Kuna mambo mawili Rais kapotoshwa

Kuna mambo mawili Rais kapotoshwa

Tatizo kubwa la Serikali yetu, " Wanajua sana namba, lakini hawajui hesabu" Serikali yetu ingekuwa inajua Hesabu, Tanzania tungekuwa mbali sana kiuchumi.
Hahahah kwani mkuu wetu si mwana mahesabu au ni mwana namba nikajua atalenga shabaha angalau!!!!!
 
Unajua kama mpotoshaji na mpotoshwaji wote wanamakosa?
 
Unajua baba mwenye nyumba hataki ushauri akiamua lake na hili la VAT kwa watalii muda mfupi lazima lilete athari kama ilivyokuwa sukari ambapo kama angekubali kukosolewa leo tusingenunua sukari 3000 mwishowe utasikia analalamika kutafuta mchawi akidai anahujumiw
hahaha usicheze na ile budget ya tril 29 tunazipataje unafikiri wakati bakuli hatutaki kutembeza na vyote lazima vifanyike kwa huo mwaka wa budget?stay tune mchawi atapatikana maana huu mchezo hauhitaji hasira.
 
Unapotosha.

Rais hakuongelea "ada ndogo" na "ada kubwa". Rais Magufuli ameongelea kodi.

Mkisoma hamuelewi basi hata kusikia hamsikii?

nini usichoelewa kuhusu kodi kubwa huongeza gharama ya kitu/huduma kwa mlaji?!
 
Unapotosha.

Rais hakuongelea "ada ndogo" na "ada kubwa". Rais Magufuli ameongelea kodi.

Mkisoma hamuelewi basi hata kusikia hamsikii?
Kodi ni dhana pana sana bi mkubwa! Kuna Excise Duty, Custom Duty, Corporate Tax, Pay As You Earn, Value Added Tax, Rolalty, na mengine mengi. Sasa jamaa anaongelea VAT wewe unaturudisha tena nyuma. Yaani unatoka kwenye specific unarudi kwenye general! Au hapo Lumumba mnaambiwa ni kodi tu basi?
 
Ada ya nini. Si ameongelea VAT au wewe ndio hukusikia. Haya tuache rais mpango wakati wa bajeti alisema ushauri wamechukua kenya. Wakati kenya wametoa hizo tozo huoni sarakasi hizo.
Kweli mkuu kenya walifanya km tunavyofanya leo lkn waliona wanapata hasara kubwa kuliko faida hivyo wakaamua kuziondoa.
Ngoja tuone anakotupeleka
Kweny miamala ya simu walisema vat ni ya kampuni lkn leo wananchi ndiyo wanaoumia kuilipa hiyo vat 18% lkn serikali imekaa kimya.
Haya bei ya sukari elekezi imeishia wapi?
Siku zote wanaoumia ni watu wa chini wanyonge na sio hao walioko juu.
Haya ajira zimesimamishwa lkn watu wanaona kawaida tu.
Anayeteseka na hii nchi ni mwananchi wa chini kbsa anayeishi chini ya dola 1 lkn hao wajuu hata km bei ya nyama kilo ifike 30,000 watanunua tu. Je, ww mtanzania mwenzangu tutaweza kununua?
 
Unapotosha.

Rais hakuongelea "ada ndogo" na "ada kubwa". Rais Magufuli ameongelea kodi.

Mkisoma hamuelewi basi hata kusikia hamsikii?
Wewe ajuza umerudi? Mkatoliki naona anazidi kuwapunguza kwenye nafasi nyeti kila siku.
 
Hoja hupingwa kwa hoja siyo porojo kama hajui uchumi leta mawazo kuhusu uchumi tuone
MALISA UCHUMI ULISOMEA WAPI NA NI CHUO GANI HICHO?
MASWALA YA GAS NA MIKATABA YA MADINI NDIO HUJUI KABISA WEWE UNACHOJUA NI KUANDIKA... WANGEONGEZA TOZO KWENYE GAS NA MADINI BADO MGESEMA WANA KIMBIZA WAWEKEZAJI...

