Kuna uhusiano gani kati ya Pesa, Umasikini na kelele

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,586
15,370
Mara nyingi mahala ambapo kuna Pesa au watu wamefanikiwa huwa kuna utulivu.

Masoko ya matajiri (supermarkets na Malls) huwa ni patulivu kuliko uswahili masoko yetu.

Wanapokaa matajiri (masaki, Oysterbay, Kapripoint (mwanza) ) huwa ni patulivu kuliko kwetu uswahilini.

Maskini huwa wanakelele nyingi sana, maneno maneno hata ukifika kwenye duka au ofisi kubwa utamjua tajiri kwa utulivu. Mfano yule jamaa anayepiga promo ya magari (Doi Macehicle) na Bosi wake Issa.

Mtu yeyote akiwa hajatoboa huwa anakelele kelele ila akizipata unaona anapoa anakuwa mkinya hakurupuki.

Siasa za nchi masikini zinakelele nyingi balaa, ila kwa matajiri zinaenda softly tu kimyakimya.

Hii ni dunia nzima.

Wakuu kuna uhusiano gani kati ya Pesa/Mali umasikini na kelele.
 
Back
Top Bottom