Kuna ugomvi wa chini chini India dhidi ya Tanzania?

Kuna ugomvi wa chini chini India dhidi ya Tanzania?

Uchumi ni sectors. The more the economic sectors the more and healthy economy. If one sector is withdrawn or doesnt funcrtion properly the economy will jeopardise. So the handsome economy is a function of more generating sectors.

Note! Ni zito huyuhuyu aliyesema mwaka huu kutakuwa na njaa kali kwa sababu mazao hamna lakini hamna njaa. Kwa hiyo take him with precaution he only wants to disaproove jpm at the expense of jk( swahiba wake)
Mungu abariki wasomi wa Tanzania......kama hiyo ndo analysis ya msomi wa kiwango cha Phd duh!!!! Elimu ni kweli bure
 
Kwa hali ilivyo huko serikalini na mtaani msitegemee any positive changes toka kwa mchato,zaidi zaidi kwa kujijua kachemsha na mambo yamekwama atatumia jeshi na TISS kunyanyasa na kuua watu ili kuzima criticisms. So watanzania tuamue moja kati ya haya mawili.
1. Kujitoa kwa hari,mali na kwa maumivu makubwa kupambana na huu mfumo mpya anaojaribu kuujenga huyu mchato.
2. Kukaa kimya kama yote haya yanayotokea sasa na yanaendelea nchini hayatuhusu.
 
Kuna nini Tanzania na India

Kwenye ziara tunayotembelea madiwani wetu wa ACT Wazalendo kuna jambo nimeliona linajitokeza mahala pengi kila ninapoongea na Wananchi. Jambo hilo ni kushuka kwa bei za mazao ambayo Wakulima walikuwa wanategemea soko la India. Mbaazi, Choroko, Dengu na giligilani ni baadhi ya mazao ambayo nimesikia malalamiko makubwa ya bei zake.

Jana nilipokuwa Sumbugu, Misungwi Wananchi walinieleza kuwa mwaka 2016 waliuza choroko kwa shilingi 300,000 kwa gunia Lakini bei hiyo ilishuka mpaka shilingi 150,000 na kwamba wanunuzi wamepungua mno. Vile vile Dengu imeshuka sana bei kutoka shilingi 7000 kwa kilo 4 hadi kufikia shilingi 2500.

Nilipokuwa Gehandu, Hanang nilielezwa kuwa bei ya giligilani imeshuka kutoka shilingi 150,000 kwa gunia mpaka shilingi 25,000 tu.

Chama chetu kilifanya utafiti wa zao la mbaazi kwa mikoa ya kusini mwaka Jana. Kadhia ya mbaazi tumeikuta pia Mkuranga, Morogoro na Mkoa wa Manyara. Bei imeshuka kutoka wastani wa shilingi 1500 kwa kilo mpaka shilingi 50 kwa kilo na maeneo mengine hakuna soko kabisa.

Swali
Mazao yote haya yaliuzwa India. Kwanini Bei zimeshuka na masoko kuanguka kabisa wakati mahitaji ya bidhaa hizi huko india yanakua mwaka hadi mwaka? Kuna nini kati ya Tanzania na India? Kuna nini Wakulima na Watanzania hawaelezwi?

Ndugu Zitto, Ukweli ni kwamba serekali ya India imefungia uingizaji wa Pulses kutoka njee kuwalinda wa kulima wao, baada ya bei ya mbaazi kuanguka India kutoka IR150/- to IR 45/-. Wakulima India wameshindwa kuuza mazao yao NA wengi wamejiua kwa sababu ya hasara NA maneno.

If you goggle TUR DAAL scandal in INDIA utapata majibu mengi sana. Wafanyi biashara wa India kabla ya kuja TZ kwanza wananunua mazao hayo Myanmar, Vietnam NA nchi karibia NA kwao than they come to Africa.

Hii site hapo chini itakuonyesha wakulima katika jimbo la Maharashtra wanavyoteseka NA zao la mbaazi:
Maharashtra wants farmers hit by falling tur dal prices to mortgage the crops | cities | Hindustan Times

2015 bei ya mbaazi ilipanda sana kwani kulikuwa NA mchezo uliofanywa NA cartels in India to manipulate the prices of Mbaazi, hili lilisababisha serekali katoa stock yao NA kiingiza sokoni kuangusha bei. Soma hapa chini;

The great Indian Dal scam revealed

Kuna mambo mengine hayahitaji siasa na kuabishana pasipo NA ukweli.
 
