#COVID19 Kuna siku Watanzania watapanga foleni za kilomita kadhaa ili kuchanja

sipotezi muda
Si ni kwa sababu corona imepewa kiki ila mbona hutumii muda humu kuzungumzia hayo magonjwa mengine hata malaria ambayo nayo inaondoa watu sana tu? Ndio maana nakwambia kama si corona kupewa kiki basi usingekuja kupiga kelele humu za kuhusu corona.
 
Korona inaweza usiuue kama Malaria na UKIMWI, lakini Ogopa sana airborne diseases. hizi ni tofauti na malaria na ukimwi. Plague ya miaka ya 1300(black death) na Spanish Influenza zote ni Airborne. Ziliuwa kwa kutisha. mwanzoni hii black death ilikuwa inaambukizwa kwa kung'atwa na viroboto wa 'panya' ambao walikuwa wanakudunga bakteria Yersinia Pestis. Sasa huyu mdudu akajigeuza, akaingia kwenye mapafu na kuweza kuambukizwa kwa njia ya hewa. hapo ndipo mamilioni ya watu wakaanza kufa. usifananishe aiborne diseases na vitu kama Malaria. huu ugonjwa unapotential ya kuua watu wengi kuliko UKIMWI na Malaria. au tuseme magonjwa yote yakiwekwa pamoja.
Unarudia tu vitu ambavyo tumeanza kuvisikia toka mwaka jana, tatizo sio ugonjwa wenyewe bali ni jinsi watu walivyoukuza huu ugonjwa na ndio tatizo lilipo. Wanaoumwa na kupona ni wengi kuliko wanaofariki ila ajabu muda wote vinaelezewa vifo tu, nakumbuka wakati huu ugonjwa bado upo China tulikataa hata wale wanafunzi wa kitanzania kule China kurudishwa kwa kuhofia kuleta ugonjwa ambao tuliona hatuuwezi hata kidogo.
 
Mbona hata huko hospitali tunafuata tu kila tunachoambiwa na daktari huku tukiamini yeye anajua kila kitu kwa sababu kasoma ni daktari, lakini uhalisia haupo hivyo. Hata hao waliyochanja si kwamba wote wamepata elimu ya chanjo ila wengi ni mkumbo tu, mtu kakaa kijiweni kaona wenzie wamechanja na yeye akaenda kuchanja wengine toka utu uzima hajachanja chanjo yeyote basi ushamba tu akaona nae kujaribu basi hawana elimu yeyote kuhusu huu ugonjwa wala hizo chanjo.
Hao madaktari unaowaamini wanasemaje kuhusu chanjo? Wengi wanaochanja wanajua kwanini wanachanja. Wengi wanaokataa chanjo hawajui kwanini wanakataa.
 
Unarudia tu vitu ambavyo tumeanza kuvisikia toka mwaka jana, tatizo sio ugonjwa wenyewe bali ni jinsi watu walivyoukuza huu ugonjwa na ndio tatizo lilipo. Wanaoumwa na kupona ni wengi kuliko wanaofariki ila ajabu muda wote vinaelezewa vifo tu, nakumbuka wakati huu ugonjwa bado upo China tulikataa hata wale wanafunzi wa kitanzania kule China kurudishwa kwa kuhofia kuleta ugonjwa ambao tuliona hatuuwezi hata kidogo.
Kama watu bado wanaujinga ni muhimu kurudiarudia. Huo ugonjwa unaua kama 3% hivi. Ila variants zinatofautiana. Inaweza kuja yenye mortality rate kubwa zaidi.

Kwani unafikiri Korona tumeiweza? Tumezamisha vichwa mchangani kama mbuni.
 
Hao madaktari unaowaamini wanasemaje kuhusu chanjo? Wengi wanaochanja wanajua kwanini wanachanja. Wengi wanaokataa chanjo hawajui kwanini wanakataa.
Madaktari kawaida yao huwa hawafikiri nje ya box hivyo ndivyo walivyofundishwa na kwao hivyo ndio huona ni usomi, ni madaktari wachache sana ambao hufikiri nje ya box.

Kwahiyo wapo madaktari ambao wanapinga si chanjo tu bali hata jinsi huu ugonjwa wenyewe jinsi unavyoshughulikiwa.
 
Si ni kwa sababu corona imepewa kiki ila mbona hutumii muda humu kuzungumzia hayo magonjwa mengine hata malaria ambayo nayo inaondoa watu sana tu? ndio maana nakwambia kama si corona kupewa kiki basi usingekuja kupiga kelele humu za kuhusu corona.
Hayo magonjwa yamezungumzwa sana, na yanazidi kuzungumzwa. Huu ugonjwa ni mpya na ni hatari sana. Lazima watu waelimishwe. Unataka mfano Ebola ikilipuka isizungumzwe sababu kuna Malaria?
 
Hayo magonjwa yamezungumzwa sana, na yanazidi kuzungumzwa. Huu ugonjwa ni mpya na ni hatari sana. Lazima watu waelimishwe. Unataka mfano Ebola ikilipuka isizungumzwe sababu kuna Malaria?
Hoja yangu ipo kwenye kuukuza huu ugonjwa kuliko uhalisia jinsi ugonjwa wenyewe ulivyo.
 
Madaktari kawaida yao huwa hawafikiri nje ya box hivyo ndivyo walivyofundishwa na kwao hivyo ndio huona ni usomi, ni madaktari wachache sana ambao hufikiri nje ya box.
Kwahiyo wapo madaktari ambao wanapinga si chanjo tu bali hata jinsi huu ugonjwa wenyewe jinsi unavyoshughulikiwa.
So unachagua madaktari wanaosema mtazamo kama wako. Yaani umeshaamua jambo, halafu ndipo unaanza kutafuta maoni ya wale wanaoendana na maamuzi yako!!!
 
Hoja yangu ipo kwenye kuukuza huu ugonjwa kuliko uhalisia jinsi ugonjwa wenyewe ulivyo.
Ugonjwa haujakuzwa. Unaua. Unadesrupt uchumi na shughuli zingine. Na unapotential ya kuwa kama tauni za kwenye biblia.
 
Kama watu bado wanaujinga ni muhimu kurudiarudia. Huo ugonjwa unaua kama 3% hivi. Ila variants zinatofautiana. Inaweza kuja yenye mortality rate kubwa zaidi.

Kwani unafikiri Korona tumeiweza? Tumezamisha vichwa mchangani kama mbuni.
Nakwambia hivi wanaokufa ni wachache kuliko wanaopona ila muda wote vinazungumziwa vifo tu,ndio maana ilifikia watu kutabiri kuwa huu ugonjwa ukija afrika tutaokota maiti barabarani na ni kweli kwa kipindi kile ilikuwa halali kusema vile.
 
Wewe umesema watu wanakufa sana, ndio nikakuuliza lini watu waliacha kufa sana?
Zitengenezwe dawa za aina zote, zijengwe kila aina ya hospitali KIFO KIPO PALEPALE
Kama kifo kipo palepale tuache kutengeneza dawa, kuchanjwa na kujenga hospitali.
 
Back
Top Bottom