzi, katika uchaguzi huo Shigella hakufanikiwa kushinda mbele ya Rehema Sombi aliyevuna kura za kishindo na Shigella kushika nafasi ya tatu .
Shigela anatajwa kuwa na nafasi nzuri ya kuweza kurithi mikoba ya Rehema Sombi kutokana na uzoefu wake wa ushiriki wa siasa za mwaka 2022 hivyo anao mtaji wa wapiga wanaomfahamu vizuri hivyo itategemeana atakavyozichanga karata zake kuelekea uchaguzi wa kumtafuta mrithi wa Rehema Sombi.

10. MOHAMED MSAGHAA

Huyu ni kijana kutokea wilaya ya Singida Mjini na ni kiongozi wa Jumuiya ya vijana kwa nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ambapo alichaguliwa mwaka jana kuongoza Jumuiya hiyo ya vijana.
Mohamed ni mhitimu wa degree ya kwanza kutoka chuo cha Sokoine University of Agriculture akibobea katika fani ya
Agricultural economics and agribusiness.

Mohamed Msaghaa anatajwa kuwa na uwezo mzuri wa kiuongozi hivyo ana nafasi nzuri ya kuweza kurithi mikoba ya Rehema Sombi kwenye kiti cha vijana Mkoa wa Singida endapo atazichanga karata zake vizuri kuelekea uchaguzi wa kumpata mrithi wa Rehema.

Uchambuzi huu wa majina ya kumi bora ya wanaotajwa tajwa umelenga
Kuwaleta vijana hao kwenye uso wa umma Ili kuibua mjadala chanya kuelekea mchakato wa kumpata Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Singida atakayerithi mikoba ya Rehema Sombi siku za usoni .

Imeandaliwa na Mwananzengo mchambuzi wa masuala ya siasa .
 
UVCCM kwa vile mmeji pambanua kuwa kazi na wajibu wenu ni unafiki na upambe Sufuriani angewafaa sana
20221228_062706.jpg

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Naona Ikungi wamelala fofofo! Hakuna hata anayetajwa?
Wapi bi Zulfat?
 
MWIGULU apewe hiyo nafasi
 
Sina hela so habari kama hizi naziona kama ni mandazi yaliyolala mwezi mzima ndo upewe uyale
 
Back
Top Bottom