Ni hivi,
Ijumaa baada ya kufunga duka nlkua nna ratiba ya kwenda kwake, ghafla nikapewa taarifa MKE wangu kakimbizwa ghafla hospitali, analalamika Tumbo linaamuuma sana.
Kanipigia kuniuliza "vipi mbona ufiki"
Nikamtaarifu sitoweza kuja kwako, niko njiani naelekea hospitali, mke wangu kakimbizwa ghafla. Nashangaa ananitumia sms za kipumbavu, nikaona asije niharibia Siku, nikapata ajali barabarani, sikuzijibu sms zake.
Baadae kanipigia Akisema "Sasa Ni pesa ya matumizi vipi, hamna chochote cha kupika uku? "
Nikamwambia "nenda Duka la mangi Apo jirani, akakupe vitu unavyohitaji vya kupika, nkija ntamlipa pesa yake". Baadae kanirudishia mrejesho kua kamkuta mkewe, kasema hakopeshi.
Nikamwambia, Basi tumia balance yako, nunulia vitu vyote vya kupika, utanipa hesabu Kisha ntaifidia nikija uko kwako. Kasema sawa.
Tangu juzi sijakwenda kwake wala kumpigia Simu, nmetuliza akili namuuguza wife kwanza.
Leo ananiuliza hivi namchukuliaje,
Hata Salam kuulizia tu mgojwa niliemtaarifu anaumwa kapelekwa hospitali ghafla anaendeleaje, hamna.
Anachoulizia direct Ni pesa zake za matumizi nilizoahidi ntafidia baada ya kuzitumia kugharamia chakula chake mwenyewe.
HUYU MWANAMKE HANA UTU, UBINADAMU WALA USTAARABU KABISA[emoji34]