Kuna mambo mawili Rais kapotoshwa

Kuna mambo mawili Rais kapotoshwa

Hivi kanuni ya uchumi inasemaje kuhusu kodi? Hapa tunaongelea walipe ama wasilipe kodi?
Bado najiuliza
 
Respect Bro,
Mimi naomba niongezeee kidogo kwenye sentensi hii.........Kanuni za uchumi zinaeleza kuwa biashara nzuri ni ile yenye faida ndogo lakini ina wateja wengi na ambayo iko kwa muda mrefu.....
Kuna vitu vingi sana ambayo uchangia kujenga muono na mtazamo wa mtu, kwa mfano elimu, malezi, exposure, watu wanaokuzunguka(ndg, jamaa na marafiki), imani ulikuziwa, na mfumo mzima wa masha uliopitia wakati wa ukuaji wako. Kama vyote hivyo nilivyovitaja hapo juu vikiwa na muelekeo chanya(positive) alafu na Mungu pia akikuongezea na Busara na Hekima utakuwa umepata faida kubwa. Kwani wanaokushauri hawatapata shida kubwa kukushauri yaliyo mema.
Ni hayo tu.
Labda tukuchague ukamueleweshe. Kazi ipo.
 
Biashara ya utalii ni biashara ya huduma,hii si kauli ya kibiashara hata kidogo itumike lugha sahihi kwa hawa wadau wanachangia pato letu la taifa.
Tuelimishe tuijue hiyo kauli ya kibiashara. Kauli ya rais ni sheria.
 
hahaha usicheze na ile budget ya tril 29 tunazipataje unafikiri wakati bakuli hatutaki kutembeza na vyote lazima vifanyike kwa huo mwaka wa budget?stay tune mchawi atapatikana maana huu mchezo hauhitaji hasira.
Na ile vat ya benki.
 
Nafikiri suala la watalii tunatakiwa tuliangalie siyo tu kwa misingi ya kodi lakini pia athari nyingine chanya kwa ujio wao au uwepo wao (kama ni wa ndani). Ujio wa watalii unaongeza mapato kwenye hoteli zilizopo ndani ya nchi lakini pia wanapokuja huku wengi wanatumika kama njia ya kuvutia wengine wanaporejea makwao.

Pia, makampuni ya usafairishaji yanapata mapato pale watalii wanapokuwa wengi, ambapo mwisho wa siku watalipa kodi. Kuna makampuni ya ndege ndogo ndogo zinazokwenda maeneo mbali ya kitalii ndani ya nchi. Uamuzi wa serikali usipovutia watalii utapelekea kupungua kwa watalii jambo ambalo litaathiri vibaya uendeshaji wa makampuni ya usafirishaji, hoteli na kadharika. Wapo pia wajasiriamali ambao wanaendesha maisha yao kwa kutegemea kuuza bidhaa kama mavazi na vinyago, kadri watalii wanavyopungua ndivyo biashara zao zinadoda na ndivyo kiwango cha fursa za ajira zinapungua. Yote haya yametoa ajira kwa watanzania wengi.

Ni vizuri serikali ikaona uwezekano wa kuwa na uvutiaji zaidi wa watalii badala ya kupandisha kodi.

Miaka ya hivi karibuni serikali kupitia Bodi ya Watalii imekuwa ikitumia pesa nyingi kutangaza utalii nje ya nchi, sasa ni vizuri serikali ikakumbuka kwamba uwekezaji amabo umefanyika miaka ya hivi karibuni ni billioni za pesa katika kujaribu kuifahamisha Tanzania katika medani ya utalii. Kupandisha kodi kunaweza kuharibu tena jitihada ambazo zimekuwa zikifanyika tena kwa gharama kubwa. Biashara ya utalii kwa sehemu kubwa inajitangaza yenyewe kupitia watalii wenyewe wanaokuwa wanaingia nchini, kama uamuzi wowote wa serikali utapelekea kuvunja moyo watalii, tuwe na uhakika kwamba baada ya muda mfupi ujao kodi hiyo hiyo tuliyokusanya kwa wachache itaanza kutumika kulipia matangazo ya gharama za juu.
 
Mmmmm na wewe ndio bure kabisa! Ameongelea idadi....ametaja namba halisi (rejea clips yake) kabisa wewe unasema kodi? JPM amepotoshwa! Hajui kanuni za uchumi wala hajui business!
Unapotosha.

Rais hakuongelea "ada ndogo" na "ada kubwa". Rais Magufuli ameongelea kodi.

Mkisoma hamuelewi basi hata kusikia hamsikii?
 
Kwa mtazamo wa kisomi jamaa ameandika vitu muhimu sana ila kwa mtazamo hasi hii mada utaingalia kiulumumba zaidi. Watalii wakiwa wengi hata wale wauzaji wa mapambo ya asili huwa nao wanaoneza kipato chao kwa namna moja au nyingine.Kwa ufupi pato la taifa sio lazima liingie moja kwa moja serikalini kwa hao watalii kulipa hela zote serikalini ila wakinunua hayo mapambo hata serikali pia inafaidika .Kiuchumi ili tuende sawa inabidi tuwe na watalii wengi zaidi nahisi Kenya walitutega kidogo nasi tukategeka maana kwenye sekta ya utalii wale jamaa ni wapinzani wetu wa kibiashara sidhani kama wanatutakia mema kwenye hiyo biashara.

Nakuunga mkono mkuu Malisa G J
 
Labda anadhani kanuni za fedha na uchumi ni sawa sawa na kukariri chemical formulae.
 
Sawa mkuu lakini vipi akisikia kuna wapo wanyama anaweza kuwaona bila VAT bado atakuja kwako kwa vile tu yeye hana tatizo la ulipaji wa VAT??SIO KWELI.

Hakuna ngorongoro wala kilimanjaro huko kenya. Hifadhi za Maasai Mara na Tsavo zimekuwa majangwa. Nilikwenda Mombasa sikuona hata kanga ambao walikuwa ndiyo kivutio kikubwa tsavo baada ya simba ambao wamebaki jina tu kwenye kitabu kinachoitwa' Simba wa Tsavo' ambao waliwala wahindi waliokuwa wanajenga reli. Kwa hiyo hakutakuwa na ombwe la watalii Tanzania.
 
Unapotosha.

Rais hakuongelea "ada ndogo" na "ada kubwa". Rais Magufuli ameongelea kodi.

Mkisoma hamuelewi basi hata kusikia hamsikii?
Hivi kuna siku umeona serikali ilipokosea..?? AU inaundwa na malaika..??
 
Kwa mtazamo wa kisomi jamaa ameandika vitu muhimu sana ila kwa mtazamo hasi hii mada utaingalia kiulumumba zaidi. Watalii wakiwa wengi hata wale wauzaji wa mapambo ya asili huwa nao wanaoneza kipato chao kwa namna moja au nyingine.Kwa ufupi pato la taifa sio lazima liingie moja kwa moja serikalini kwa hao watalii kulipa hela zote serikalini ila wakinunua hayo mapambo hata serikali pia inafaidika .Kiuchumi ili tuende sawa inabidi tuwe na watalii wengi zaidi nahisi Kenya walitutega kidogo nasi tukategeka maana kwenye sekta ya utalii wale jamaa ni wapinzani wetu wa kibiashara sidhani kama wanatutakia mema kwenye hiyo biashara.

Nakuunga mkono mkuu Malisa G J
Multiplication effect know how
 
Back
Top Bottom