Kuna nini kati ya Mwigulu na Zitto?

Kuna nini kati ya Mwigulu na Zitto?

teh teh teh mvujisha siri huyo, alafu ni bitozi flani hivi mwenye sauti tamu kama delila, wakati yeye mkulima tu! Tatizo lake ubitozi kajifunzi ukubwani.
 
Kama anamkubali sana mbona hakutumia wadhifa wake ndani ya MACCM kuwashawishi MACCM wenzake wampe kadi ya uanachama na hivyo kumkaribisha rasmi CCM? Au kumkubali kwake ni kuwa ndani ya CHADEMA ili kuendeleza usaliti kwa manufaa ya MACCM? Wanafiki utawajua tu huwa
 
Sisi vijana hatutakiwi kukaa kutukana au kuhukumiana nani yuko sahihi nani hayuko sahihi. Vijana tunatakiwa tushikamane na kulaani mienendo yoyote ya hivyo inayofanywa ama na vijana wenzetu au wazee wetu.
Vijana tunatakiwa kuamua hatima ya nchi yetu maana sisi ndio tutakaolipeleka gurudumu mbele ili lipokelewe na kizazi kijacho.
Ni upungufu wa akili kufikilia kwamba baba yangu ataishi miaka hamsini ijayo wakati sasa hivi anamiaka sabini. Huyu hawezi kuwa mmoja wawatu watakaoiona tanzania miaka 50 baadae. Vijana lazima tujifunze kuwatumia wazee wetu kutushauri. Haipaswi na wala siyo sahihi kuwasumbua na kuwahangaisha wazee wetu kwa kuwatuma waende ikulu kupambana na changamoto za karne ambayo si yao. Sisi vijana tunatakiwa tuingie pale mjengoni tupambane na changamoto zakileo na zadunia yaleo.
Sisi vijana vita hii niyetu. Tunatakiwa tuwe msitari wa mbele kuipigana. Nia aibu vitani kijana akijibanza nyuma ya mzee . Sisi tuwe mbele wazee watupe uzoefu wao.
Kama kweli tunahitaji mabadiliko ya nchi yetu basi nilazima tuondokane na umasikini wa kimawazo. Huu umasikini wa kimawazo ni sumu. Ni kansa. Inaua. Inaua kijana , mzee na watoto.
Vijana tuache uoga na tuende mbele tuaminiane sisi kwanza ili tuwe na umoja wakuipigana vita hii ya karne. Ni jambo la ajabu sana kijana mwenye nguvu kujificha nyuma ya kibabu kilicho kilichoshika mkuki eti kijana huyu akiamini kitamlinda. Yaani kijana msomi aliyetumia kodi za wananchi anataka kukaa mstari wa nyuma wakati wa mapambano eti kisa kuna kizee kakitanguliza mbele. Jamani haya nimatumizi mabaya ya wazee. Sisi vijana tuwe mbele, wazee wawe nyuma watushauri. Siyo kuwatanguliza.
Ni jambo la ajabu sana eti kijana anakosa kujiamni, anakosa kuamini vijana wenzake halafu yuko nyuma ya kikongwe. Hili binafsi siliamini.
Nyerere na wenzake tunaowakumbuka leo siku ya muungano, tunawakumbuka kwa matendo yao walipokuw vijana. Historia inatuambia walifanyA mengi enzi za ujana wao. Walipozeeka waliugua, walifariki. Sisi vijana wa leo tufanyeni kazi ya nchi tuache kujitoa akili. Nani asiyejua kwamba kazi inatakiwa ifanywe kwa umri fulani halafu mtu akizeeka astaafu? Umri wa kustaafu tumejiwekea wenyewe kisheria. Miaka sitini unastaafu kwa hiari na miaka sitini na tano ni lazima. Sasa huu ugonjwa unaotuingia akilini vijana wakushabikia watu waliostaafu waende Ikulu ni ugonjwa gani huu?? Uzoefu wa mzee yeyote tunauhitaji kwa ushauri. Siyo kwa kuwaweka wazee wetu mstari wa mbele. Hata hivyo kuna uzoefu mwingine ni wa hovyo sana wala hatuuhitaji. Hatuhitaji uzoefu uliouwa viwanda vyetu, hatuhitaji uzoefu uliotuletea EPA, hatuhitaji uzoefu ulioleta richmond, hatuhitaji uzoefu ulioleta Escrow, hatuhitaji uzoefu unaofanya mpaka leo watanzania hawana makazi, hawamiliki ardhi kisheria, hawana mikopo vyuoni wala hawawezi kuafodi milo mitatu kwa siku. Tunahitaji mwanzo mpya. Tuacheni kuwa watumwa vijana. Sisi wenye kero tuweni mstari wa mbele tupambane tujiletee maendeleo. Wazee wameshafanya yao. Ndo maana ukiwaomba Cv zinajaa magunia. Kama hatutaki unafiki na uzandiki basi sisi vijana tutafuteni kijana mwenzetu, anayeamini kAtika yale tunAyoyaamini, tumuweke ashike usukani pale magogoni, wazee wetu wabaki kutushauri.
 
