Kuna ugomvi wa chini chini India dhidi ya Tanzania?

Kuna ugomvi wa chini chini India dhidi ya Tanzania?

Si mlimfunga jamaa jela kwa masifa ya kise.nge, tulieni
 
Pia tungejaribu kuangalia kuanguka kwa mazao kama Nazi, kahawa na pamba enzi zile nini kilisababisha ndo iwe kama literature review zetu then sasa tutajua why now mazao haya. Unajua enzi zile sisi tulikua ndo wauzaji wakubwa wa bidhaa nlizotaja mpk zikapelekea baadhi ya nchi ikiwemo uarabuni kugombea kututawala lakini baada ya miaka kadhaa mbele zimekua sio kitu so yaezekana sababu iliyoiangusha bidhaa zile ndo the same zinayoitenda bidhaa hizi
Wachina wanafanya research nyingi apa Tanzania bila ya sisi kujua. Mfano mdogo hawa wachina wanachofanya ni izi bidhaa zote zinazozalishwa apa Tanzania za kilimo wanafanyia Research na wanaenda kuzalisha kwao na kuuza. Na wakisha zalisha wanauza bei ya chini kuliko kule, hawa wachina ni tatizo sio apa Tanzania tuuu, hata kwa mataifa ya USA na European. Wanaharibu biashara nyingi sana
 
Labda wahindi wenzi wa kizazi kipya wameacha kuwa vegetarians na vegan na wameanza kula nyama
 
Chini ya Utawala wa CCM na kwa Sample za Watawala tulionao, hakika Maendeleo kuifikia Kenye tu Itatuchukua si Chini ya Miaka 50!
 
Mataifa mengi duniani yanajua na kusimamia uzalendo kwa taifa na watu wake. Unapo mgusa raia wao kwa harrasment wao huonyesha positive action.

Diplomasia ya kimataifa imepoteza mwelekeo hususani diplomasia ya kiuchumi,rais ana kwepa kwenda ziara za nje ya East Africa ambapo angeweza kukutana na marais wenzake na kutafuta fursa za kiuchumi yeye ana kazi ya Ku share uzoefu wa kidiktekta na madikitekta wakongwe wa east africa
 
A

Ana udoctor gani. Hivi ni vitu vya kawaida kila mtu ambaye hata hajasoma angeviona. Kwani hujui kuwa wahindi au india ndo ilikuwa namba moja duniani kuuza tanzanite wakati ni ya kwetu. Sasa kitendo cha jpm kuzungushia ukuta tanzanite yote isiibiwe tena au isiuzwe kimagendo huoni kama wahindi wamechanganyikiwa ns india kwa ujumla uchumi wake unaweza poromoka. Hili ni swala la mda tu na jpm amefanya la maana kwa maslahi mapana ya taifa. Acha akina zitto wabwabwaje mana hawana kiki tena siku hizi kama walivyotuaminisha zamani kwamba ni watetezi kumbe wezi tu
sasa unafikiri tanzanite itaacha kuibwa sababu imezungushwa ukuta??mambo mengine bwana
 
Kwanza maajenti wakubwa wa makampuni ya India yanayonunua haya mazao ni hawa wafanyabiashara wetu hapa Bongo kama kina Manji, Mo and the likes. Kitendo cha kuwa destabilize wao, kunawafanya kutopromiti effectively hayo mazao India kwa wateja wao. Kumbuka Marketing in the competitive world is a continue issue. WAMESUSA.

Pili. Serikali kuingilia ingilia biashara na kufikiri kuongea na serikali ya India ndo kutafanya hao wafanyabiashara wanunue. NOPE!!! Mahusiano ni kati ya biashara na biashara. Serikali ya India haina kiwanda wala duka.

Sisi wa alizeti, hata mashudu hayaendi tena India.Halaf diplomasia inainua biashara sana. Tena kwa impact kubwa. Mkuu wa nchi anapotoka yeye mwenyewe kwenda kwa mkuu wa nchi nyingine kuyajenga inashawishi kiheshima zaidi kuliko kutuma tuma watu walio chini yake. JUST THINKING LOUD!!
Manji anauraia wa India?
 
Yeye ni Dar-Mwanza-Chatto au akijitahidi sana ni Dar-Kampala- Chatto..
Tanzania sijui imekumbwa na balaa gani Mungu wangu.


Yaani hadi aibu kabisa ila ngoja tumsubirie na nadhani hapo alipo sasa hivi atajua kwanini kuna kitu kinaitwa Diplomasia maana sidhani kama hata uji unateremka kuna watu wamemkalia kooni acha wapambane nae tuu hakuna namna
 
Tukifanya kila tatizo chanzo chake kuwa cha kisiasa tutakua tunakosea hata Katika kutatua matatizo yenyewe.

Ungeenda mbele zaidi na kuja na concrete facts zinazosupport assumption yako kuwa kuna tatizo Kati ya Tanzania na India.

Ila ninachokiona hapa ni tofauti ya bei ya sasa na zamani.

