Kuna nini tabora?

Mchili

JF-Expert Member
Aug 19, 2009
725
46
Hivi karibuni mh waziri Mkuu alikua na ziara mkoani Tabora ya zaidi ya wiki na katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja, Mh. Raisi nae yuko kwenye ziara ya kikazi mkoani humo Tabora. Swali najiuliza kulikoni viongozi wa kitaifa kutoka chama hicho hicho kutembelea mkoa mmoja kikazi kwa kipindi kifupi hivyo?

Kwani raisi asingeweza kumwagiza Pinda kufanya hayo anayoyafanya yeye sasa na kuokoa gharama, au ndio wameagizwa na RA wakamsafishe kiaina huko??
 
Tabora Ndiko kuliko na Siri ya madaraka ya JK Rostam Aziz wanaaenda kumfagilia Rostam Aziz.Nami nashindwa kuelewa kuna wakati nashindwa kuelewa hivi hawa viongozi wetu wanakitu kinaitwa ratiba au wanakurupuka kwa sababu hata hiyo ziara ya waziri mkuu Pinda inaonekana kama vile haikuandaliwa tizama hapa
http://haki-hakingowi.blogspot.com/2010/02/ziara-ya-waziri-mkuu-mkoani-tabora.html#comments nashindwa kuelewa
 
Magret Sitta naye ana masiku tele Tabora, jamani Maggie uwaziri sio kwa ajili ya wanaTabora. Hebu angalia ustawi wa jamii nyingine nchini Tanzania. Unaacha ofisi muda wote huo au umeihamishia Tabora?

Please Maggie, may be unataka kugombea ubunge, umechoka ubunge wa kuteuliwa au unamsaidia mzee kwenye underground campaign. Lakini ni vyema ukatekeleza majukumu yako ya msingi kwanza mamaaa.

Samahani kama nimekukwaza Maggie Sitta.
 
Inaonekana RA ametoa order kuwa jina likasafishwe na kuanzia mkuu wa nchi mpaka wasaidizi wake. Sijaona project ya maana waliyoenda kukagua kwa maendeleo ya wanaTabora zaidi ya kutoa ahadi za kisanii.
 
Nimeipata hii ya Pinda hata jukwaa hakuna, - dalili za kukurupuka bila maandalizi.


Kiti kikiteguka itakuaje hapo?
 
Inaonekana RA ametoa order kuwa jina likasafishwe na kuanzia mkuu wa nchi mpaka wasaidizi wake. Sijaona project ya maana waliyoenda kukagua kwa maendeleo ya wanaTabora zaidi ya kutoa ahadi za kisanii.

Hilo ni agizo la anayeogoza nchi behind the scene kwamba akasafishwe kwa wananchi ili asikose ubunge.Nchi hii kweli tunaviongozi hamnazo.
 
Kuna mambi mbili mbaya zenye sumu ya uadui huko, moja ya sitta na moja ya burushi na zinaharibu umoja wa wanaCC hivyo kutishia chama!!!
 
Masikini Wanyamwezi sisi. Tumefanywa Ng'ombe wa maziwa ya KURA.

Wilaya ya Sikonge kuna kata ya Kitunda, hakuna Rais ambaye alishawahi kufika huko. Kikwete akataka kuvunja miiko na akaenda. Gari ikakwama na ikabidi aende kwa helkopita na kurudishwa kwa helkopita hapa Sikonge. Kutoka hapo ndipo akapanda gari kurudi Tabora mjini.

Maisha bora wengine hata magari kwetu hayafiki. Ukiiona barabara utafikiri njia ya kupitishia ng'ombe. Ila sisi Wanyamwezi hata hatuna noma. Tumeshampa kura CCM kwani ni chama pekee na kiongozi pekee duniani wa ngazi za juu ambaye amefika kwetu kuja kutuona.


Road from Kitunda to Rungwa (Mbeya).

http://tzlivenews.com/blogs/blog/3954-kikwete-rais-wa-kwanza-kutia-mguu-kitunda.html
 
-Hii ni aibu tupu ati!

-Ila serikali haiko sensiteve katika matumizi yake,expenditure ziko juu kwa ajili ya mambo ambayo ni unproductive hivyo inflation inakua ngumu kurudi chini.Atakayeumia ni raia wa kawaida
 
Unauliza kuna nini?

King maker kachafuliwa, lazima aogeshwe kwa sabuni za kila aina ili atakate. Ikibidi hata kupanda juu ya mti, alimradi sauti ipae na wadanganyika waingie mkenge kama kawa!

Ee Mungu tunusuru!
 
Kura za Ushindi zipo tabora lazima waziweke sawa kabla mambo hayajaharibika zaidi , nafikiri Mwanza na Shinyanga kutakuwa na hati hati upinzani mzuri ukipatikana.Singida mteremko, Mara???, Kagera???, Kigoma??? S'wanga naona Mteremko.
Hata Barabara ya Nzega Tabora itaanza mwaka huu karibu ya uchaguzi magrade tutayaweka pale. CCM ni chama cha hadithi hadithi njoo , utamu kolea ...... na sungura mjanja tokea.
 
bana mkubwa, tabora kuna mambo mawili, cha kwanza ni uchawi wanaenda kutambika kwa kina fundikila huko, cha pili wanategemea kuiondoa tabora ngome ya lipumba, wanajua tabora watu wengi wanaipenda cuf.
 
bana mkubwa, tabora kuna mambo mawili, cha kwanza ni uchawi wanaenda kutambika kwa kina fundikila huko, cha pili wanategemea kuiondoa tabora ngome ya lipumba, wanajua tabora watu wengi wanaipenda cuf.

Wabunge wangapi wa CUF na wangapi wa CCM?
 
Si huyu mmiliki wa rais alishatangaza kuwa hagombei tena? Imekuweje?
 
na huko tabora wameambiwa utaundwa mkoa mwingine wa katavi ambao utakuwa ni urambo na mpanda nk
 
Viongozi wetu hawana agenda yoyote, wanachotaka ni kuonekana tu! Ukiuliza wote wawili walikuwa hasa wanaenda kufanya nini hutapata jibu la maana.
Ukweli ni kuwa itatuchukua muda mrefu sana kupiga hatua, kama namna yetu ya kufikiri itabaki hivi.
Huenda hawa ni reflection ya watanzania tufikirivyo!! Urais sio jina, ni vitendo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…