Toka lini taifa linaloendeshwa na mtu alitakiwa awe machungani anachunga ng'ombe likafanikiwa kibiashara.Tumtoe kwanza huyu mfugaji ndo hata biashara za kimataifa zitakuwa.
 
Mi nilitarajia mtu kama Zito aje na majibu mujarabu badala ya kuuliza swali. Zito ni msomi wa uchumi naambiwa, Mbunge mkongwe na kiongozi mzito katika Nyanja nyingi. Zitto, come up with an analytical, clear and simple answers to your humble people instead of difficult questions.
 
Rais amelala usingizi wa nusu kaputi kuhusu shida halisi za watanzania, na akikurupuka kutoka usingizini basi ni kufukuza watendaji wake, kununua na kuwaangamiza wapinzani na mwisho kuvamia bandarini na kujidai kukamata cargo zilizoagizwa na taasisi za serikali.

Mawaziri nao wamekuwa kama kuku wa kienyeji, kutwa kuzurura ovyo na kudokoa dokoa (kutatua shida ndogo ndogo za mwananchi mmoja mmoja na hapo hapo kuwaadhibu watumishi wa umma) na mwisho wanawika kama kuku (Wanaropoka matamko yasiyokuwa na kichwa wala mkia ili kutafuta kick).

Serikali imepoteza mwelekeo.
Taifa limepoteza mwelekeo.
Nchi inazidi kuangamia kwa kasi.
Mkuu... Agiza Soda, umenena mpaka nimefrahi safi sana this is JF
 
Ni mambo madogo tu yakidiplomasia
Bila shaka Serikali itayamaliza kabla ya Msimu ujayo

Jibu ulilolitoa nadhani walikuwa walitoe wale tuliowazoea, sasa utawapa KAZI kweli kutunga SENSTENSING( Refer quote from SRM - Mbeya on Sugu Judgement) nyingine kaka, sio vizuri hivyo utaitwa mchochezi bure 🙂 🙂🙂😀😀😀😀😀
 
Matatizo ya bei ya mbaazi India, Ndugu ninawekea links ya matatizo ya bei huko India. Ikiwa bei ni chini kwa hilo zao ambalo wao ndio walimaji wampjawapo wakubwa ulimwengini ni India.
Farmers protest against government decision of fixing toor dal price | The Economic Times Video | ET Tv

Ukitaka kujua bei ya mbaazi ama mazao in India tumia link hii; itakusaidi kujua ukweli NA kuepuka na propaganda za wanasiasa NA utafutaji wa kiki za kisiasa, pia utaepuka na uchonganishi usiokuwa NA tija.

Agriwatch - Tur (Pigeon Pea) Prices in India, Tur (Pigeon Pea) News, Tur (Pigeon Pea) News India,Tur (Pigeon Pea) Supply and Demand, Tur (Pigeon Pea) Import and Export, Tur (Pigeon Pea) Production and Consumption in India, Tur (Pigeon Pea) Markets, Tur (Pigeon Pea) Price outlook and Price forecast
 
effect ya manji kua harrassed na akina mo wakasusa kununua, mkumbuke yule mkandaras wa india rais alimnyang'anya passport kule mtwara bila kutumia demokrasia hayo ndio malipo india imetulipa.

Manji ni mtanzania wala sio raia wa India, wahindi waliokuja tanzania walikuja kabla ya India kupata uhuru, NA ilikuwa haijagawanywa kuwa India, Pakistan NA Bangladesh . wengi wao hawajitambui wawe sehemu gani. Ila ukweli wao ni watanzania leo NA kesho.

Ni aibu kujifanya is msomi NA unajibu hoja bila kutafakari NA kufanya research.
 
Yeye ni Dar-Mwanza-Chatto au akijitahidi sana ni Dar-Kampala- Chatto..
Tanzania sijui imekumbwa na balaa gani Mungu wangu.
Kikwete ndio katuletea yote haya,, bora tu angaemuacha Rafiki yake Lowasa asimamishwe na chama,, kuliko kumfanyia roho mbaya ili Membe ndio awe mgombea, ,hatma yake sasa ndio haya, wakulaumiwa ni JK,, ni Kheri mapungufu ya Lowassa kuliko huyu Ngosha, ,,Lowasa kwanza
hana roho mbaya
 
Kwanza maajenti wakubwa wa makampuni ya India yanayonunua haya mazao ni hawa wafanyabiashara wetu hapa Bongo kama kina Manji, Mo and the likes. Kitendo cha kuwa destabilize wao, kunawafanya kutopromiti effectively hayo mazao India kwa wateja wao. Kumbuka Marketing in the competitive world is a continue issue. WAMESUSA.