Wewe umekuja vizuri walau umeielewa mada yangu kidogo, ni ukweli usiopingika kuwa zitto ni rafiki mkubwa wa jk na kuna kipindi nilikuwa sudan hawa watu niliwaona pamoja na mbunge mwingine wa chama kingine, wakiwa wameambatana na jk, na mwigulu nae ni kipenz cha jk na hicho cheo cha unaibu katiba mkuu alipewa na jk kupitia halimashauri kuu ya chama cha mapinduzi kule dodoma na yote ni baada ya mwigulu kuiponda hoja ya upinzani iliyowasilishwa na naibu katibu wa chama cha maendeleo na democrasia.

Kwa andiko lako hapo juu umenifanya nizame chimbo tena ili niunganishe dots, lakini all in all siri kubwa wanaijua wahusika

Kwani siasa ni uadui? yani kuwaletea watu maendeleo ni swala la uadui? walio ccm, CUF CDM wote ni watanzania bali wanatofautiana katika mitazamo ya jinsi gani ya kuwaletea watanzania maendeleo that all.
 
Kama anamkubali sana mbona hakutumia wadhifa wake ndani ya MACCM kuwashawishi MACCM wenzake wampe kadi ya uanachama na hivyo kumkaribisha rasmi CCM? Au kumkubali kwake ni kuwa ndani ya CHADEMA ili kuendeleza usaliti kwa manufaa ya MACCM? Wanafiki utawajua tu huwa

Mkuu wa Kaya mwenyewe alishindwa kumshawishi,pamoja na jitihada zake zote,ZZK hakukubali kwenda CCM,seuze hao watoto wa jana.
 
Mkuu nakusifu kwa uzi wako huu unaoonyesha unachambua mambo kwa makini. Kwa kifupi ni kwamba watu walio chini ya BOSS mmoja kwa nia moja huwa hawagombani hata kama wanatoka vyama tofauti. Mwigulu ni hazina ya mkuu wa kaya na Zitto ni rafiki mkubwa wa mkuu wa kaya, hapo unategemea nini?. Wawili hawa kuwa nyama tofauti mwingine kuwa upinzani na mwingine kuwa ccm hayo ni kupotezea tuu lkn hao wote lao ni moja.

