Kuna nini kati ya Mwigulu na Zitto?

Kuna nini kati ya Mwigulu na Zitto?

Katibu Mkuu wa magwanda Dr.W.Slaa aka babu, hampati Zitto kwa lolote, Zitto ni kijana, mwerevu, mchapa kazi, msomi, kwa juhudi zake pekee aliinyanyua chadema aka kadima na kuifikisha hapo ilipo.

Zitto hatujamuona wala! akifanya kazi za unaibu katibu mkuu wa chadema, sio saizi yake, huyo ni zaidi ya Katibu Mkuu na Mwenyekiti wa chadema kwa pamoja.

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
Na Mwigulu je?
 
Mwigulu humshambulia Dr Slaa kwa sababu ni mwiba kwa ccm,
Usitegemee hata siku moja usikie zito kasemwa ujue hana jipya.
Mti wenye matunda ndio upigwao mawe.
 
Mwigulu sio propagandist ila ni gaidi na mfadhili wa ugaidi. Propaganda haifanywi kwa kufanya ugaidi na kubambikia watu kesi za kigaidi.

Mwana mwema hutumia neno la kiungwana kuelezea jambo lisilo la kiungwana kwa waungwana na wasio waungwana ili asimkwaze asiye muungwana ...nimemwita propagandist purposely! Ila ningeweza kwenda mbali zaidi....
 
Nadhani Zitto na Mwigulu walishaenda kwa yule mganga aliyewalisha viapo PM7.
....Ulishawahi kuwasikia akina Juliana Shonza na Mwampamba wakimsema vibaya Zitto hata siku moja? labda kama wanataka ukoo wao wote ufe.
 
Zitto ni mwanasiasa mahiri anauwezo wa kujenga hoja yaani hutumia nguvu ya hoja lakini ni 'selfish',

Mwigulu si mwanasiasa mahiri hana uwezo wa kujenga hoja, hoja zake ni za kulazimisha (hoja za nguvu), binafsi huwa namwona ni 'opportunist'.

Zitto(selfish) na Mwigulu(opportunist) hawana malengo yanayofanana hawawezi kuwa na mahusiano ya kawaida, kama kutatokea lazima kuwe na 'bond' fulani (maslahi) yanayowalazimisha.
 
Zitto siyo threat kwa CCM. Full stop.
Zitto alisharubuniwa zamani na kina Mwigulu kuivuruga Chadema. Bahati mhaya alikuta viongozi wengi wa chsma chake wamekomaa. Hakuna aliyejisumbua naye.
Mnakumbuka kampeni za mwaka 2010, nani alimwona Zitto jukwaani akikampenia chama chake? CCM hawana shida naye sababu waishamuweka kwenye kiganja. Yeye ni kama Ryatonga Mrema. Tofauti ni kwamba mmoja ni mzee na mwingine kijana.
Dili ilikuwa hivi; hawa watu wa CCM walitaka kuigawa CDM kupitia Zitto na kampeni ya dini. Walitaka Zitto atoke na kundi la wafuasi hili general election ikifika, CCM ishinde bila usumbufu. Mchezo ulishtukiwa na kuanzia hapo Zitto akawa ignored na viongozi wengine wa CDM. Ndo maana huwa haonekani nao. Walimwacha ajiue kisiasa.
Ukiwaangalia Mwigulu na Zitto, ni vijana wadogo ila wangekuwa Mbwa, basi usingewatumia mawindoni. Hawachelewi kukung'ata wewe mwenyewe. Hapa nina maana kwamba siasa zao hazina future. Wamejiharibia vipaji vyao kwa kukubali kuwa ma ndumila kuwili. Mwigulu anakubali kutumika kwenye michezo michafu na kuacha finger print all over the place. Huyu anahope kwamba CCM itakuwepo kumlinda forever. Nakwambia utawala ukichange tu, Mwigulu atashtakiwa karibu kila Mkoa.
Bwana Zitto kwa wale wanaofatilia siasa, huyu haaminiki. Mara naacha siasa, mara nimo, mara naenda Somalia, Sudan kufundisha. Hivi Zitto anaweza kumfundisha nani? Hizi ni dalili za denial au natural death. Kidonda cha kuwageuka wanasiasa wenzake ndo kinauguzwa hapa.
Msikilizeni kwa makini, anawasema vibaya wabunge wenzake. Mfano juzi tu aliwambia watu kwamba hakwenda bungeni kupigana ngumi...akifanya reference kwa Sugu. Mimi sio mwana siasa ila naamini Zitto anapaswa kuwa mature sasa. Utoto umemzidia. Hata kama hawapendi wenzake, kuna mature approach anaweza kuzitumia.
Conclusion.
Zitto sio mwanasiasa. Ni ndumila kuwili na ni mtu anaweza kutumiwa na chama chochote kuharibu, huku akidhani anajiinua mwenyewe. Ana self interest zinazozidi interest za taifa. Ni mtoto na hajakomaa kisiasa.
Bwana Mwigulu, haijui CCM. Huyu atageukwa sio muda mrefu. Ila aombe sana taifa lisibadili utawala maana atashtakiwa!
Zitto na Mwigulu, waumini wao...yaani watu wanaowasikiliza, ni watu wajinga, watu wasiopenda kujishughulisha kujua mambo na low information people. Hawawezi kwenda kwa watu waelevu. Na hii ni dalili za mwisho wao.
Simjui zaidi Mwigulu, ila anayependa kumfatilia Zitto, soma mambo yake humu humu JF na facebook. Mpaka unamaliza, utaishia conclusion yangu.
 
