Mikakati hii ya kimafia ikifanyika Simba SC itakuwa Bingwa, wasiwasi wangu uko kwa Uongozi wenye kusalitiana

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,694
109,128
Kikiundwa tu Kikosi Kazi cha Umafia (Michezo Michafu) ya Soka la Tanzania (Bongo) kisha Kikaaminiwa, kukawa na Usiri nina uhakika Simba SC ikizicheza Mechi Nne tu za Yanga SC ile ya Mtibwa Sugar FC, ya KMC FC, ya Namungo FC, ya Mbeya City na yetu ya Sisi na Wao huku Simba SC tukikubaliana kuanzia sasa tushinde Mechi zetu zote kwa 99% Simba SC itakuwa Bingwa.

Wasiwasi wangu mkubwa ni huu;

Management ya sasa ya Simba SC imekosa kabisa Unity kama iliyo Kauli Mbiu ya Simba SC isemeyo Nguvu Moja.

Ndani ya Administration ya sasa ya Simba SC kuna Usaliti na Unafiki mwingi hali ambayo ni Kikwazo kwa Kupambana na Yanga SC na tuwe Mabingwa.

90% ya Viongozi wa Simba SC sasa na hata baadhi ya Watendaji wa Simba SC na kule katika Timu Benchi la Ufundi kuna Watu ambao kwa Tamaa zao za Pesa ni wepesi sana Kununulika na Kutumika mno na Maadui (Mahasimu) Wetu.

Kingine hata kama kutakuwa (kutaundwa) Kikosi Kazi hiki cha Umafia (Michezo Michafu) ili Yanga SC angalau ipate Sare Mechi Nne na ifungwe na Simba SC je, kwa sasa Simba SC yetu ina Kikosi cha Kukuhakikishia Ushindi kwa 100% kwa Mechi zake zilizobakia za NBC Premier League?

Kwanini mara kwa mara GENTAMYCINE Mimi ambaye ni mwana Simba SC Kindakindaki nawapa Yanga SC 60% hadi 75% za kuwa Mabingwa tena?

Jibu langu ni jepesi sana kwamba Yanga SC ya sasa inaongozwa na Watu si tu Werevu bali pia ni Mangwena (Mafundi) wa Umafia wa Soka na Janja Janja ya Soka la Bongo na pia wana Timu Kabambe ya kuwapa Matokeo chanya ya Uwanjani kwa angalau 85% hafi 95% kwa Mechi zao.

GENTAMYCINE naandika haya kwa Masikitiko na Uchungu mkubwa tu kwani zaidi ya mara hapa hapa JamiiForums niliandika Kuwaasa Simba SC yangu jjuu ya hili ila hakuna ninaloona likifanyika na Mahasimu Wetu Yanga SC wanaendelea tu Kutuacha.

Simba SC ya sasa ingepata Warithi wa Umafia kama Marehemu Priva Mtema, Marehemu Mzee Bamchawi na Marehemu Hanspoppe hawa Yanga SC kila Siku wangekuwa Wanalia.

Na naumia zaidi kuona Mafia wachache waliobaki na ninaowaani kama Poti wangu Magori, Mtani wangu wa Kiha Kaduguda na Bingwa wa Kujitoa Mhanga Kassim Dewji (KD) hawatumiki ipasavyo kwa Kusaidiwa na Watu Wengine (nikiwemo GENTAMYCINE Mwenyewe) tusiopenda Kujulikana ili Simba SC yetu itusue.

Uongozi wa Simba SC na wana Simba SC Wenzangu kushindana na Yanga SC na Kumshusha alipo (ilipo) inataka Kazi ya Ziada na hata ikibidi baadhi kupata Matatizo au Hatari kwa Maslahi ya Timu yetu Kitu ambacho kwa Wana Simba SC wa sasa nawaona ni Waoga, Mabishoo na hawajali.

Marehemu Mzee Juma Mnonji alikubali Mkono wake wa Kulia upate Shida maishani mwake ili Simba SC imfunge Mzambia mbele ya Rais Hayati Kenneth Kaunda je, tunao Watu wa aina hii kwa Simba SC yetu ya sasa/leo?

Nikisema Yanga SC ni Mabingwa tena kwa Msimu huu msininunie GENTAMYCINE kwani namaanisha, najua kilichopo na nina PhD ya Soka la Tanzania na Michezo yote Michafu.
 
Mambo yote Yangewezekana kama Yanga wangekua wanapitisha bakuli, kwasasa Simba ata watumie fedha zote za ukoo wa MO Dewji hawana uwezo wa kuipiku Yanga katika Ubingwa.
Yanga uwa inahitaji nguvu kidogo tu ya kiuchumi kutwaa ubingwa, Yanga ilisha wekezwa kwenye network ya Nchi nzima.
Ndio maana ata wakati wanapitisha bakuli hawakuwai kushika nafasi ya tatu.
 
Timu inayocheza kibingwa huwa haisumbuki sana na kupata matokeo chanya uwanjani... Ukiwatazama vizuri watani utaona hakika wanapambania tena kuchukua ubingwa msimu huu, mfano mechi yao na Kagera sugar walizidiwa kila eneo uwanjani lakini wakapata matokeo mazuri, mechi na Prison wakavuna points 3 muhimu na hata mechi ya juzi na Azam wakafanikiwa, hizo kwangu me zilikua ngumu sana kwa Yanga kutoboa lakini kusema kweli jamaa wanapambana sana hawana blah blah. Tukiweka ushabiki pembeni timu yetu ya Simba kuna mahali wanapoteza umakini wao wa kupambana!
 
Zwazwa kama zwazwa!funga bakuli lako, SIMBA,SIMBA HAMIA HUKO UNAPOONA WAKO SAWA SIO KILA UKISHAPIGA WANZUKI unakuja kupiga kelele SIMBA,SIMBA
Umemaliza Kunitukana au bado labda?
 
Walushakuwepohao unaosema wangekuwepo sasa Yanga ingekua inalia saivi na bado Yanga ilikua inashinda na inachukua ubingwa. Tengeneza kikosi imara ambacho kitakuhakikishia ushindi kwa walau 90% halafu achana na ulozi cheza mpira uwanjani.

Utashangaa tu mwenyewe unaanza kukaribia level za Yanga
 
Back
Top Bottom