OMOYOGWANE
JF-Expert Member
- Dec 30, 2016
- 3,630
- 9,175
Kazi ya macho ni kuona, vile vile kazi ya masikio ni kusikia,
Lakini sio kila tunachokiona au kukisikia kina ukweli ndani yake,
Kuna wakati macho na masilio hutudanganya
mfano: unaweza kuona samaki yupo mtoni kwenye kina kifupi cha maji kumbe yupo chini ktk kina kirefu tofauti kabisa na unachokiona kwa macho yako
Wapo waliopoteza uhai kwa kupima kina cha maji kwa miguu, sababu kubwa ni kwamba macho yaliwadanganya,
unaweza kuona mtu anafanya biashara flani na anauza sana, basi nawewe haraka haraka ukaamua kufungua biashsra kama yake, baada ya miezi mitatu ukajikuta umefilisika au kupata hasara takatifu,
Kuna wakati mtu anaweza kukuambia biashara flani inalipa, basi nawewe ukaamua kuingia kichwa kichwa mwisho wa siku unajikuta umechezea za uso biashara imedoda,
Ukipita mjini utaona mji umejaa maduka ya kila aina, yapo miaka yote hayafilisiki basi nawewe ukaamua kujichanga ukafungua duka hapo hapo mjini mwisho wa siku unajikuta matumizi ni makubwa kuliko faida 😄 unaikimbia fremu hata kabla kodi haijaisha,
Sio kila unachokiona au kukisikia ndivyo kilivyo, kuna wakati macho na masikio huwa yanatudanganya.
Tunachokiona au kukisikia kinakuwa tofauti kabisa na uhalisia
Wakuu amini amini nawaambieni kuna biashara ni cover, biashara yenyewe haifanyikii hapo,
Tuwe makini, wenye kazi msikurupuke kuacha kazi mkakimbilia kujiajili bila kufanya utafiti kwa utulivu mkubwa.
Nawasilisha, povu ruksa.