Katibu Mkuu wa magwanda Dr.W.Slaa aka babu, hampati Zitto kwa lolote, Zitto ni kijana, mwerevu, mchapa kazi, msomi, kwa juhudi zake pekee aliinyanyua chadema aka kadima na kuifikisha hapo ilipo.

Zitto hatujamuona wala kumsikia akifanya kazi za unaibu katibu mkuu wa chadema, sio saizi yake, huyo ni zaidi ya Katibu Mkuu na Mwenyekiti wa chadema kwa pamoja.

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
Alafu inakuwaje ikiletwa hoja kama hii hapa jukwaani watetezi wanakuwa ni hawa ambao wanajulikana wazi kutoitakia meme cdm!? Haya ngoja tusikilizie 'jeshi la mtu mmoja' likiendelea na kujenga chama huko Rukwa na Tabora.

 
Zitto ni kipenzi cha wapenda maendeleo, ulivu, amani na umoja wa kitaifa. Watu wa namna hiyo ndani ya CCM ni wengi, ndio maana wanampenda Zitto. CCM haichukii upinzani au wapinzani, CCM inachukia siasa za kugawanya taifa kwa misingi ya kibaguzi na ulaghai...
Naomba nikukumbushe kidogo. Mwigulu alishasema anao maadui wawili wakubwa hapa duniani(kumbuka huyu ni kiongozi mkubwa CCM) ambao ni Shetani na Dr Slaa. Sasa wewe ni CCM gani unaizungumzia?
 
Babu hana zaidi ya porojo.

Watanzania tunazihitaji porojo za babu kwa sababu zinawaamsha watawala na kuwafanya wachape kazi. Porojo zake ndio zilizoibua EPA, porojo zake ndio zilizopelekea kuimarishwa kwa PCCB na mambo mengine mengi. Kweli porojo za babu zinahitajika katika nchi hii.
 
Babu ndio katibu mkuu lazima tumpe hadhi yake, ingawa majukumu yamemshinda. Unanini weyee?

Nina babu pia ila sijawahi kumuongelea vibaya wala kuhumhoji walikutana wapi na bibi......
 
Binafsi sisumbuki na hoja ya Masanjab kuhusu 'uhusiano' wa Mwigulu na Zitto.

Lakini nina mashaka makubwa pale ambapo ZeMarcopollo, Mingoi, Songoro, FF, Ritz, Thahta, Mlengo wa kati, na M23 'wanapomkubali' Zitto na kumponda Dr Slaa.

Hapo lzm wana agenda rasmi. Zitto mdogo wangu, ukikubali sifa za hawa niliowataja itabidi ujichunge sana, sio kweli kuwa wanapenda mafanikio yako kisiasa.
 
Siku zote zitto huwananga viongozi wa serikali na sio wa vyama! Anapomnanga mtu huwa analenga direct utendaji wake na athari yake moja kwa moja kwa wananchi! Ukinangana na mwigulu wote mnakuwa hamna malengo zaidi mtadhalilishana tu. Zitto yuko makini

umemaliza mkuu..Salute!
 
Mi nadhani wanaogopana, maana kila mmoja anajiona ana akili kuliko mwingine. (mchumi namba moja) nadhani hapo ndio tatizo lilipo.
 
Zitto hanaga siasa za kuambiwa bali mtu wa fact. Zitto hafanyi kazi ya unaibu wake kama kiongozi wa CHADEMA(KADIMA) ila anaifanya mh Mnyika unataraji atakutana wapi na Mwigulu?
 
Lakini pia mleta mada ungejiuliza zaidi kwanini mh zitto kabwe anapendwa na watanzania wengi wakiwemo wabunge wa ccm na vyama vyengine na sio Mwigulu peke yake. Zitto ana ajenda za kitaifa na sio za kichama.
 
wote TISS member hao, wanatekeleza majukumu yao ndo maana wanakwepana kukutana pamoja wakashtukiwa. lengo lao ni moja amini msiamini na sitaki nione mtu anataka nitoe maelezo ya ziada.
 
Back
Top Bottom