Kuna mambo mawili Rais kapotoshwa

Kuna mambo mawili Rais kapotoshwa

Naunga mkono juhudi za Rais kuongeza wigo wa pato la taifa, lakini anahitaji wachumi wazuri kumshauri kwa sababu kuna mambo anapotoshwa. Mojawapo ni hili la watalii. Rais amesema ameongeza ada ya watalii (VAT) na asiyetaka asije. Anasema ni heri kupata watalii wachache wanaolipa ada kubwa kuliko watalii wengi wanaolipa ada ndogo. Kuna mambo mawili Rais kapotoshwa;

#Mosi, kanuni za uchumi zinaelekeza kutoza ada ndogo kwa rasilimali isiyoisha na kutoza ada kubwa kwa rasilimali inayoisha. Kwa mfano watalii wanapaswa kutozwa ada ndogo kwa sababu hawapunguzi chochote kuja kutembelea Tanzania, na sekta ya madini/gesi zinapaswa kutozwa ada kubwa kwa sababu zinapungua kadri zinavyotumika (ipo siku zitaisha).

Rasilimali ambazo zikitumika zinaisha zinapaswa kuwa na ada kubwa, na zile ambazo zikitumika haziishi ada yake inapaswa kuwa ndogo. Simba wa mikumi hawezi kufa kwa kuangaliwa na watalii milioni 1 au kupigwa maelfu ya picha, wala mlima Kilimanjaro hauwezi kudidimia kwa sababu watalii wengi wameupanda. Kwahiyo ada ya utalii inapaswa kuwa ndogo (affordable).

Lakini ilivyo kwa sasa ni vice versa. Rasilimali zinazoisha kama gesi na madini zinatozwa ada ndogo na zile zisizoisha kama utalii zinatozwa ada kubwa. Rais anapaswa kushauriwa vzr zaidi ktk hili.

#Pili; Si kweli kwamba tukipata watalii wachache wanaolipa ada kubwa mapato yetu yataongezeka kama alivyosema Rais Magufuli. Mapato yangeongezeka kama tungepata watalii wengi wanaolipa ada ndogo si watalii wachache wanaolipa ada kubwa. Kanuni za uchumi zinaeleza kuwa biashara nzuri ni ile yenye faida ndogo lakini ina wateja wengi, na sio yenye faida kubwa lakini ina wateja wachache.

Ndio maana Bakhresa anauza juice na maandazi lakini anawazidi wanaouza magari. Hii ni kwa sababu Bakhresa anapata faida ndogo kwa watu wengi tofauti na wauza magari wanaopata faida kubwa kwa watu wachache. Bakhresa anaweza kupata faida ya sh.200 tu kwa kila juice lakini akauza juice milioni moja kwa siku. So akapata faida ya milioni 200 daily. Muuza magari anaweza kupata faida ya milioni 10 kwa kila gari lakini akauza gari 1 tu kwa siku. Kwa hesabu hii Bakhresa amemzidi muuza magari kwa milioni 190 kila siku.

Kwahiyo kama tukitaka kufanikiwa ktk sekta ya utalii kodi ya VAT iondolewe. Hii itafanya kupata watalii wengi watakaolipa ada ndogo hivyo kupata mapato makubwa, kuliko sasa hivi ambapo tunapata watalii wachache wanaolipa ada kubwa na hivyo kuambulia mapato madogo.

Na athari zake zimeanza kuonekana kwa sababu idadi ya watalii imepungua maradufu tangu gharama zilipopandishwa. Wengi wamekimbilia Kenya. Hakuna mtalii anayeweza kulipa mamia ya dola kumuona Simba Tarangire wakati nusu ya pesa hiyo anaweza kuitumia kumuona Simba mbuga ya Tsavo nchini Kenya. Hii si dalili nzuri kwa ustawi wa uchumi wetu. Nitaeleza vizuri kwenye #JamboLeo ya jumanne July 26.

Malisa G.J
Uchambuzi mzuri sana nimeupenda ila umeacha kidg kueleza athari ya kukosekana kwa watalii kutokana na tozo la VAT kwenye mahoteli ya kitalii ambayo pia yanachangia pato la serikali kwa njia ya kulipa kodi. Nakupongeza sana kwa uchambuz wenye ushauri mzuri ila tatizo kuna wachache humu wataanza kunyanyua midomo yao na kupuuza ushauri huu. Big Up mkuu
 
Unapotosha.

Rais hakuongelea "ada ndogo" na "ada kubwa". Rais Magufuli ameongelea kodi.

Mkisoma hamuelewi basi hata kusikia hamsikii?

Wanaopiga kelele waelewe kuwa mzungu anaheshimu sana ulipaji wa kodi. Tena tukijitegemea itakuwa nafuu kwao kwani ziara za kutembeza bakuli zitapungua. Kwa taarifa sahihi ni kwamba tour operators hawataki uwazi katika mapato yao na wanaogopa hizo return za VAT zitawaumbua.
 
Mleta mada umeeleweka vizuri tu.

Tunaoko elekea ni gizani...utalii ungeweza kuongeza sana pato la taifa, lakini si kwa kupiga vijembe hivi mara hatutaki watalii maskini. Haya majigambo hayawezi kutusaidia chochote.
 
Unapotosha.

Rais hakuongelea "ada ndogo" na "ada kubwa". Rais Magufuli ameongelea kodi.

Mkisoma hamuelewi basi hata kusikia hamsikii?
Haya wewe ndio unaelewa kuliko wengine. Hivi ile Mnayokata kwenye miamala ya simu Pesa na benki ni nani anayetakiwa kulipa!?
 
