Kuna unyang'anyi wa kidola unaendelea Tanzania

Wanajanvi, kabla ya kuleta thread hii nimejiridhisha kutoka chanzo zaidi ya kimoja, leo asubuhi kuna mtu amenipa habari za kushtusha, sikutaka kuamini lakini nikaenda chanzo kingine na chenyewe kikajiridhisha toka chanzo kingine na wakasema ni kweli.
Ni hivi sasa hivi matajiri wananyanganywa pesa zao na serikali bila kupenda, wakija wakakukosa kwenye kodi wanakwambia kinagaubaga kwamba kodi yetu inaonekana unalipa vizuri lakini unaonekana una pesa nyingi kwenye account zako, kwa hiyo kinachofanyika wanakwambia tunataka kiasi fulani la sivyo tutafunga account zako! Mfanya biashara anakuwa hana namna zaidi ya kuachia mzigo!. Hii habari ni ya kustusha sana kwa nchi inayoendesha utawala wa sheria. Huu ni ujambazi wa kidola na haukubaliki.
Kwa hiyo kama una pesa nyingi kwenye account zako be vigilant ujambazi huu hauchagui lakini kibaya zaidi unaiangamiza nchi yetu watu wanakimbiza mitaji nje.
Hillo unalosema nikweli nikianza naoparesheni sangara huku ziwa Tanganyika wamekuta uvuvi sio haram lakini kwakuwa pesa ndio ilikuwa shida yao wamechoma nyavu bilautaratibu nakunyanganya engine za uvuvi nakusema zikakombolewe kwa pesa laki 5 kilamashine na engine zingine nikwaajili ya kufanya safari za maboat kubeba mizigo na abiria kutoka sehemu kwenda sehemu zote wamekusanya sasa tunajiuliza kwanini hivi shida niuvuvi haram za maboti unashika zanini serekali imeamua kukaba azarani kwa kisingizio cha tokomeza uvuvi haram utasikia tumekuasanya mapato kweli nawanajisifu sema tumedhulumu watu sio kukusanya mapato
 
Kaisome post niliyoijibu kwa bandiko hilo.

Nani alikwambia Magu hanunui papai?
Zakia Megji alikuwa kimya muda mrefu wa kukosa ulaji na ww ukawa kimya. Mara tu kapata ulaji na ww umeanza kutokea jukwaani. Ni bahati mbaya au tuunganishe dots?
 
Hebu%20jaribu%20kueleza%20ujumbe%20una%C3%B2jitokeza%20kwenye%20mchoro%20huu%20wa%20katuni%20...jpeg
 
Kuna Mama alichelewa kufuatilia hela ya Miradhi ya mume wake, akakuta akaunt iko dormant na hela iliyokuwepo, 4.3 Mill imepelekwa Hazina, tena ya Dodoma, so Bank husika ikamuomba mama afuatilie huko, wao wameelekezwa na BOT kuwa hela za namna hiyo apewe hazina kuzitunza
 
Mtoa mada anaonekana kuwa hana upeo mkubwa wa uelewa na anatutaka nasi kushabikia propaganda zake zisizo mshiko,wala ushahidi wowote,inaoneka kama vile anataka kuwatisha baadhi ya wajasiliamali wawe na wasiwasi na serikali yao, hizi habari inaonekana dhahiri kuwa ni za kutungwa na ndio maana hakumtaja hata mfanyabiashara aliyenyang'anywa pesa zake na serikali, ni wajinga wachache tu ndio wataamini upuuzu huu.
Wewe ita propaganda....mie nimemuamini 100%
 
Juzi Rais katangaza waziwazi TRA wasiwabughudhi wananchi kwa estimates za kodi. Siku ya pili naibu Waziri akamsimamisha kazi Afisa Mwenye cheo wa TRA Dodoma kwa makosa ya kubughudhi wafanya biashara.

Leo serikali hiyo hiyo ifanye aliyoleta mleta mada?

Labda angesema kuna maafisa walio waaminifu wanafanya hayo ningemuelewa. Lakini dola? Hapo bado kabisa kutuaminisha wengine.

Sasa hivi kinachoendelea hapa JF ni wale wa upinzani kuja na kila uongo wa kuipaka matope serikali ya CCM. Nahisi wale vijana waliokuwa kitengo cha IT cha ukawa safari hii wameanza mapema fitna zao za kijinga.

Lakini wanaharakati wa CCM tunawahakikishia kuwa tupo macho na hatujasinzia.
Kwani 25%ya waastaafu kaleta nani? 15 % kaleta nani? Ni nani huyu anayejiita raisi wa masikini huku akibana kuongeza mishahara na kuongeza makato kama ya heslb? Serikali hii inajiombea upofu wa jicho moja ili wewe upate wa macho yote
 
Ajabu! Huu uzi nilijua utafungwa jana au angalau ungepewa kile kianzio pendwa; Tetesi. Au labda kuna kweli, Mo na mfanyabiashara Zachari mzee wa mabinduki mkuje huku mtueleze.
 
Back
Top Bottom