Katika siasa za Tanzania kuna accomodative politician and isolationist politician.
Mh. Zitto Kabwe anaendesha siasa zake kwa misingi ya accomadative politics kwa maana kuwa, siasa zake zina nafasi ya masikilizano na pia makubaliano na makundi mengine yaliyoko ndani na nje ya chama chake.
Tatizo lililopo hapa ni baadhi ya wanaCHADEMA wamejengwa kisiasa katika misingi ya isolationist politics kiasi cha kujenga fikra na mitazamo ya kihasama kati ya wao kwa wao au kati yao na vyama vingine vya kisiasa. Sababu kuu ni hii fikra ya kudhani wao ni bora kuliko wengine, na ili ufanikiwe lazima uwe mmoja wao. Huu ni aina fulani ya ubinafsi wa kisiasa ambao unasababisha kutumia njia zozote zile katika kufanikisha malengo yake.
Hili kundi ndani ya CHADEMA ambalo siasa zake ndizo zinazofanywa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, ukichunguza kwa undani utagundua kuwa ndilo ambalo linamuona Mh. Zitto kama siyo active kwenye siasa zao.
Mh. Mwigulu yeye siasa zake niza mlengo wa isolationism kama lilivyo kundi ndani ya CHADEMA linalomuona Mh. Zitto siyo active kwenye siasa zao.
Kwa kawaida, kundi lenye mlengo wa siasa za isolationist huwa halipikiki kwenye chungu kimoja na kundi jingine lenye mlengo kama huo. Ndiyo maana Mh. Mwigulu ni sumu kwenye hili kundi ndani ya CHADEMA lakini kwa vile Mh. Zitto ni accomodative politician, siyo ajabu kumuona kwenye maelewano na makundi mengine pamoja na kwamba isolationist wanakuwa hawana imani naye 100%.
Accomodative politicians wengine ninaowaona kwenye uongozi wa juu ndani ya CHADEMA ni kama Mh. Mbowe, Mh. Mnyika, Said Arfi...