Tuambie nini kimekufanya uhisi kuwa kuna tatizo Kati ya India na Tanzania?
 
India waliwajengea uwezo wakulima wao, kwasasa Hawa import hayo mazao,ila serikali yao ilishaingia mkataba na serikali yetu kununua ayo mazao. Kinachotakiwa waangalie namna ya kutupunguzia hasara.
 
Ni mambo madogo tu yakidiplomasia
Bila shaka Serikali itayamaliza kabla ya Msimu ujayo
Utetezi wa kitoto kuwahi kutokea! Yaani unataka wakulima wetu wa choroko wasubiri mdimu ujao wakati sasa hivi wameshaanza kupepeta choroko zao! Hata hivyo wacha cha moto tukione maana tulikuwa tunashangilia mno kwamba tumepata jembe, kumbe jitu lenyewe taahira! Natamani huku kwetu choroko ziuzwe shilingi 150 kwa kilo!
 
Utetezi wa kitoto kuwahi kutokea! Yaani unataka wakulima wetu wa choroko wasubiri mdimu ujao wakati sasa hivi wameshaanza kupepeta choroko zao! Hata hivyo wacha cha moto tukione maana tulikuwa tunashangilia mno kwamba tumepata jembe, kumbe jitu lenyewe taahira! Natamani huku kwetu choroko ziuzwe shilingi 150 kwa kilo!
Hakuna Nchi isiyo na Changamoto
 
Hehehe wewe kweli limbukeni hivi hapa Tanzania kuna tajiri ambae akiguswa serikali itatetereka, hao walanguzi unawaita matajiri?

Na wakina eBay, Amazon, Facebook, Google, alibaba, Apple, hawa ndio matajiri ambao serikali zao zinawahusudu na wana impact kubwa kwenye chumi za mataifa yao

Sasa wachuuzi wa mbaazi ambayo kila mtu anaweza kufanya hiyo biashara ndio unawaita matajiri, wasifuate utaratibu wa Tanzanite yetu sababu choroko zitatudodea? Una hasara
Umeeleza vizuri sana
 
Kuna nini Tanzania na India

Kwenye ziara tunayotembelea madiwani wetu wa ACT Wazalendo kuna jambo nimeliona linajitokeza mahala pengi kila ninapoongea na Wananchi. Jambo hilo ni kushuka kwa bei za mazao ambayo Wakulima walikuwa wanategemea soko la India. Mbaazi, Choroko, Dengu na giligilani ni baadhi ya mazao ambayo nimesikia malalamiko makubwa ya bei zake.

Jana nilipokuwa Sumbugu, Misungwi Wananchi walinieleza kuwa mwaka 2016 waliuza choroko kwa shilingi 300,000 kwa gunia Lakini bei hiyo ilishuka mpaka shilingi 150,000 na kwamba wanunuzi wamepungua mno. Vile vile Dengu imeshuka sana bei kutoka shilingi 7000 kwa kilo 4 hadi kufikia shilingi 2500.

Nilipokuwa Gehandu, Hanang nilielezwa kuwa bei ya giligilani imeshuka kutoka shilingi 150,000 kwa gunia mpaka shilingi 25,000 tu.

Chama chetu kilifanya utafiti wa zao la mbaazi kwa mikoa ya kusini mwaka Jana. Kadhia ya mbaazi tumeikuta pia Mkuranga, Morogoro na Mkoa wa Manyara. Bei imeshuka kutoka wastani wa shilingi 1500 kwa kilo mpaka shilingi 50 kwa kilo na maeneo mengine hakuna soko kabisa.

Swali
Mazao yote haya yaliuzwa India. Kwanini Bei zimeshuka na masoko kuanguka kabisa wakati mahitaji ya bidhaa hizi huko india yanakua mwaka hadi mwaka? Kuna nini kati ya Tanzania na India? Kuna nini Wakulima na Watanzania hawaelezwi?
Nashukuru Mh Zitto umelileta hili kama swali pamoja na kwamba majibu yake mengine ni ya wazi na mengine yatahitaji uchunguzi kidogo.
Utakumbuka mwaka jana 2017 ule msimu wa mbaazi ..bei zilidondoka sana. Na serikali iliupata ujumbe na ikahamaki kweli. Ghafla Waziri Mwijage akasema wanalifuatilia. Nakumbuka alifunga safari hadi India na aliporudi hakuwa na majibu tangible zaidi ya kusema kuna siasa kidogo na mambo ya kidiplomasia ambayo yatakuwa sawa..
Mimi nilifika rufiji na kukuta wakulima wamefungia mbaazi ndani. Wakadai si tu kwamba bei zipo chini ila hata hao wanunuzi wenyewe hawapo.
Angalau kidogo zao la ufuta waliuza ingawa bei ilikuwa ya hasara pia.
Hao wakulima waliendelea kudai wanunuzi wao wengi huwa ni wenye asili ya kihindi na wabongo wachache.
Kiukweli wamepata hasara kubwa. Wamenunua dawa za kuhifadhia lakini hakuna wanunuzi hadi leo.