NI WAZI HUJUI NA WENGI HAMJUI KINACHO ENDELEA KWENYE HIYO GAS...
 
Hii nchi yetu na wao hawana cha kutushauri. Kwanza wanyamaze watuache tufanye kazi. Shut up until 2020 full stop. Polisi simamieni utekelezaji wa hilo.
 
Mi nachoona ni angepiga kimya...maana tunatangaza utalii huku rais anasema (indirectly) kuwa kama mmesusa hakuna anayejali...

Kodi walipe na hakuna haja ya kurudia rudia kutangaza hili...wanaweza wasije si sababu ya gharama ila sababu watanzania hawajali ujio wao...akati nchi nyingine zinawapigia magoti...
BIASHARA ushawishi

Vitendo ni bora mara mia kuliko maneno. Siyo kila kitu lazima uzungumzie.
Kumpiga adui kimya kimya unashinda vita kirahisi kuliko kutangaza.
 
Mi nachoona ni angepiga kimya...maana tunatangaza utalii huku rais anasema (indirectly) kuwa kama mmesusa hakuna anayejali...

Kodi walipe na hakuna haja ya kurudia rudia kutangaza hili...wanaweza wasije si sababu ya gharama ila sababu watanzania hawajali ujio wao...akati nchi nyingine zinawapigia magoti...
BIASHARA ushawishi

Naomba nigeuze upande wa pili wa shilingi katika hili.

Hata hao watalii wanahitaji miundo mbinu iliyo bora ambayo lazima itokane na kodi zao, kwa sasa hatuna chanzo kingine cha kufikia matarajio hayo zaidi ya kuangalia kilichopo kwenye bakuli letu. Hayo madini na mirabaha kwenye taasisi tulizoziuzia hisa au mashirika yetu tulishaingizwa mkenge na watangulizi wa mheshimiwa kumudu kupata kile tunachostahili ni jambo ambalo linahitaji mchakato maana ni suala la mikataba mibovu kwa hiyo nchi haiwezi kusimama ni lazima maisha yaendelee na watu tusonge mbele.

Tukifanikiwa kuboresha mazingira ya miundo mbinu yetu watalii watakuja maana tunavyo vivutio ambavyo wengine hawana na ni lazima kuna cream ya watalii tutakayoipata ambayo iko tayari ku spend.

Mimi naamini iko nia njema kwa kweli, kinachotakiwa ni usimamizi mzuri na pesa kuelekezwa katika kuboresha maeneo ya vivutio.
 
Tanzania tunalenga high value tourist.Mtalii anayekaa hotel za kitalii.Anakuja analala hotel anaalipa dola 800 kwa siku ambayo ni sawa na milioni moja na laki sita.Mtalii mmoja kama huyo sio sawa na kuleta watalii 100 WANAOLIPA GUEST HOUSE uchochoroni 16,000 kwa siku.Unakuwa na umati wa watu maskini mjini.ANGALIA GHARAMA wanazoweza sababisha kwa kunya na kuzoa huo uchafu wa mtu mmoja na hao mia .Utajikuta ukitoa gharama za kuzoa vyoo vyao unabaki na hela ndogo mno kama faida ukiendekeza umati wa watalii maskini.
Piga hesabu hao 100 watanufaisha wangapi kulingana na kipato chetu, na huyo mmoja atanufaisha wangapi kulingana na kipato chetu!
 
Njaa ndugu yangu, Njaa acha kabisa. waliposema adui yako Muombee Njaa walikuwa wameona mbali. Asilimia Kubwa ya matendo ya binadamu na maneno yao nyuma yake yanasukumwa na Njaa. Njaa tu. wala hamna kitu kingine ni njaa tu.

Nimeanza kukupenda kama sasa umejirekebisha na kuanza kumsifu Mkatoliki.
 
Back
Top Bottom