Kuna mambo mawili Rais kapotoshwa

Kuna mambo mawili Rais kapotoshwa

Tanzania tunalenga high value tourist.Mtalii anayekaa hotel za kitalii.Anakuja analala hotel anaalipa dola 800 kwa siku ambayo ni sawa na milioni moja na laki sita.Mtalii mmoja kama huyo sio sawa na kuleta watalii 100 WANAOLIPA GUEST HOUSE uchochoroni 16,000 kwa siku.Unakuwa na umati wa watu maskini mjini.ANGALIA GHARAMA wanazoweza sababisha kwa kunya na kuzoa huo uchafu wa mtu mmoja na hao mia .Utajikuta ukitoa gharama za kuzoa vyoo vyao unabaki na hela ndogo mno kama faida ukiendekeza umati wa watalii maskini.
 
Big up Malisa,

Lakini pia Rais hajashautiwa vizuri suala la kupoteza ajira. Upungufu wa meli na watalii usiangaliwe kwa maana ya serikali inapata nini kama kodi lakini ilipaswa kuangalia inalinda vipi ajira na hata kutengeneza ajirampya. Kwa mtazamo waje wachache ama makontainer machache kuna ajira zinapoteA. JE YALE MAPATO TUNAYOYAPAT yanatengeneza ajira nyingi kuliko tulizopoteza?(substitution effect).
 
Jingine kama dhamira nikuhakikisha kodi inakusanywa vilivyo, basi ile misamaha ya kodi kwenye mafuta yanayopelekwa kwenye migodi iondolewe. Pia nafuu za kodi zinazotozwa migodini ziondolewe ili kuwe na usawa kwenye maeneo yite ya uzalishaji.
 
Unapotosha.

Rais hakuongelea "ada ndogo" na "ada kubwa". Rais Magufuli ameongelea kodi.

Mkisoma hamuelewi basi hata kusikia hamsikii?
Unaelewa tofauti ya kodi(tax) na ada(fees) wewe? Niambie malipo ya kuzuru mbuga za wanyama yanawezaje kuwa tax? How do they calculate in terms of percentage if it's tax?
 
Acha uhayawani wewe,.,. Unajiona unafatilia Sana kuliko wengne? Aliongelea map to makubwa na madgo PIA... Don't be stupid... Afu huwa nakutazama na pumba zako uko kama hayawani flan hv
 
Kwanza kuna tofauti kubwa sana kwa ujio wa watalii wachache na wengi kwa wananchi wa kawaida mmoja mmoja.
Hili hata akienda kuwauliza wale wakina mama wa kimasai wauza shanga wanaweza kumuelimisha.
Ina maana hao wakina mama wanajua hiyo tofauti japokuwa hawana elimu ila Rais hajui?Ndio maana yako hiyo???
 
Naunga mkono juhudi za Rais kuongeza wigo wa pato la taifa, lakini anahitaji wachumi wazuri kumshauri kwa sababu kuna mambo anapotoshwa. Mojawapo ni hili la watalii. Rais amesema ameongeza ada ya watalii (VAT) na asiyetaka asije. Anasema ni heri kupata watalii wachache wanaolipa ada kubwa kuliko watalii wengi wanaolipa ada ndogo. Kuna mambo mawili Rais kapotoshwa;

#Mosi, kanuni za uchumi zinaelekeza kutoza ada ndogo kwa rasilimali isiyoisha na kutoza ada kubwa kwa rasilimali inayoisha. Kwa mfano watalii wanapaswa kutozwa ada ndogo kwa sababu hawapunguzi chochote kuja kutembelea Tanzania, na sekta ya madini/gesi zinapaswa kutozwa ada kubwa kwa sababu zinapungua kadri zinavyotumika (ipo siku zitaisha).

Rasilimali ambazo zikitumika zinaisha zinapaswa kuwa na ada kubwa, na zile ambazo zikitumika haziishi ada yake inapaswa kuwa ndogo. Simba wa mikumi hawezi kufa kwa kuangaliwa na watalii milioni 1 au kupigwa maelfu ya picha, wala mlima Kilimanjaro hauwezi kudidimia kwa sababu watalii wengi wameupanda. Kwahiyo ada ya utalii inapaswa kuwa ndogo (affordable).

