Kuna mtu anaiua CCM kwa speed ya rocket

Kuna mtu anaiua CCM kwa speed ya rocket

Kama anadhani atafanikiwa kwa style hii,bwana huyu nampa pole sana na ajue tu yote haya yanayoendelea kwa sasa ni "kete turufu" kwa upinzani na ni cancer inayoua taratibu chama chake.

Kiukweli kadri siku zinavyokwenda ndivyo wengi wanagundua hafai na wengi wanaacha kumuunga mkono na mwisho wa siku atabaki na supprt ya kikundi kidogo sana cha watu wanaomuunga mkono na hawa watakuwa ni wale wanaonufaika na uwepo wake na hata hao sio wote watakaokuwa wanafurahishwa na matendo yake bali ni katika kulinda tu vibarua vyao.

Yuko gizani na haoni kilicho mbele yake mpaka pale yatakapotimia kwakuwa hivi ndivyo ilivyopangwa kwamba kupitia yeye Taifa litakombolewe.

Usiniulize imeandikwa katika kitabu gani na ni katika mstari gani bali subiri kuona haya yakitimia.

Mungu ana makusudi na watu wake na ana njia nyingi anazotumia kufanikisha mipango yake kwa faida ya watu wake na njia nyingine huwa ni chungu zeenye taabu na mateso mengi kama tunavyoshuhudia sasa katika nyakati hizi za mpito.

Time will tell.
usione ile timu ya chama imekaa kimya. huyu bwana anaweza kuwa raisi wa kwanza toka ccm kuongoza kwa miaka mitano tu. watu wamechoka nae ujuaji mwingi mno. yeye kajifanya mchumi mkuu wa serikali matokeo yake ndo hayo. ninaona njia mbadala za kuua rushwa, kuua ufisadi, kurudisha nidhamu nk bila ya kuathiri maisha ya kwa kiwango kilichopo sasa. sasahivi kila mtu analia. kulikoni? ninapata mashaka sana kuona watanzania wote wanalalamika hapo najua kweli hali sio nzuri. kama unarekebisha uchumi katika style ambayo sekta binafsi nayo inafifia badala ya kushamiri basi ujue haurekebishi uchumi bali unauua. huwa nashangaa anaposema viwanda wakati anaua mazingira vutivu ya viwanda. nani avutiwe kuwekeza wakati uwezo wa kununua wa wananchi hauvutii kuwekeza? kodi za ajabuajabu? bajeti iliyopangwa mwaka jana nasikia hadi sasa utekelezaji ni kichekesho ikiwa imebaki miezi mitatu tu ipangwe bajeti nyingine. tabu inaanzia kwenye ujuaji tu. gavana wewe, igp wewe, mwanasheria mkuu wa serikali wewe, everything you hapo mambo hayawezi kwenda.
 
Sasa kama anaiua ccm wewe kinakuuma nini?si ufurahie kwa kukaa kimya ungoje ccm ife?unavyopiga kelele unastua tufanye mabadiliko ili ufaidike na kuondoka kwake au ufaidike na ccm kuimarika?
Tuacheni na ccm yetu,tumedhamiria kufanya mabadiliko ya kweli,tutapimwa 2020
Sasa hivi think tank ya serikali ya CCM ni Bashite.
 
Watajipanga saa ngapi kuchukua nchi badala ya kujenga chama wanashinda mahakamani kwa makesi lukuki ya kujitakia?,watakuja shutka kumekucha waanze kulia wameibiwa kura
Leo mmeambulia nini zaidi ya aibu na fedheha huko Mahakamani?
 
Kiukweli Magufuli anaua chama. Ila mwacheni akiue kwa manufaa ya wengi
Ila Mungu atuhurumie jamani. CHADEMA imeshajifia imebaki kuokota wauza madawa ya kulevya na MAFISADI, sasa na CCM nayo ife?
 
Ila Mungu atuhurumie jamani. CHADEMA imeshajifia imebaki kuokota wauza madawa ya kulevya na MAFISADI, sasa na CCM nayo ife?
Na ife kabisa. Ccm imebaki jina tu. Ndo maana mkulu anahaha udhibiti wapinzani. Jingazi
 
Halafu 2020 Magufuli atawagaragaza kwa kipigo cha mbwa mwizi mje tena hapa kulia lia kuwa mmeibiwa kura sisi hatuangalii sura hata agombee nani sisi ushindi tumezaliwa kushinda na si kushindwa iwe jua ama mvua ushindi lazima
msipeleke tu askari wenu wakawafukuza raia na kuwapiga ili muingize kura za ziada, si tunawajua mnavyodakwa na masanduku ya kura zilizopigwa tayari, nyie wenyewe kwenye kura za maoni mnapigana sembuse kupiga raia na wapinzani
 
Huyu jamaa hata akiua ccm, bado sioni upinzani wa kuichukua nchi. Hatuna wapinzani imara, wanaoweza kusimama na kuiongoza nchi, labda DJ na genge lake waondoke.

CCM ilitakiwa iondoke mda mrefu, angalau 2010 au 2015 tulitakiwa tumeshaizika kama KANU huko Kenya, lakini kwa upinzani upi? Upinzani na wapinzani wengi ni puppets wa CCM, wachumia tumbo na wafanyabiashara, refer ujio wa EL na mlungula aliotengeneza DJ.
 
Huwa nikizisikiliza napatwa na hasira kupita kiasi,halafu ndiyo huyu aliyesema naomba mnikosoe nitakapoteleza leo hataki hata kuguswa.CCM wametuletea balaa kubwa hawa majamaa

...inabidi uwaombe ndugu zako waweke sumu ya mende mbali na wewe[emoji12]
 
Speed yake in nzr ila anaharaka ktk majibu na namna anavyotenda kaz hasa ktk kushughulikia mahitaji yawatu mahala pakaz
 
Hebu muombeeni dua Mzee Mugabe kuna habari kwamba kapelekwa huko Far east kwa matibabu.
 
Huyu jamaa hata akiua ccm, bado sioni upinzani wa kuichukua nchi. Hatuna wapinzani imara, wanaoweza kusimama na kuiongoza nchi, labda DJ na genge lake waondoke.

CCM ilitakiwa iondoke mda mrefu, angalau 2010 au 2015 tulitakiwa tumeshaizika kama KANU huko Kenya, lakini kwa upinzani upi? Upinzani na wapinzani wengi ni puppets wa CCM, wachumia tumbo na wafanyabiashara, refer ujio wa EL na mlungula aliotengeneza DJ.
Wewe ni mnafiki tu!
 
Wapinzani sasa nimeanza kuwaelewa taratiibu, mkijipanga vzr 2020 mkaweka hoja vzr nitawaelewa vzr zaid. Kuna turufu nyingi za kujengea hoja na nikawaelewa sana
 
Back
Top Bottom