Simulizi: Fated To die (Mwenye Hatma ya Kufa)

McCord

JF-Expert Member
Apr 13, 2023
233
568

FATED TO DIE
(MWENYE HATMA YA KUFA)
SEHEMU YA 01

“Baby, mambo ni mengi nashindwa hata kutulia” aliongea Salome akiwa ameshikilia simu yake, yalikuwa majira ya usiku na alikuwa akiongea na mpenzi wake ambaye kwa muda huo alikuwa maeneo ya mbali na nyumbani kwao. Baada ya kama nusu saa kupita hatimaye maongezi baina ya Salome na mpenzi wake aliyekuwa akifahamika kwa jina la Clinton yalifikia tamati, baada ya maongezi hayo Salome alirudi tena ndani ya nyumba yao na kuelekea chumbani.

Kwa majira haya ya usiku hakupenda kuongea na simu akiwa ndani kwani hakutaka wazazi wake wasikie
alichokuwa akikiongea. Akiwa bado chumbani kwake alisikia mtu akigonga kwenye mlango wa
chumba chake. “Salome mwanangu fungua mlango” aliongea mama yake Salome, mama huyu alikuwa mtu wa Mungu sana na hakupenda mwanae awe na mahusiano na watu ambao kwake aliona kama watu
wasioleweka kabisa.

“Mama ni nini tena usiku huu? Sasa hapo nitalala saa ngapi?” aliuliza Salome akiwa anaufuata mlango kichovu na baada ya kuufungua mama yake aliingia ndani ya chumba cha mtoto wake. “Nina jambo la kukuuliza” aliongea mama yake Salome akiwa anamuangalia binti yake usoni, mama ni mama baada ya sekunde kadhaa za kumtazama binti yake usoni aligundua jambo.

“Anaitwa nani?” aliuliza mama yake Salome akiwa anatoa tabasamu, Salome alilijua lile tabasamu vizuri na mara nyingi huwa lilikuwa likitokea baada ya mama yake kugundua kitu fulani, licha ya kutojua mama yake aligundua nini alijaribu kutulia na kutoa uoga wote kichwani.

“Nani tena mama?” aliuliza Salome, muda huu alishindwa hata kumuangalia mama yake usoni, aibu na hati zilikuwa zikimtafuna kwa wakati mmoja, mama yake Salome aligeukia upande ambao mtoto wake alikuwa amegeukia akiwa anapanga nguo zake na kuziweka kwenye begi.

“Huyo huyo mwanangu, nataka nimuone mkwe wangu au unasemaje mrembo wangu?” aliongea mama Salome akiwa anatoa tabasamu kubwa ambalo halikuwa na chembe ya unafki. Salome alituliza akili na kumuangalia mama yake ambaye muda huu naye alikuwa akimsaidia binti yake kupanga nguo na kuziweka kwenye begi.

“Hamna kitu mama” aliongeea Salome akiwa anatoa tabasamu la chini chini na kutazama upande mwingine. “Mimi najua mwanangu kwa furaha hiyo hauwezi kuwa peke yako, mimi nataka nimjue hata kwa picha kama itawezekana” aliongea mama Salome kwa kusisitiza akiwa anamuangalia binti yake.

“Huyu hapa” aliongea Salome na kuifuata droo ambayo ilikuwa kwenye kabati lake la nguo na hapo aliitoa picha moja ambayo alipiga na Clinton mwaka mmoja uliopita, baada ya kumpatia mama yake ile picha na yeye aliitazama na kutabasamu kisha akamgeukia binti yake na kumuuuliza swali la ghafla.

“Ameahidi kukuoa?” aliuliza mama Salome swali ambalo hata Salome mwenyewe hakujua lilianzia wapi kwani hakutarajia kama mama yake angeuliza swali lile kwa haraka sana. “Mama mbona una haraka hivyo, ndo kwanza hata uchumba wetu haujafikisha hata miaka mitatu, tukimbilie wapi ?” alijibu Salome muda huu alikuwa tayari ameshamaliza kupanga nguo kwenye begi na alilitoa lile begi juu ya kitanda chake na kuliingiza kwenye kabati ambayo ilikuwa upande wa kulia wa chumba chake.

“Siwezi jua nyie vijana wa siku hizi mnafanyaga mambo haraka haraka mno” aliongea mama Salome na baada ya hapo alitoka kwenye chumba cha mwanae baada ya kumfunika na kuhakikisha alishalala, baada ya hapo aliichukua ile picha ya pamoja ya Clinton na binti yake na kuipiga picha kwa kutumia simu yake aina ya Samsung version mpya kwa miaka ya 2017.

Baada ya kutoka chumbani kwa binti yake alitoka nje ya sebule na kuelekea sehemu ya nje ya nyumba
na baada ya hapo alipiga simu kwa mtu fulani. “Ndio bosi” iliongea sauti ya upande wa pili wa simu, sauti hii ilikuwa na mikwaruzo kama sauti ya bati ambalo lilikuwa linaburuzwa , kwa usikikaji wa sauti ile ilikuwa dhahiri kwamba muongeaji eiza alikuwa mtumiaji wa pombe za kienyeji laa sivyo alikuwa mtu wa kutumia vilevi
vingine vikali zaidi ya pombe za kienyeji.

“Nimekutumia picha Telegram, nitafutie huyo kijana wa kiume na hakikisha nakutana naye mapema sana” baada ya kuongea hayo maneno mama Salome ambaye jina lake ni Highness Mshani alirejea ndani na kurudi chumbani ambako alimuacha mumewe mzee Mshani. Familia ya mzee Mshani ilikuwa na watoto watatu wawili walikuwa wakike na mmoja alikuwa wakiume na ndio aliyekuwa wa mwisho kwenye familia na huyu alikuwa akisoma mkoani Dar Es Salaam kwenye shule binafsi ya bweni ambayo ilikuwa ya wavulana tu.

Salome alikuwa mtoto wa pili wa mzee Mshani na alikuwa amemaliza masomo ya ngazi ya chuo na alikuwa na digrii ya uhandisi wa software aliyoipata kwenye chuo kikuu cha Dae Er Salaam maarufu kama UDSM. Dada mkubwa alifahamika kwa jina la Lightness yeye aliolewa na alikuwa na mtoto mmoja wa kike na alikuwa akiishi na familia yake mkoani Morogoro.

Siku ilipokucha mambo mengine yaliendelea kama kawaida kwenye familia ya mzee Mshani, Salome alimpigia simu Clinton na kumtakia siku njema na baada ya hapo aliungana na wanafamilia kupata kifungua kinywa kwa majira ya asubuhi na alijua baada ya hapo mchana angeenda kwa Clinton na angelala huko huko na kumtaarifu mama yake kwamba alilala kwa rafiki yake aliyekuwa anafahamika kwa jina la Sapister ambaye alikuwa akiishi kwenye mji mdogo wa Mbalizi jijini Mbeya.

Umbali kutoka maeneo ya Jacaranda ambako Salome alikuwa akikaa mpaka mahali ambapo Clinton alikuwa akikaa haukuwa mrefu kwani ilihitaji gari moja mpaka kufika maeneo ya Soweto ambako ndiko alikokuwa akikaa Clinton. "Leo una ratiba gani mwanangu?” aliuliza mama Salome akiwa anamtazama binti yake ambaye
alionekana kuwa na furaha mno.

ITENDELEA
Je, mama Salome anataka kufanya nini na Clinton? Je, Salome atagundua kuhusu mpango wa
mama yake?
 

Attachments

  • fated to die.png
    fated to die.png
    268.3 KB · Views: 45

Similar Discussions

Back
Top Bottom