Kuna Uhalali au ulazima kwa kampuni za simu kutoa namba za simu za mtumba (zilizotumika na watu wengine walio hai au kufa)?

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Mar 1, 2016
12,695
31,480
Wasalaam wana JF

Nilikua nachangia kwenye uzi mmoja uliokua unajadili ulazima wa kuhifadhi number za simu za marehemu, nikawaza kwa maandishi, JE KUNA SABABU GANI YA KAMPUNI ZA SIMU KUTOA NAMBA ZA SIMU ZA MTUMBA?

Kwangu mimi, kumiliki number ya simu ya mtumba (iliyotumiwa na mtu mwingine aliye hai au aliyekufa) inaweza kukuweka kwenye mazingira yasiyo rafiki.

Nawaza tu, mathalani huyo mtu alikua ni kicheche au mkopaji sugu, unaweza ukapigiwa simu kibao na michepuko yake au wadai.

Nadhani kampuni za simu ziliangalie hili katika mapana yake. Kuna hesabu za probability tulifundishwa kwamba kwa idadi ya number tulizonanzo kwenye number zetu za simu, wanaweza wakaendelea kutoa number bila ya kurudia kwa miaka 100

Ikishindikana watuambie wateja kwamba hizi ni number mpya na hizi ni za mtumba (yaani zimetumika) ili mteja aweze kufanya an informed decision

Kama unabisha andamana
 
TUMSIFU YESU KRISTO.... NI KWELI INAKERA SANA WE WAZIA NAMBA YAKO YA MTU WA KARIBU ALISHAKUFA ILA UNAKUTA NAMBA YAKE BADO IPO HEWANI

AU ULIE KUWA UNAMDAI ALIKUFA NA DENI LAKO NA UNAJUA DENI LINAVYOUMA SIKU UNASEMA HEBU NGOJA NI JARIBU KUPIGA UNAKUTA SIMU INAITA
Kwangu mimi hii ni kama wana nia ya kuchonganisha wananchi
 
Kuna siku tulikuwa kwenye semina, wahusika walituambia kuwa hizi namba wao huwa wanalipia kwa mamlaka zinazohusika.
Kwa hiyo mtu akiacha kutumia kwa miezi kadhaa mchakato wote wa kuiingiza sokoni hiyo namba kwa mteja mpya huanza.
Badala ya kutengeneza namba mpya na kuongeza idadi ya gharama za kulipia wanaamua kuziingiza sokoni tena zile ambazo hazitumiki kwa muda mrefu.
 
Katibu Muenezi, baba wa wanyonge, Muheshimiwa sana, Paul Makonda wananchi tuna kilio chetu
 
Kuna siku tulikuwa kwenye semina, wahusika walituambia kuwa hizi namba wao huwa wanalipia kwa mamlaka zinazohusika.
Kwa hiyo mtu akiacha kutumia kwa miezi kadhaa mchakato wote wa kuiingiza sokoni hiyo namba kwa mteja mpya huanza.
Badala ya kutengeneza namba mpya na kuongeza idadi ya gharama za kulipia wanaamua kuziingiza sokoni tena zile ambazo hazitumiki kwa muda mrefu.
Hii ni shortcut ya kijinga kwenye mfumo wa kijinga.

Hiyo fee inatakiwa iwe ndogo kiasi kwamba, ukimpa mteja wa mwisho hiyo fee kama "connection fee" hata asijali sana. Na aelewe kuwa hiyo connection fee itampa namba mpya ambayo haitakuwa na usumbufu wa kupigiwa na watu asiowajua wanaomtafuta mtu tofauti.

Watu wengi wakipewa hii elimu na kupewa a reasonable one time connection fee, watalipa hiyo fee tu.

