Kuna ubaya gani kumpa zawadi hii?

Kuna ubaya gani kumpa zawadi hii?

Nina girlfriend wangu ambaye tumedumu miezi kadhaa na tumepanga kuoana pindi uchaguzi utakapomalizika!

Amehitimu chuo cha biashara tangu mwaka Jana na mpaka sasa hajafanikiwa kupata ajira!

Nafahamika kwa wazazi wake nae anajulikana kwetu.

Sasa jana alisherehekea siku yake ya kuzaliwa
sherehe ilifanyika nyumbani kwao mida ya saa 1 jioni.

Wiki moja kabla ya sherehe hiyo nilikuwa safarini nikamuahidi kumnunulia zawadi nzuri kwa ajili ya birthday yake.

Sasa hiyo jana alikuwa na shauku ya kutaka kujua nimemletea zawadi gani !

Mda ulipowadia nilienda taratibu kumkumbatia kipenzi changu na kumzawadia cherehani mpya aina ya butterfly pamoja na kuahidi mbele ya umati kuwa nitatoa gharama zote za mafunzo ya kozi ya miezi mitatu ya ushonaji ili baada ya kumaliza mafunzo aweze kujiajiri.

Lakini cha ajabu mpenzi wangu alionyesha hakufurahishwa na zawadi hiyo!

Jana usiku kanisms kwamba "umenichukuliaje mimi lakn?"

Nikampigia akasema eti alitegemea ningemnunulia zawadi ya maana kumbe hovyo!

Leo nimemtumia ujumbe tuonane hakunijibu nimejaribu kumpigia mda wote hapokei simu yangu!

Naomba mnishauri eti hiyo zawadi ina ubaya gani au ningemnunulia nini ikiwa sina uwezo wa kununua gari?!

Aiseee
Mh huo ugali kauzu.
Izo ndio shoo za kibabe
 
Umemiss nini? Niletee mwenyewe au mpe wifi Apologise lady aniletee maana wewe unaweza ukatokomea kama ulivyotokomea na zile hela zangu

Yaani ibra87 amenidhalilisha sa jana, eti mi napenda pesa, yeye alitaka nipende mawe, tena akinipa hiyo kadi aje na 100000 ya faini.
 
Last edited by a moderator:
Yaani ibra87 amenidhalilisha sa jana, eti mi napenda pesa, yeye alitaka nipende mawe, tena akinipa hiyo kadi aje na 100000 ya faini.

Daaaah!! Hiyo hela inatoka kwenye bajeti yangu au nje ya bajeti yangu?
 
Last edited by a moderator:
Daaaah!! Hiyo hela inatoka kwenye bajeti yangu au nje ya bajeti yangu?

Atajua yeye atatoa wapi?? Yeye anataka mi pesa iniogope, mim nataka pesa inizoee, ikiniona iniite.

Sitaki hata kumsemesha mdogo wangu ibra87, kwa kosa lakunitenganisha na pesa.
 
Last edited by a moderator:
Atajua yeye atatoa wapi?? Yeye anataka mi pesa iniogope, mim nataka pesa inizoee, ikiniona iniite.

Sitaki hata kumsemesha mdogo wangu ibra87, kwa kosa lakunitenganisha na pesa.

Hahahaaaa! Mtajuana wenyewe
 
Last edited by a moderator:
Cherehani na MASISTA du wapi na wapi kaka?Hapo yy alijua ni simu Iphone 6 S au kadi yako ya ATM umpe na password kabisa

Hawa viumbe hawafikirii kama wewe,wengi wao ni opportunist
 
Ye alifikiri labda ni Samsung Galaxy S6 Edge, yaani isiwe toleo jipya, bali toleo lijalo. Cherehani kutoana vigimbi.
 
Kaka umefikiria sana n unamapenz ya dhati. Nakushauri mpe muda ipo siku atakuelewa tu. Usikate tamaaa. Mimi ni degree holder na nimeajiriwa lkn sasa najifunza cherehan japo kuna watu wananidharau. Ila mi nawangalia tu
 
Daaaah! We ni kiboko! Kwa elimu aliyonayo cherehani haina mashiko!! Kama ungelikaa nae ukamuuliza ni zawadi gani alihitaji, au kwakuangalia plan zake na fikra zake ungetambua ni kipi kingemfaa!!
Kweli elimu yote ile akaitundike kabatini na aanze kushona nguo?!?

CHerehani si anaweza hata kuweka ndani awe anashonea watoto nguo??

Cherehani ina ubaya gani? Ila labda ulichokosea ni kutokujua interest za mpenzi wako, ila sioni kama hiyo zawadi ina ubaya wowote.
 
CHerehani si anaweza hata kuweka ndani awe anashonea watoto nguo??

Cherehani ina ubaya gani? Ila labda ulichokosea ni kutokujua interest za mpenzi wako, ila sioni kama hiyo zawadi ina ubaya wowote.

Hajui kushona sasa.
 
Yani kwenye ulimwengu wa teknohama mwendo wa mambo ya kisasa kabisa unawaza cherehani ya kuzungusha na mkono na kunyonga kwa miguu. Ungewaza zaidi ya hapo. Je yeye angekuletea zawadi ya "Tool box" na ngazi, na akaahidi kugharamia mafunzo yako kwa hivyo vifaa,ungejisikiaje?

hahahahahahahahahah,kumamake walai hii ni best ever! JF inanipa raha mpaka nataka kuruka ruka.
 
Humu great thinkers wachache,
nina vyerehani na dryers kadhaa.
Sijawahi kushona wala kujifunza lakini nina hesabu ya uhakika kila wiki.
Acheni ushamba mnnaosema cherehani haina mashiko.
 
Kwahiyo ukipewa zawadi ya gari wakati hujui kuendesha utalikataa??:biggrin:

Gari kila mtu anaendesha...sio interest...ni muhimu kujua kuendesha gari. Tatizo si aina ya zawadi. Angejua kwanza interest ya mchumba wake. Kujifunza kushona tena na cherehani mtu anatakiwa apende sio kujifunza tu kwasababu umepewa zawadi.

Lakini anaweza akampeleka kozi ya ushonaji (kama mchumba atakubali) ili zawadi isikae bure.
 
Duh!!! Hiyo zawadi ingenikuta mimi wallahi ungefurahi ningeipokea vizuri sana kisha ningekupa mipango yangu juu ya hiyo cherehani mpaka ungependa, hapo sasa sijui ungekimbia maana bajet ingecost si chini ya 20M .

Cc cute b
 
Last edited by a moderator:
Duh!!! Hiyo zawadi ingenikuta mimi wallahi ungefurahi ningeipokea vizuri sana kisha ningekupa mipango yangu juu ya hiyo cherehani mpaka ungependa, hapo sasa sijui ungekimbia maana bajet ingecost si chini ya 20M .

Cc cute b

We everlenk wala huna tabu. Jezi ya Man U tu unaridhika, au sio?
 
Last edited by a moderator:
Cherehani na MASISTA du wapi na wapi kaka?Hapo yy alijua ni simu Iphone 6 S au kadi yako ya ATM umpe na password kabisa

Hawa viumbe hawafikirii kama wewe,wengi wao ni opportunist

Opportunist hawako hivyo kila jambo kwao hulifanya liwe productivity.......huyo ni duu tu....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom