Kuna unyang'anyi wa kidola unaendelea Tanzania

Tatizo linakuja pale ambapo una vielelezo vyote kama Mo lakini watu wanataka pesa yako kwa nguvu siyo kodi.
Acheni kudanganyana! Yani nawewe unaamini Mo kachukuliwa Trillion 1...!!!! uo uendawazimu
 
Kuna viashiria vya unyang'anyi wa kidola, kwenye sheria kama hizi, bodi ya mikopo kukata asilimia 15 kwa wanufaika wote regardless ulikuwa na mkataba wenye asilimia pungufu ya hiyo wakati wa kukopa, sheria mpya ya mifuko ya hifadhi za jamii. Kama hayo yamewezekana ya mleta mada si ya kubeza hata kidogo.
Hayo yote uliyoandika yana ushahidi, tuambie hilo kwenye thrd lina ushahidi gani? Tusikusanye maudhi yote tuliyonayo ili kuhalalisha yasiyo na ushahidi.
 
Utafikiwa tu siku moja na dikteta na utaamini but it will be too late! Walianza akina Lissu, ukanyamaza. Wafanyabiashara, unabisha. Waandishi wa habari, ukanyamaza. Mabenki, ukasema wapiga dili. Mafao ya wafanyakazi, umenyamza. Kuna siku itafika kwako. Ndio sheria ya udikteta.
Twende na Magufuli 2020.
 
Juzi Rais katangaza waziwazi TRA wasiwabughudhi wananchi kwa estimates za kodi. Siku ya pili naibu Waziri akamsimamisha kazi Afisa Mwenye cheo wa TRA Dodoma kwa makosa ya kubughudhi wafanya biashara.

Leo serikali hiyo hiyo ifanye aliyoleta mleta mada?

Labda angesema kuna maafisa walio waaminifu wanafanya hayo ningemuelewa. Lakini dola? Hapo bado kabisa kutuaminisha wengine.

Sasa hivi kinachoendelea hapa JF ni wale wa upinzani kuja na kila uongo wa kuipaka matope serikali ya CCM. Nahisi wale vijana waliokuwa kitengo cha IT cha ukawa safari hii wameanza mapema fitna zao za kijinga.

Lakini wanaharakati wa CCM tunawahakikishia kuwa tupo macho na hatujasinzia.
unaonaje tukianza na #MEMBE
 
Ungetaja idara inayofanya hivyo kwa wafanyabiashara inawezekana ni lambda kijikundi cha watu matapeli. Huyo mtoa habari wako angekuambia na ACCOUNT ya serikali na Bankambayo pesa hizo zinaingizwa
Kwenye uharifu don't expect that kind of tranaparency
 
Hayo yote uliyoandika yana ushahidi, tuambie hilo kwenye thrd lina ushahidi gani? Tusikusanye maudhi yote tuliyonayo ili kuhalalisha yasiyo na ushahidi.
Unataka ushahidi gani wakati humu humu kwenye watu wametoa ushuhuda yamewakuta wao. Soma comment zote siyo unarukaruka tu
 
This is coordinated mzee, uharamia unapofanywa na dola utakimbilia wapi, ndo maana watu wanakimbizia mitaji nchi jirani. Hivyo vyombo ulivyovitaja ndo vilituletea picha za cctv za kamera ya simu, they have to comply with the situation.
Ziweke hizo picha za CCTV ili wahusika waumbuke
 
Hayo yote uliyoandika yana ushahidi, tuambie hilo kwenye thrd lina ushahidi gani? Tusikusanye maudhi yote tuliyonayo ili kuhalalisha yasiyo na ushahidi.
Ushahidi wa kimazingira, kwenye matukio kama hayo na watendaji kama wale kamwe hutopata ushahidi unao utaka.
 
Back
Top Bottom