Kuna watu hawaelewi hata utaratibu wa uraia pacha.
Ukwelei ni kwamba nchi haiwezi kukupatia uraia wa nchi yao kienyeji tu.
Kwanza wanataka wajue uraia wa nchi yako wakati unaomba uraia wa nchi yao.
Watafuqtiliq kama uraia wa nchi yako unaruhusu uraia pacha au hauruhusu .
Kama unaruhusu wanakupa uraia wa nchi yao na pia nchi yako ya zamani inataarifiwa kwamba umepatiwa uraia wa nchi flani hakuna siri.
Kama nchi yako hairuhusu uraia pacha kabla ya kupewa uraia wa nchi nyingine inabidi ule kiapo cha kuukana uraia wa nchi yako pia kukabidhi passport ya nchi yako ambayo itarudishwa wizara ya mambo ya nje hapo ndipo unakabidhiwa passport ya nchi yako mpya tena baada ya kufundishwa mila tamaduni za nchi hiyo.
Kwa utaratibu huo kwa hiyo kamwe haiwezekani kwa raia kutoka nchi isiyoruhusu uraia pacha akawa na uraia wa nchi nyingine kiujanja ujanja hao mnaowasema kama akina rostam azizi kitu ambacho wanacho ni residence permit.
Watu wanaweza kuwa na residence permit hati ya makazi ya zaidi ya nchi moja.
Mfano unakuta mimi ni mtanzania nina passport ya Tanzania so naweza kuishi tanzania kama raia, lakini pia nina residence permit ya Canada, halafu pia nina residence permit ya USA ambapo naweza kuishi huko kama mkazi ila sio raia wa hizo nchi