Lakini ilivyo kwa sasa ni vice versa. Rasilimali zinazoisha kama gesi na madini zinatozwa ada ndogo na zile zisizoisha kama utalii zinatozwa ada kubwa. Rais anapaswa kushauriwa vzr zaidi ktk hili.

#Pili; Si kweli kwamba tukipata watalii wachache wanaolipa ada kubwa mapato yetu yataongezeka kama alivyosema Rais Magufuli. Mapato yangeongezeka kama tungepata watalii wengi wanaolipa ada ndogo si watalii wachache wanaolipa ada kubwa. Kanuni za uchumi zinaeleza kuwa biashara nzuri ni ile yenye faida ndogo lakini ina wateja wengi, na sio yenye faida kubwa lakini ina wateja wachache.

Ndio maana Bakhresa anauza juice na maandazi lakini anawazidi wanaouza magari. Hii ni kwa sababu Bakhresa anapata faida ndogo kwa watu wengi tofauti na wauza magari wanaopata faida kubwa kwa watu wachache. Bakhresa anaweza kupata faida ya sh.200 tu kwa kila juice lakini akauza juice milioni moja kwa siku. So akapata faida ya milioni 200 daily. Muuza magari anaweza kupata faida ya milioni 10 kwa kila gari lakini akauza gari 1 tu kwa siku. Kwa hesabu hii Bakhresa amemzidi muuza magari kwa milioni 190 kila siku.

Kwahiyo kama tukitaka kufanikiwa ktk sekta ya utalii kodi ya VAT iondolewe. Hii itafanya kupata watalii wengi watakaolipa ada ndogo hivyo kupata mapato makubwa, kuliko sasa hivi ambapo tunapata watalii wachache wanaolipa ada kubwa na hivyo kuambulia mapato madogo.

Na athari zake zimeanza kuonekana kwa sababu idadi ya watalii imepungua maradufu tangu gharama zilipopandishwa. Wengi wamekimbilia Kenya. Hakuna mtalii anayeweza kulipa mamia ya dola kumuona Simba Tarangire wakati nusu ya pesa hiyo anaweza kuitumia kumuona Simba mbuga ya Tsavo nchini Kenya. Hii si dalili nzuri kwa ustawi wa uchumi wetu. Nitaeleza vizuri kwenye #JamboLeo ya jumanne July 26.

Malisa G.J
Ndugu yangu Malisa kuna mambo huyajui. Bora ukae kimya. Tulipofikia mambo yalikuwa sivyo. Lazima kuweka nidhamu kwanza
 
Tanzania tunalenga high value tourist.Mtalii anayekaa hotel za kitalii.Anakuja analala hotel anaalipa dola 800 kwa siku ambayo ni sawa na milioni moja na laki sita.Mtalii mmoja kama huyo sio sawa na kuleta watalii 100 WANAOLIPA GUEST HOUSE uchochoroni 16,000 kwa siku.Unakuwa na umati wa watu maskini mjini.ANGALIA GHARAMA wanazoweza sababisha kwa kunya na kuzoa huo uchafu wa mtu mmoja na hao mia .Utajikuta ukitoa gharama za kuzoa vyoo vyao unabaki na hela ndogo mno kama faida ukiendekeza umati wa watalii maskini.
Ficha upumbavu wako.
 
Unaelewa tofauti ya kodi(tax) na ada(fees) wewe? Niambie malipo ya kuzuru mbuga za wanyama yanawezaje kuwa tax? How do they calculate in terms of percentage if it's tax?
Achana nae uyo,kashikiwa akili .
 