Tatizo unaweza kukuta mfumo wa kijinga unaweka li fee kubwa, kwa kuongeza namba tu, mpaka makampuni ya simu yanatafuta shortcuts. Katika zama hizi za teknolojia kweli watu wanashindwa kuweka mfumo wa kuhimili namba? Mimi nafikiri kitu cha muhimu ni resources kama bandwidth, IP addresses (ambazo zinaweza kuwa katika dynamic lease ya miezi kadhaa na hivyo zikabadilika kadiri ya matumizi) etc.

Suppose mtu kafanya kosa kubwa la jinai, kwa kujua hivyo kaitelekeza namba. Haya makampuni hayaoni kuwa kuanza ku trace nani alikuwa na namba lini yanajitengenezea kazi kubwa zaidi na kuwekea maswali mambo ya chain of custody kuliko kuwa na mtu mmoja tu mwenye hiyo namba?
 
Hii ni shortcut ya kijinga kwenye mfumo wa kijinga.

Hiyo fee inatakiwa iwe ndogo kiasi kwamba, ukimpa mteja wa mwisho hiyo fee kama "connection fee" hata asijali sana. Na aelewe kuwa hiyo connection fee itampa namba mpya ambayo haitakuwa na usumbufu wa kupigiwa na watu asiowajua wanaomtafuta mtu tifauti.

Watu wengi wakipewa hii elimu na kupewa a reasonabke one rime fee, watalipa hiyo fee tu.

Tatizo unaweza kukuta mfumo wa kijinga unaweka li fee kubwa, kwa kuongeza namba tu, mpaka makampuni ya simu yanatafuta shortcuts. Katika zama hizi za teknolojia kweli watu wanashindwa kuweka mfumo wa kuhimili namba? Mimi nafikiri kitu cha muhimu ni resources kama bandwidth, IP addresses (ambazo zinaweza kuwa katika dynamic lease ya miezi kadhaa na hivyo zikabadikika kadiri ya matumizi) etc.

Suppose mtu kafanya kosa kubwa la jinai, kwa kujua hivyo kaitelekeza namba. Haya makampuni hayaoni kuwa kuanza ku trace nani alikuwa na namba lini yanajitengenezea kazi kubqa zaidi kuliko kuwa na mtu mmoja tu mwenye hiyo namba?
Hakika, kingine wanapaswa wamfahamishe mteje mpya (disclosure) kwamba hiyo number imetumika, ili mtu afanye an informed decision
 
Hakika, kingine wanapaswa wamfahamishe mteje mpya (disclosure) kwamba hiyo number imetumika, ili mtu afanye an informed decision
Hapo kwenye transparency na disclosure nafikiri kuna tatizo kubwa sana la utamaduni.

Kuna siku nilikuwa likizo Dar, nikaenda pale Mlimani City, natafuta namba ya Tanzania kutumia kwenye likizo.

Sasa, matangazo yao ya vifurushi na bei yakawa kama hayaeleweki eleweki hivi.

Nikaanza kuwauliza, maswali yangu yakawa technical na detail oriented.

Wale jamaa badala ya kujibu maswali, wakawa kama wananishangaa na kunipa vibes zile za "Wewe vipi? Mbona unakuwa kama hujui style zetu za kibongo?".

Yani kifupi vifurushi vilikuwa na false advertisement kibao, halafu wao walikuwa washazoea watu wananunua bila maswali, mimi nilivyokuja na maswali wakawa wananishangaa.
 
umeandika kitu kikubwa sana, ni reflection ya aina ya watu tulionao kwenye jamii yetu na kwenye soko la ajira. Utendeaji wa hizi kampuni za simu ni reflection ya product za wahitimu wetu
 
Unajua kuna kipindi TCRA walitaka kuja na mfumo wa Number managment portability (NMP).
Hii ilikuwa inatakiwa kuwa mtu anakuwa na umiliki halali wa laini yake, kwa maana kwamba unaweza kutoka mtandao mmoja ukahamia mtandao mwingine kwa kutumia laini hiyo hiyo.

hili wazo lilikuwaga zuri na ingesaidia sana endapo mtu asingefurahishwa na huduma za mtandao fulani basi anahamia mtandao mwingine bila kupoteza majina ya watu wake.