Pili. Serikali kuingilia ingilia biashara na kufikiri kuongea na serikali ya India ndo kutafanya hao wafanyabiashara wanunue. NOPE!!! Mahusiano ni kati ya biashara na biashara. Serikali ya India haina kiwanda wala duka.

Sisi wa alizeti, hata mashudu hayaendi tena India.Halaf diplomasia inainua biashara sana. Tena kwa impact kubwa. Mkuu wa nchi anapotoka yeye mwenyewe kwenda kwa mkuu wa nchi nyingine kuyajenga inashawishi kiheshima zaidi kuliko kutuma tuma watu walio chini yake. JUST THINKING LOUD!!

Nyie ndugu zetu hamueleweki, kikwete alipokuwa anatembea kuijenga nchi mlimsema NA kumtusi, huyu kagoma kusafiri mnamsema.

Siku akianza safari pia mtamsema. Hakuna Jema kwenu, TANZANIA HAINA SHIDA YA ADUI WA NJEE, TUNAO MAADUI WA NCHI HUMU HUMU NYUMBANI.

Hi ni laana kubwa sana
 
India ni nchi muhimu sana,
na ndipo soko lilipo hasa ,kama watu vichwa ngumu na arrogant kama Netanyao wanaenda india na kukaa wiki wakiunganisha deal za biashara,

kina Rohani wanapishana kwenda india kuingia makubaliano ya kibiashara,

putin mbele ya mhindi ananyenyekea ili auze ndege zake,

hata marekani akifika kwa mhindi kiburi anaweka pembeni ili aivute india kwenye kambi lake,

itakuwa sisi ambao uchumi wetu wameshikilia hawa wahindi?.

Hawa watu wanaushirikiano sana,na haijalishi huyo mhindi kazaliwa mpanda ama uyole,maadamu ni mhindi,wao wanahesabu ni mtu wao tu
 
Hehehe wewe kweli limbukeni hivi hapa Tanzania kuna tajiri ambae akiguswa serikali itatetereka, hao walanguzi unawaita matajiri?

Na wakina eBay, Amazon, Facebook, Google, alibaba, Apple, hawa ndio matajiri ambao serikali zao zinawahusudu na wana impact kubwa kwenye chumi za mataifa yao

Sasa wachuuzi wa mbaazi ambayo kila mtu anaweza kufanya hiyo biashara ndio unawaita matajiri, wasifuate utaratibu wa Tanzanite yetu sababu choroko zitatudodea? Una hasara
Acha dharau na kujidanganya, kama kila mtu anaweza kununua mbona ww hujanunua mbaazi za wakulima ?
 
Jibu:

India imeweka kodi kwenye mbaazi. Ilikuwa 0% ila kuanzia tarehe 8/11/2017 mbaazi zitatozwa kodi 50%. Hiyo inamaaniasha kuwa bei price imekatwa by 50%. Pia kuna rules zingine wameweka kuhusu fumigation kwenye mazao, na kupunguza quota za importation, etc. Hii wamefanya ili kulinda pia wakulima wa India ambao walikuwa wanashindwa kushindana na Canada, USA na Australian farmers.
Kunde choroko na vingine vimewekewa tarrif ya 30% mwezi Desemba mwaka jana.

Siyo Tanzania tu, hata United States na Canada wamekuwa affected vibaya sana na hatua hii. Pia, siyo kila kitu ni ugomvi. Vingine mara nyingi ni mambo ya biashara tu.

View attachment 703452

India imeanza kuzalisha mazao hayo pia katika rate ya 1960s. Uzalishaji wa mbaazi india umepanda kwa kiasi kikubwa baada ya kuporomoka tangu miaka ya 80s.
Kobello, ktk Komenti zote zilizotolewa, na hata na thread yenyewe, wewe ndiye uliyepost scientifically. Umemaliza mjadala. Mengine ni stori za kitaa tu.
 
Back
Top Bottom