A
Anonymous
Guest
Nimeamua kuandika hapa kwa kuwa JamiiForums inafuatiliwa na watu wengi ndani na je ya Nchi, mtandao huu unafuatiliwa na watu wa kawaida, Viongozi na Watu wengine mashuhuri. Ningependa kuwaomba kwa unyenyekevu mkubwa kabisa andiko langu hili liende hewani.
Ikiwezekana andiko hili lifikisheni kwenye mitandao yenu ya Kijamii linalohusu malalamiko kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi hususani kwa Jeshi la Polisi.
Ipo hivi, mdogo wangu (naomba nisimtaje jina) ni Mtumishi wa Jeshi la Polisi ambaye amekuwa akiomba kusoma Shahada ya Sheria kwa miaka mitatu mfululizo akiwa ametimiza vigezo vyote ikiwa ni pamoja na Admission Letter ya chuo husika.
Viongozi wa Wilaya yake na Mkoa anaofanyia kazi wanampitishia maombi yake kuwa aruhusiwe kusoma lakini changamoto inakuja kwa watumishi wa Makao Makuu ya Polisi Dodoma Masjala ya Operation na Mafunzo.
Kitengo hicho kimsingizi ndiyo kinachohusika kupokea Maombi ya Askari wanaoomba kusoma Kozi mbalimbali, hupokelewa kisha kupelekwa kwa Kamishina wa Operation na Mafunzo kabla ya Kupelekwa kwa IGP ili kuidhinishwa.
Askari wa Masjala hiyo huwa wanahitaji kupewa kiasi kikubwa cha pesa angalau kuanzia Tsh. 300,000/= kwanza ndipo maombi yapelekwe kwa Viongozi wanaotakiwa kuyapitisha, kama mhusika hatatoa chochote kitu basi maombi hayo hutupwa au hata kuchomwa moto ilhali wengine wanaotuma pesa hizo huwa wanapata ruhusa za Masomo.
Hali hii inawavunja moyo Watumishi wa Jeshi hili na inapunguza Uaminifu kwa kuwa wanaombana Rushwa wao kwa wao lakini pia wanatenda kinyume na Sheria ukizingatia wanafanya kazi kwa Viapo vya Uaminifu na Utii.
Natanguliza shukrani zangu za dhati kwani naamini hii itawasaidia wengi ambao wameomba ruhusa za Masomo kwa Mwaka huu wa Masomo 2023/2024.