Sijui mpango ule uliishia wapi, ila kuna nchi wana hizi mifumo, na kuhusu laini yako kupewa mtu mwingine nilishawahi sikia kwamba ni bora watumie line hizo kuliko kuandaa zingine sababu ya gharama.
 
Wanatuchanganya sana hawa makampuni ya simu. Mi nilipoteza simu yenye laini mbili za kampuni mbili tofauti, baada muda watu wangu wanaonipigia kwa namba hizo zinapokelewa na watu wengine. Nimefuatilia nirudishiwe namba zangu nikajibiwa kapewa mtu mwingine. Wanadai laini isipoonekana hewani kwa muda wa miezi miwili/mitatu anapewe mtu mwingine. Sasa sijui kama hiyo namba itakuwa na wamiliki wawili kwa mujibu wa usajili au huwa wanafuta usajili wa awali ili apewe mtu mwingine. Mi mwenyewe nimewahi kupewa namba ya mtu mwingine nikawa nasumbuliwa kila wakati napigiwa simu na nisiowajua
 
Unajua kuna kipindi TCRA walitaka kuja na mfumo wa Number managment portability (NMP).
Hii ilikuwa inatakiwa kuwa mtu anakuwa na umiliki halali wa laini yake, kwa maana kwamba unaweza kutoka mtandao mmoja ukahamia mtandao mwingine kwa kutumia laini hiyo hiyo.

hili wazo lilikuwaga zuri na ingesaidia sana endapo mtu asingefurahishwa na huduma za mtandao fulani basi anahamia mtandao mwingine bila kupoteza majina ya watu wake.

Sijui mpango ule uliishia wapi, ila kuna nchi wana hizi mifumo, na kuhusu laini yako kupewa mtu mwingine nilishawahi sikia kwamba ni bora watumie line hizo kuliko kuandaa zingine sababu ya gharama.
Upo na unafanya kazi
 
TUMSIFU YESU KRISTO.... NI KWELI INAKERA SANA WE WAZIA NAMBA YAKO YA MTU WA KARIBU ALISHAKUFA ILA UNAKUTA NAMBA YAKE BADO IPO HEWANI

AU ULIE KUWA UNAMDAI ALIKUFA NA DENI LAKO NA UNAJUA DENI LINAVYOUMA SIKU UNASEMA HEBU NGOJA NI JARIBU KUPIGA UNAKUTA SIMU INAITA
Wala usihofu mpendwa! Kila kitu kinaenda katika mizania ya haki! Mpendwa ebu nikujibu kikristo! Mitandao ya simu inarejesha kwa usajili mpya kama line ya simu itakuwa dormant kwa kipindi cha mwaka mmoja! Kisheria katika mizania ya haki mmiliki wa hiyo line anakuwa amepoteza sifa ya uhalali wa umiliki wa line asipoitumia kwa kipindi cha mwaka mmoja! Ukipewa ukaisajili kwa namba mpya na jina la NIDA kuanzia hapo ni mali halali yako! Makampuni ya simu lazima yafanyehivyo vinginevyo namba zitaisha. Kwa mfano: namba ya utambulisho wa mtandao husika ni namba nne za mwanzo yaani "0712" zinazofuatia ni jumla ya namba 6. Hizi namba sita unaweza kuzipanga bila kujirudia 9x9x9x9x9x9=531,441.
Kwahiyo namba moja ukiiondoa kwenye matumizi kwasababu eti mtumiaji ana rekodi mbaya inakuwa ni hasara kwa kampuni na mwisho wa siku wataishiwa na namba. Hivyo namba isipotumika lazima apewe mtumiaji mpya na maisha yaendelee
 
Back
Top Bottom