SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,129
- 7,895
Mabibi na Mabwana wa JF,
Naandika uzi huu hii ikiwa mara ya kwanza kabisa mimi kushare habari hii mahali popote. Sijawahi kumwambia mtu, hata familia yangu haijui kuhusu hili.
Nalileta kwenu kwa sababu nimenuia kabisa hili suala lazima nilitatue mwaka huu. Najaribu kuendelea kutambua watu ambao wanaweza kunisaidia kwa sababu nguvu inayonishikilia naona inaendelea kukaza kamba kweli kweli yaani siyo utani.
Kiufupi, kuna siku moja nikiwa kijana mdogo nilikuwa napanda basi wakati naelekea kukaa kwenye siti njiani nikapishana na mtu mmoja amevaa baibui jeusi amejifunika hadi usoni. Ilikuwa ni hapa hapa Dar es Salaam. Nakumbuka hadi kituo nilichokuwa nimepanda. Wakati napishana naye akaniwekea vidole machoni. Mimi nikapata kama bumbuazi fulani hivi yeye nadhani akashuka.
Kiufupi, maisha yangu hayajawa sawa toka wakati huo. Mimi ni mtu mwenye uwezo sana kiakili ila hata chuo niliishia katikati tena GPA yangu ikiwa ya juu. Wenzangu wamesogea sana na wengine wanaitwa waheshimiwa sasa hivi wakati mimi nimekuwa mtu ambaye hata nijaribu vipi niko pale pale. Na hata familia yangu kiujumla ukianzia kaka na dada zangu wana hali fulani ya kuhangaika tu wote. Tungeweza kufanya mambo makubwa binafsi na hata pamoja ila hakuna tunaloweza kuonyesha mpaka sasa.
Story yangu ni ndefu sana na nimepitia mengi mno nisingependa kuyaelezea hapa.
Kuna wakati tukio hili huwa linaondoka kwenye fikra zangu ila kuna wakati vitu fulani vinatokea mfululizo halafu nakumbuka siku ile.
Mimi ni mtu wa maombi, najaribu sana kuwa hivyo. Sijakata tamaa na sitakata tamaa, lakini najiulizaga nitasubiri mpaka lini?
Naomba ushauri tafadhali. Hali yangu lazima ibadilike sasa hivi.