Kuna namna ya kumuombea dua marehemu Eid hii ya Kuchinja?

Wingawinga

JF-Expert Member
Oct 31, 2021
622
1,523
Wandugu nilikuwa nauliza, kuhusu mpendwa wangu ambaye ni marehemu, je, nitaweza mrehemu vipi kupitia hii Eid ya kuchinja? Yeye ni Musilamu na mimi sielewi chochote kuhusu hilo suala, hivyo ninaomba muongozo, kuna mnamna ya kusoma dua kwa kipindi hiki cha Eid ya kuchinja? Je, umuhimu wake ni upi kufanya sasa hivi badala ya baadae?

Niliwahi kukaa na mtu mmoja akaniambia marehemu wengi siku ya Alhamisi kwenda Ijumaa hutoka makaburini na kwenda majumbani walipoishi na kuanza angalia mazingira na wengine hulia. Je, hiyo habari ina ukweli gani na Eid hii ni Alhamisi, je, naweza kufanya jambo gani kuweza contact marehemu na kuongea naye au tu kumpa messege kwamba ninampenda sana na nitaendelea kumpenda daima?

Je, kama mpendwa wangu kachukuliwa msukule, nikimfanyia dua ina maana ndio nimeshakubaliana na kwamba aende moja kwa moja? Sijamfanyia dua proper mpaka leo na amefariki miezi michache iliyopita, sababu nina wasiwasi nikimfanyia dua ina maana nimekubali kwamba kafa wakatii bado naamini hajafariki ila kachukuliwa.

Naombani muongozo wenu, asanteni.
 
Back
Top Bottom