Ati ni kweli kuwa kuna kada hata wafanye Kazi miaka mia hawezi kuwa na nyumba kama ya Mwijaku?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
Habari wakuu!

Baada ya kuwakandia Machawa na kuwatukana vilivyo mpaka humu ndani uzi wangu kufutwa.

Moja ya viongozi wa bodi ya Machawa Tanzania alinipigia simu jana akiwa na furaha nyingi. Nikiwa najua kuna dili la kibiashara linakuja, nashangaa ananiambia unamuona Mwijaku huko.

Nikamwuliza kafanyaje? Akanijibu, alichofanya kuna bàadhi ya kada hata wangefanya kazi miaka mia na wapewe kiunua mgongo bado hawataweza kujenga nyumba kama ya Mwijaku.

Nikamkatia Simu. Akatuma sms wala sikuifungua. Nilijua ni mpuuzi tu. Sasa nauliza, uchawa unalipa eeeh! Lengo la kuhamasisha uchawa ni nini? Ni kwamba hawajiamini na wanatafuta kutambuliwa ndani ya jamii?

Au je Mwijaku kama moja ya viongozi waandamizi wa uchawa kuonyesha nyumba yake ni kujaribu kuwazima midomo kina siye tunaosakama shughuli yao? Au ni majibu kwa wale wanaomuona ni mwanaume wa hovyo na sasa kawajibu kivitendo kuwa yeye ni mwanaume wa aina gani?

Je, kulikuwa na ulazima upi wa Mwijaku kuonyesha mafanikio ya kazi yake?
Je, kuwawatia moyo Machawa wengine wakaze?
Àu je, kuwafungua macho vijana kuwa kazi yoyote ukiifanya kwa moyo na kwa bidii inaweza kukutoa?
Au je, kuwakatisha tamaa adui na hasimu wake?

Je, huu ndio mwanzo wa Machawa na wale wote wanaofanya kazi zinazodharauliwa ingawaje sio haramu nao kuonyesha kuwa wanapata mafanikio makubwa kwa kazi hizohizo zinazodharaulika. Tuliona kwenye kazi ya muziki ikiwa miongoni mwao kazi zilizodharaulika, kwa sasa wanamuziki kwa kiasi chake wanakaheshima kadogo na bado wanahangaika kujenga heshima?

Kazi ya udalali nayo je viongozi wake waandamizi nao watajibu kwa vitendo kama walivyofanya Machawa?

Wakati sisi Wasomi na wenye elimu za juu na pengine kazi kongwe ambazo zinaheshimiwa kwenye jamii tukiwa hatuna maisha mazuri na hata vijumba vyetu vikiwa dhoofu hali, je tuna haja ya kubadili mtazamo kuhusu maisha na kazi?

Hii inawaambia nini vijana waliomaliza chuo na waliokochuoni kuhusu fursa zilizoko kwenye jamii baada ya kumaliza masomo yao?

Je, tutabdilike ikiwa dunia itatuletea mabadiliko ya kazi mpya na zile za zamani kupitwa na wakati?

Kazi kama utengenezaji wa Memes, Stand up comedy, maigizo mafupi mafupi mtandaoni, online business, n.k je ni wakati wa kuzitambua na kuziheshimu ikiwa watumiaji wake wanapata pesa za kuendesha maisha yao na kuishi maisha mazuri ingawaje wale kina siye hatutaki kuona hilo?

Embu Acha nipumzike.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Mkuu kada iyo labda uitaje. Maana ile nyumba ya Mwijaku ikizidi sana labda Mil 200 na kuna mtu anapokea kiinua mgongo mil 300 ashindwe kusimamisha mjengo kama ule?

Milioni mia tatu ukipewa sasa hivi huwezi jenga nyumba ya milioni mia tatu sana sana ukijitahidi saaana milioni mia.
 
Wanaoweza ni wale wenye zaidi ya iyo milioni miatatu.

Wanaopewa mikopo asilimia 90 wanashindwa kufanya kile walichokopea.
Nyumba ndio kitu rahisi kujenga kama una kipato endelevu. Kuna watu wana nyumba za 300m ukimshtukiza leo lete 5m hana, wengi tu. Kwanini? Kwasababu hakujenga kwa sababu ana 300 au 500m benki,kajenga taratibu leo kapata 1m kesho 5m keshokutwa 3m mpaka anamaliza ujenzi. Haihitaji uwe na 300m benk au zaidi ili ujenge nyumba ya 300m ni kuwa na kipato endelevu na nia thabiti.
 
Kazi kama utengenezaji wa Memes, Stand up comedy, maigizo mafupi mafupi mtandaoni, online business, n.k je ni wakati wa kuzitambua na kuziheshimu ikiwa watumiaji wake wanapata pesa za kuendesha maisha yao na kuishi maisha mazuri ingawaje wale kina siye hatutaki kuona hilo?
Kila kazi na iheshimiwe.
NB: Kazi ni shughuli yoyote halali inayokuingizia kipato.
 
Back
Top Bottom