Naunga mkono juhudi za Rais kuongeza wigo wa pato la taifa, lakini anahitaji wachumi wazuri kumshauri kwa sababu kuna mambo anapotoshwa. Mojawapo ni hili la watalii. Rais amesema ameongeza ada ya watalii (VAT) na asiyetaka asije. Anasema ni heri kupata watalii wachache wanaolipa ada kubwa kuliko watalii wengi wanaolipa ada ndogo. Kuna mambo mawili Rais kapotoshwa;

#Mosi, kanuni za uchumi zinaelekeza kutoza ada ndogo kwa rasilimali isiyoisha na kutoza ada kubwa kwa rasilimali inayoisha. Kwa mfano watalii wanapaswa kutozwa ada ndogo kwa sababu hawapunguzi chochote kuja kutembelea Tanzania, na sekta ya madini/gesi zinapaswa kutozwa ada kubwa kwa sababu zinapungua kadri zinavyotumika (ipo siku zitaisha).

Rasilimali ambazo zikitumika zinaisha zinapaswa kuwa na ada kubwa, na zile ambazo zikitumika haziishi ada yake inapaswa kuwa ndogo. Simba wa mikumi hawezi kufa kwa kuangaliwa na watalii milioni 1 au kupigwa maelfu ya picha, wala mlima Kilimanjaro hauwezi kudidimia kwa sababu watalii wengi wameupanda. Kwahiyo ada ya utalii inapaswa kuwa ndogo (affordable).

Lakini ilivyo kwa sasa ni vice versa. Rasilimali zinazoisha kama gesi na madini zinatozwa ada ndogo na zile zisizoisha kama utalii zinatozwa ada kubwa. Rais anapaswa kushauriwa vzr zaidi ktk hili.

#Pili; Si kweli kwamba tukipata watalii wachache wanaolipa ada kubwa mapato yetu yataongezeka kama alivyosema Rais Magufuli. Mapato yangeongezeka kama tungepata watalii wengi wanaolipa ada ndogo si watalii wachache wanaolipa ada kubwa. Kanuni za uchumi zinaeleza kuwa biashara nzuri ni ile yenye faida ndogo lakini ina wateja wengi, na sio yenye faida kubwa lakini ina wateja wachache.

Ndio maana Bakhresa anauza juice na maandazi lakini anawazidi wanaouza magari. Hii ni kwa sababu Bakhresa anapata faida ndogo kwa watu wengi tofauti na wauza magari wanaopata faida kubwa kwa watu wachache. Bakhresa anaweza kupata faida ya sh.200 tu kwa kila juice lakini akauza juice milioni moja kwa siku. So akapata faida ya milioni 200 daily. Muuza magari anaweza kupata faida ya milioni 10 kwa kila gari lakini akauza gari 1 tu kwa siku. Kwa hesabu hii Bakhresa amemzidi muuza magari kwa milioni 190 kila siku.

Kwahiyo kama tukitaka kufanikiwa ktk sekta ya utalii kodi ya VAT iondolewe. Hii itafanya kupata watalii wengi watakaolipa ada ndogo hivyo kupata mapato makubwa, kuliko sasa hivi ambapo tunapata watalii wachache wanaolipa ada kubwa na hivyo kuambulia mapato madogo.

Na athari zake zimeanza kuonekana kwa sababu idadi ya watalii imepungua maradufu tangu gharama zilipopandishwa. Wengi wamekimbilia Kenya. Hakuna mtalii anayeweza kulipa mamia ya dola kumuona Simba Tarangire wakati nusu ya pesa hiyo anaweza kuitumia kumuona Simba mbuga ya Tsavo nchini Kenya. Hii si dalili nzuri kwa ustawi wa uchumi wetu. Nitaeleza vizuri kwenye #JamboLeo ya jumanne July 26.

Malisa G.J
MALISA UCHUMI ULISOMEA WAPI NA NI CHUO GANI HICHO?
MASWALA YA GAS NA MIKATABA YA MADINI NDIO HUJUI KABISA WEWE UNACHOJUA NI KUANDIKA... WANGEONGEZA TOZO KWENYE GAS NA MADINI BADO MGESEMA WANA KIMBIZA WAWEKEZAJI...

NI WAZI HUJUI NA WENGI HAMJUI KINACHO ENDELEA KWENYE HIYO GAS...
 
Back
Top Bottom