DOKEZO Polisi, WMA wanatunyanyasa Wakulima wa Kiteto na kuna mazingira ya Rushwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Sisi baadhi ya Wakulima wa Vijiji vya Mwitikira, Ndaleta, Katikati na Ngabolo Wilayani Kiteto Mkoani Manyara tunapenda kujibu na kutoa ufafanuzi juu ya kinachoendelea kuhusu wenzetu kadhaa kukamatwa kwa madai mbalimbali kikubwa ikiwa ni suala la mgogoro wa ardhi.

Ujumbe huu ufike kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, TAKUKURU, Usalama wa Taifa na viongozi wa juu wa Serikali hasa Rais Samia Suluhu Hassan.

Bila kuingilia kinachoendelea Mahakamani lakini ni vema Watanzania na Dunia ijue kilichotokea na kinachoendelea nyuma ya pazia.

RPC wa Manyara, George Katabazi katika maelezo yake kuhusu kuwakamata Wakulima wenzetu katika suala hilo, amesema sababu za kuwakamata Wakulima wenzetu ni kuwa eti walikataa kuondoka eneo la Hifadhi baada ya kutakiwa kufanya hivyo na Askari wa WMA, jambo hilo si kweli kabisa.

Ieleweke kuwa eneo hilo la mashamba ambalo sisi tulirejea kwa ajili ya shughuli zetu za kilimo, limekuwa na mgogoro kwa muda mrefu.

Awali, mamlaka zilituondoa Wakulima kwa madai kuwa ni hifadhi wakati huohuo wenzetu Wafugaji wakawa wanaendelea kutumia kulisha mifugo yao kama kawaida.

Shauri hilo lilifikishwa Mahakama ya Mwanzo Kibaya, ikawa Kesi Namba 182 ya Mwaka 2019, Mahakama hiyo ikasema suala hilo ni kesi ya mgogoro wa ardhi na si jinai, hivyo ikatakiwa ipelekwe Baraza la Ardhi.

WMA wakatakiwa kwenda Baraza la Ardhi lakini hawakufanya hivyo.

Tuliporejea shambani tukakamatwa tena na kufunguliwa Kesi Namba 202 Mwaka 2019, wakatubambikia kesi kuwa Wakulima tumeua Wanyama.

Wakatuchukua kati yetu, watatu wakapelekwa Manyara, cha kushangaza mmoja akapelekwa Arusha wakati Wilaya ya Kiteto ambapo ndipo ulipokamatiwa na kufunguliwa kesi ipo Manyara.

Tukapambana na kupiga kelele mwenzetu akarejeshwa Manyara na walioenda kushtaki hawakufika Mahakamani, baada ya muda kesi ikafutwa.

Tuna wasiwasi kuna mazingira ya rushwa katika hili linaloendelea sasa, kwani kabla ya Wakulima wenzetu kukamatwa kuna mfugaji mmoja alitoa kauli tata akiwa kwenye Kijiji cha Olboloti, Wilaya ya Temba.

Alisema, namnukuu “Hao wanaojifanya wameenda shambani kwa oda ya Baraza la Ardhi watakutwa na kesi ya nyara za Serikali”. Kweli siku chache baadaye hilo likatokea.

Mkuu wa Mkoa aliyepita aliandika barua ya Mwaka 2020 inayomuelekeza DC wa Kiteto kuwa Ofisi yake inatakiwa itupe maeneo mbadala na kama hilo haliwezekani basi turejeshwe kwenye maeneo yetu ya awali.

Barua ipo na ni ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, sasa huyu Mkuu wa Mkoa wa sasa mbona anatoa kauli tofauti? Inamaana hana rekodi za watangulizi wake kuhusu kile walichokiamua?
1cc666a0-6578-4980-ad21-787e90b019e5.jpg

Barua kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ikimuelekeza Mkuu wa Wilaya kutupatia Wakulima maeneo mbadala kama wanataka kutuondoa kwenye ardhi yetu, lakini viongozi hawakuifanyia kazi na wanaipuuza.

Sisi Wakulima tunanyanyasika kwa kuwa hatuna hela? Anadai hadi kufikia Januari 15, 2024 kutakuwa na muafaka wa mgogoro, lakini haweki wazi anatatua vipi wakati kila kitu kipo kwenye maandishi na kwa nini haizungumzii barua ya mtangulizi wake kuhusu uamuzi alioufanya?

Serikali ya Mkoa haitulindi Wakulima kabisa, wanatufanya tuamine kuwa kuna maslahi binafsi ya Wafugaji na WMA.

Kuhusu wenzetu walioshikiliwa na kuwekwa ndani kwa sasa walikuwa wapewe dhamana Ijuma ailiyopita Novemba 24, 2023, lakini Mahakama ikasema inahitaji wadhamini wawe wawili, ikashindikana.

Leo Novemba 27, 2023 baada ya sisi kurejea tukiwa na uthibitisho wote, bado imeshindikana wanadai hadi Novemba 30, 2023 licha ya kuwa masharti yote yamekamilika.

Kingine ni kuwa kuna makarani ambao wametengeneza mazingira ya kutaka kupozwa ili nao washughulikie suala hilo.

Baadhi ya ndugu ambao wapo ndani hasa Wanawake pasipo sisi kujua walichanga jumla ya Sh 200,000 na kukabidhi kwa baadhi ya watu wa usalama wakiamini watawasaidia, sasa hivi wanatupigia simu wanalia wanasema wametoa hela na hakuna kilichofanyika.
 
Back
Top Bottom