Tukiacha yote ni kwamba kuna tatizo kubwa sana ktk uendeshaji wa uchumi wa nchi yetu awamu ya tano.
Angalau awamu ya kwanza ya BABA JKN ilieleweka inajenga uchumi gani na njia zilikuwa wazi. Hata hotuba za Baba wa Taifa ziliwaeleza wananchi nini cha kufanya.
Siijui kiundani awamu ya Mzee Mwinyi. Awamu ya Mkapa alieleweka ingawa Sera mbovu ya ubinafsishaji ilitumaliza..
Kikwete hakueleweka pia ila labda kilichomsaidia alikuwa na uwezo wa kuwasikiliza watu wenye maoni tofauti. Hiyo ilimfanya kidogo kuna sehemu asonge mbele na private sector ilijengeka sana awamu yake.

Sasa hii awamu ya tano haina dira na haitaki maoni yoyote yale..
Kiufupi kilimo , uvuvi , ufugaji na primary sector zinapitia ktk tanuri la moto na hakuna mipango ya pamoja ya kiwizara ya Ku contain hizo primary activities.

Jiulize huko kanda ya ziwa waziri kawachomea watu nyavu na mitumbwi. Halafu hakuna nyavu mbadala. Kuna nyavu ziko mpakani Sirari miezi sasa serikali haitoi vibali.

Hivi hiyo ni serikali inayosomana kweli?.

Anyway kila anayeshauri kwa kukosoa awamu hii anaitwa mpinzani na wanasema ashughulikiwe mara ndo alikuwa mpiga dili.

Wanajificha ktk koti la uzalendo ilihali ni wezi wakubwa na bora wangeishia kuiba tu bali pia wanaua uchumi wa watanzania wadogo.

Primary sector imeuwawa. Biashara ndogo ndogo zinapigwa kodi za kufa mtu. Biashara za uchuuzi zinaonekana haramu. Biashara kubwa zinauwawa na matamko na mikurupuko ya taasisi za serikali na rais mwenyewe.
Sasa kuna Uchumi hapo!!
Kazi watu wanasifu tu... Upuuzi..

Maigizo ni mengi kuliko uhalisia ktk serikali hii.
 
Rais amelala usingizi wa nusu kaputi kuhusu shida halisi za watanzania, na akikurupuka kutoka usingizini basi ni kufukuza watendaji wake, kununua na kuwaangamiza wapinzani na mwisho kuvamia bandarini na kujidai kukamata cargo zilizoagizwa na taasisi za serikali.

Mawaziri nao wamekuwa kama kuku wa kienyeji, kutwa kuzurura ovyo na kudokoa dokoa (kutatua shida ndogo ndogo za mwananchi mmoja mmoja na hapo hapo kuwaadhibu watumishi wa umma) na mwisho wanawika kama kuku (Wanaropoka matamko yasiyokuwa na kichwa wala mkia ili kutafuta kick).

Serikali imepoteza mwelekeo.
Taifa limepoteza mwelekeo.
Nchi inazidi kuangamia kwa kasi
.

Labda uko kwenu Zanzibar
 
Unataka kusema nini?

Kwamba tunaweza kumaliza kujenga ukuta alafu wanunuzi wakasema hawanunui tena Tanzanite?

Hebu jamani tuwe Wazalendo.
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Swali
Mazao yote haya yaliuzwa India. Kwanini Bei zimeshuka na masoko kuanguka kabisa wakati mahitaji ya bidhaa hizi huko india yanakua mwaka hadi mwaka? Kuna nini kati ya Tanzania na India? Kuna nini Wakulima na Watanzania hawaelezwi?
Jibu:

India imeweka kodi kwenye mbaazi. Ilikuwa 0% ila kuanzia tarehe 8/11/2017 mbaazi zitatozwa kodi 50%. Hiyo inamaaniasha kuwa bei price imekatwa by 50%. Pia kuna rules zingine wameweka kuhusu fumigation kwenye mazao, na kupunguza quota za importation, etc. Hii wamefanya ili kulinda pia wakulima wa India ambao walikuwa wanashindwa kushindana na Canada, USA na Australian farmers.
Kunde choroko na vingine vimewekewa tarrif ya 30% mwezi Desemba mwaka jana.

Siyo Tanzania tu, hata United States na Canada wamekuwa affected vibaya sana na hatua hii. Pia, siyo kila kitu ni ugomvi. Vingine mara nyingi ni mambo ya biashara tu.

upload_2018-3-2_0-57-35.png


India imeanza kuzalisha mazao hayo pia katika rate ya 1960s. Uzalishaji wa mbaazi india umepanda kwa kiasi kikubwa baada ya kuporomoka tangu miaka ya 80s.
 

Attachments

  • india.jpg
    india.jpg
    21.3 KB · Views: 55
Back
Top Bottom