Polisi nchini wana roho mbaya na kauli chafu

Old guard

JF-Expert Member
Dec 15, 2020
1,493
2,697
Kiukweli nimejawa na sumu kali sana kwa jeshi la polisi, hawa majamaa sio watu wa haki, wamejawa na dhulma, tamaa na roho mbaya, ukikutana nae kavaa kiraia kama mtu vile, sasa kutana nae kavaa sare zake, roho ya ushetan imeshamtawala wanajiona wapo juu ya haki.

Tena usiombe ukutane na mwanamke yupo counter, wanamidomo michafu sana, matusi yamewajaa sana midomoni.

Nawachukia sana hawa majamaa, mbona wanajeshi roho zao ni tofauti na nyie? Ndio maan hamuendelei kazi kujazana kweny nyumba za kota.
 
Mwanajeshi kafundishwa kuua ingia anga zao ndio utajua Wana roho mbaya au nzuri.
Anaua kwa kutumia nini ambacho polisi hawana....in short wanajeshi wana nidhamu sana lakini pia kazi za jeshi haziwakutanishi na wananchi kila siku....tofauti na jeshi LA polisi ambao kila siku lazima wakutane na kila aina ya vioja....so walishakuwa waswahili vile vile hadi kuchambana wanajua vizuri tu.
 
Nimecheka Kwa sauti kabsaa
 
Tena usiombe ukutane na mwanamke yupo counter wanamidomo michafu san matusi yamewajaa san midomoni.
Ni kwenye taasisi gani nchi hii utamkuta mtu yupo counter ukajibiwa au kupokelewa vizuri? Mpaka kwenye mabenki ambako eti mteja ni mfalme ni nyodo tupu sembuse polisi?

Ila NIDA na uhamiaji wanaongoza kwa nyodo dah! 🚮🚮🚮
 
Dah umesema ukweli mtupu.
bongo customer care shida tupu.
Hata sijui tatizo ni nini?

Mdada wa NIDA alikuwa na hasira yule dada sijaona. Utafikiri kalazimishwa kuja kazini wakati kazi aliomba mwenyewe na si ajabu alihonga mpaka mbususu ili kuipata.

Ilibidi nimkomalie na kumwambia kuwa alichokuwa anafanya siyo kizuri maana sisi ni Watanzania wenzake na yeye ameajiriwa ili kutuhudumia. Nilimwacha anasonya sonya pale...nikamuomba kitambulisho changu kikitoka anijulishe...

Ajabu kweli baada ya wiki tatu tu akanitumia meseji kuwa kitambulisho kipo tayari. Ningekuwa kijana kidogo ningemshupalia nimgegede ili kulipiza kisasi kauli zake za hovyo ile siku ya kwanza.....

Ila baadaye alinitonya kuwa eti siku ile ya kwanza nilipompiga mkwara aliogopa. Kwa jinsi nilivyokuwa nimevaa alifikiri eti mimi pengine nilikuwa mzee kutoka TISS nimekuja kupeleleza 😁😁😁😁
 
Ni kwenye taasisi gani nchi hii utamkuta mtu yupo counter ukajibiwa au kupokelewa vizuri? Mpaka kwenye mabenki ambako eti mteja ni mfalme ni nyodo tupu sembuse polisi?

Ila NIDA na uhamiaji wanaongoza kwa nyodo dah! 🚮🚮🚮
Tatizo ni uhakika wa kupata mshahara. Wangekuwa wanalipwa kwa commission (au kulipwa kwa kazi uliyofanya), wafanyakazi wote wangekuwa na nidhamu na wangechapa kazi;

Hii ya kulipwa mshahara mwisho wa mwezi inafanya watu wasijali customer care maana wana uhakika wa kulipwa hela mwisho wa mwezi bila kujali wamemhudumia nani na kwa namna ipi.
 
Kiukweli nimejawa na sumu kali sana kwa jeshi la polisi, hawa majamaa sio watu wa haki, wamejawa na dhulma, tamaa na roho mbaya, ukikutana nae kavaa kiraia kama mtu vile, sasa kutana nae kavaa sare zake, roho ya ushetan imeshamtawala wanajiona wapo juu ya haki.

Tena usiombe ukutane na mwanamke yupo counter, wanamidomo michafu sana, matusi yamewajaa sana midomoni.

Nawachukia sana hawa majamaa, mbona wanajeshi roho zao ni tofauti na nyie? Ndio maan hamuendelei kazi kujazana kweny nyumba za kota.
Kuna jamaa yangu huyo,yeye ni mizinga mwanzo,kati mpaka mwisho wa mwezi Hana ela,ila yeye umpe tuuuuuuu,
 
Askari ni adui anapofunza kutii sheria ni rafiki anapokusaidia kuvunja sheria.
Tii sheria bila shuruti
Kuna umuhimu au ulazima kabisa wa kurudisha zile fomu za polisi (na. 101) almaarufu kama Notification. Mtu ulikuwa ukikamatwa na polisi kwa tuhuma za kuvunja sheria za barabara, kwenye fomu unakubali kosa au kulikataa.

Ukikubali, unalipa faini na ukikataa unafikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma hizo, na mahakama ikithibitisha utalipa faini. Sasa vile vimashine wamepewa polisi, wamejigeuza wao ndio mahakama, utake usitake, utalipa faini. Njia pekee ya kutolipa faini ni kutoa rushwa.
 
Tatizo ni uhakika wa kupata mshahara. Wangekuwa wanalipwa kwa commission (au kulipwa kwa kazi uliyofanya), wafanyakazi wote wangekuwa na nidhamu na wangechapa kazi;

Hii ya kulipwa mshahara mwisho wa mwezi inafanya watu wasijali customer care maana wana uhakika wa kulipwa hela mwisho wa mwezi bila kujali wamemhudumia nani na kwa namna ipi.
Mkuu una hoja...

Naomba usikilizwe!
 
Back
Top Bottom