unafaa kuwa FBI wewe maana utagundua mengi, upeo wako wa kutafakari ni mzuri.
Nakuwekea aliyoandika Waberoya 2010 kuthibitisha ulichoandika.
Mimi nimekuwa nikimfuatilia mheshimiwa Zitto, tangu alipoongoza mapinduzi ya kupindua serikali ya DARUSO mwaka 2002/2003 wakisaidiana na Ridhwan Kikwete na Omar Ilyas. Kipindi hicho nikiwa mmoja wa mawaziri wa serikali, ambayo ilipona kupinduliwa. Na tumekuwa wote ndani ya bunge la UDSM-USRCMimi personally nimekuwa muwazi sana na mkweli katika kila kitu kinacholigusa taifa hili na hasa uhuru wa mawazo na maoni ambao umedhihirika kuwa watanzania wengi sio kuwa hawana, bali huwa wepesi sana kuamini mambo na ni waoga kuonekana wanapingana na hali iliyopo.Mtazamo huu umenifanya nimpende Zitto na JF members wowote wale ambo huwa wanapenda kufikiria nje ya box, au another direction/angle. Zitto amekuwa akinifurahisha kwa kuleta changamoto za kuleta mawazo tofauti na kile ambacho wengi huwa wanafikiria.Zitto ni kweli anapenda sifa, kama binadamu mwingine yeyote yule, ila unapotaka sifa kwa kusimamia haki na ukweli na hasa unapopigania haki basi sifa hii ni sifa timilifu na inapendeza. Omar Ilyas naye alikuwa mmoja wao wa wanaopenda sifa ila kwa sasa naona amekua kidogo, nadhani Salim A Salim amemkuza.Si nia yangu niwaharibie hawa jamaa , ila ni hali yangu kueleza ninachowaza baada ya kuwafuatilia hawa watu tangu enzi hizo. Sijajua status ya Omar Ilyas kwenye issue nzima za udini, siwezi kumtuhumu, personally nimemuona ni mtu mzuri tu na anayependa wote pasi kujali udini ila bado ni rafiki wa Zitto!Tuendelee: Role model wa Zittoni Salim A. Salim, rais bora kwake yeye ni Kikwete, MD bora aliyewahi kumsema yeye ni Rashid Idrisa yule wa TANESCO.Tie, cord, umoja, Urafiki wa Zitto, Ridhwan, Omar Ilyas ni mkubwa sana kuliko maelezo, hili group lililotaka kuipindua serikali ya Kayombo-DARUSO, ili wao wapate madaraka si tu ni la hatari bali la kuangaliwa sana. Ridhwan amekuwa akijitetea sana yeye anataka ku-practise sheria hili hali kutaka uongozi amekuwa akitamani tangu siku nyingi sana.Ukiwa rafiki na Ridhwan umekuwa rafiki wa Kikwete!!! Huwezi kuwa adui wa JK ukawa rafiki wa Ridhwan, JK si tu anampenda Ridhwan kama motto, bali kama mwanaCCM mwenzie aliye tayari kulinda interest zao.Si ajabu Zitto kuwa alikuwa mmoja wa wanakamati ya bunge ya kuchunguza madini, maana JK anampenda Zitto, ambaye ni rafiki wa Ridhwan!Alichotamka Juzi ni mwendelezo wa kumuonyesha JK kuwa yuko ‘NAYE’ na yuko mbali na chadema na kuwa yeye hakuwa na mawazo kama wanachadema wengine!!!. Hakuishia hapo tu bali alisema JK amefanya mengi Kigoma! Hivyo hakuona sababu ya kutoka nje ya bunge, kwa hiyo hakwenda kabisa, Huu ujumbe haukuwa kwa wananchi, ulikuwa unaenda kwa JK rafiki yake! Hata kama JK kafanya mambo mengi huko jimboni kwake Kigoma ni wajibu wake kama rais na haikuwa zawadi.Kilichonifanya nijiulize je what makes Zitto na JK kuwa marafiki? Je Zitto na JK walikuwa wanajuana kabla ya JK kuwa rais? Definitely Yes!Je swali gumu na baya ambalo halina ushahidi ni je Zitto kuwa inclined kwa JK, Salim na kuwapenda baadhi ya viongozi wa kiislam je ni mdini?..........I mean chunguzeni hili. May be not! Kindly don’t conclude! What Salim teaches Zito?? Salim is CCM, is Salim and JK close friends? Cause Ommy and Zitto are close friends, Ooh! Ommy ni personal assistant wa Salim, Nauliza Kama Ridh, Zitto, Ommy ni marafiki then Salim and JK ni maadui? Find out please. However, we all know JK ni mdini, maana alianza harakati za udini tangu akiwa UDSM miaka hiyo….na hili fuatilieniNani anayejua Zitto ana mtambo wa kusaga kokoto na alipata tender ya barabara ku-supply kokoto? Is he defending his interest indirectly?Au ni kuwa ni great thinker ambaye anaishi kwa falsafa zake ambazo hatuzijui! Je mnafikiri Zitto kuwaambia waandishi wa habari yaliyojiri ndani ya chadema alikuwa hajui watu watamrudi? Who is greater to him? JK, wananchi wake Kigoma, mali au?I mean we should be careful na watu kama Zitto yes they are bright, mmh! But they might be dangerous for the opposition existence. But we should examine him carefully and not judge him. Nimegusia tu swala la uislam maana mpaka leo kuna baadhi ya waislamu wanaofikiri kuwa wanaiweza kuigawa nchi hii kidini, na kuna wakristo wanaofikiri wanaweza kuigawa nchi hii kidini.
 
Kuna uzi unamaswali nane kwa chadema,tumeshindwa kijibu,twendeni tukatetee chama ili tuaminike tunachokisema.
 
Sasa wewe huelewi nini? Utamchukia au kumshushua mtu anayeiba na kukuletea data? Mbona jibu ni simple sana
 
Wanamjua ni msalitiwa pamoja na kumsifia sana mwanasiasa mahiri, ana akili kuliko wote CHADEMA na ni maarufu kuliko CHADEMA walijua wakimkaribisha tu basi usaliti angeufanya ndani ya MACCM, hivyo kumsifia kote ni kutaki abaki ndani ya CHADEMA ili MACCM yaendelee kunufaika.

Mkuu wa Kaya mwenyewe alishindwa kumshawishi,pamoja na jitihada zake zote,ZZK hakukubali kwenda CCM,seuze hao watoto wa jana.
 
Back
Top Bottom