Naunga mkono juhudi za Rais kuongeza wigo wa pato la taifa, lakini anahitaji wachumi wazuri kumshauri kwa sababu kuna mambo anapotoshwa. Mojawapo ni hili la watalii. Rais amesema ameongeza ada ya watalii (VAT) na asiyetaka asije. Anasema ni heri kupata watalii wachache wanaolipa ada kubwa kuliko watalii wengi wanaolipa ada ndogo. Kuna mambo mawili Rais kapotoshwa;

#Mosi, kanuni za uchumi zinaelekeza kutoza ada ndogo kwa rasilimali isiyoisha na kutoza ada kubwa kwa rasilimali inayoisha. Kwa mfano watalii wanapaswa kutozwa ada ndogo kwa sababu hawapunguzi chochote kuja kutembelea Tanzania, na sekta ya madini/gesi zinapaswa kutozwa ada kubwa kwa sababu zinapungua kadri zinavyotumika (ipo siku zitaisha).

Rasilimali ambazo zikitumika zinaisha zinapaswa kuwa na ada kubwa, na zile ambazo zikitumika haziishi ada yake inapaswa kuwa ndogo. Simba wa mikumi hawezi kufa kwa kuangaliwa na watalii milioni 1 au kupigwa maelfu ya picha, wala mlima Kilimanjaro hauwezi kudidimia kwa sababu watalii wengi wameupanda. Kwahiyo ada ya utalii inapaswa kuwa ndogo (affordable).

Lakini ilivyo kwa sasa ni vice versa. Rasilimali zinazoisha kama gesi na madini zinatozwa ada ndogo na zile zisizoisha kama utalii zinatozwa ada kubwa. Rais anapaswa kushauriwa vzr zaidi ktk hili.

#Pili; Si kweli kwamba tukipata watalii wachache wanaolipa ada kubwa mapato yetu yataongezeka kama alivyosema Rais Magufuli. Mapato yangeongezeka kama tungepata watalii wengi wanaolipa ada ndogo si watalii wachache wanaolipa ada kubwa. Kanuni za uchumi zinaeleza kuwa biashara nzuri ni ile yenye faida ndogo lakini ina wateja wengi, na sio yenye faida kubwa lakini ina wateja wachache.

Ndio maana Bakhresa anauza juice na maandazi lakini anawazidi wanaouza magari. Hii ni kwa sababu Bakhresa anapata faida ndogo kwa watu wengi tofauti na wauza magari wanaopata faida kubwa kwa watu wachache. Bakhresa anaweza kupata faida ya sh.200 tu kwa kila juice lakini akauza juice milioni moja kwa siku. So akapata faida ya milioni 200 daily. Muuza magari anaweza kupata faida ya milioni 10 kwa kila gari lakini akauza gari 1 tu kwa siku. Kwa hesabu hii Bakhresa amemzidi muuza magari kwa milioni 190 kila siku.

Kwahiyo kama tukitaka kufanikiwa ktk sekta ya utalii kodi ya VAT iondolewe. Hii itafanya kupata watalii wengi watakaolipa ada ndogo hivyo kupata mapato makubwa, kuliko sasa hivi ambapo tunapata watalii wachache wanaolipa ada kubwa na hivyo kuambulia mapato madogo.

Na athari zake zimeanza kuonekana kwa sababu idadi ya watalii imepungua maradufu tangu gharama zilipopandishwa. Wengi wamekimbilia Kenya. Hakuna mtalii anayeweza kulipa mamia ya dola kumuona Simba Tarangire wakati nusu ya pesa hiyo anaweza kuitumia kumuona Simba mbuga ya Tsavo nchini Kenya. Hii si dalili nzuri kwa ustawi wa uchumi wetu. Nitaeleza vizuri kwenye #JamboLeo ya jumanne July 26.

Malisa G.J
Kweli kabisa, mara nyingine huwa najiuliza hao washauri wa Rais wanamwogopa au???

Hii ni commerce ya form one.
 
Nakupongeza mchambuzi wa hili suala, nina amini ipo siku wataelewa, Suala la utalii ni suala ambalo ni nyeti sana, linahitaji umakini mkubwa kabla ya likufanyia maamuzi yoyote. Si muda mlefu watu wata anza kupoteza ajira zao,
 
Mleta mada umeeleweka vizuri tu.

Tunaoko elekea ni gizani...utalii ungeweza kuongeza sana pato la taifa, lakini si kwa kupiga vijembe hivi mara hatutaki watalii maskini. Haya majigambo hayawezi kutusaidia chochote.
Unajua baba mwenye nyumba hataki ushauri akiamua lake na hili la VAT kwa watalii muda mfupi lazima lilete athari kama ilivyokuwa sukari ambapo kama angekubali kukosolewa leo tusingenunua sukari 3000 mwishowe utasikia analalamika kutafuta mchawi akidai anahujumiw
 
Naunga mkono juhudi za Rais kuongeza wigo wa pato la taifa, lakini anahitaji wachumi wazuri kumshauri kwa sababu kuna mambo anapotoshwa. Mojawapo ni hili la watalii. Rais amesema ameongeza ada ya watalii (VAT) na asiyetaka asije. Anasema ni heri kupata watalii wachache wanaolipa ada kubwa kuliko watalii wengi wanaolipa ada ndogo. Kuna mambo mawili Rais kapotoshwa;

#Mosi, kanuni za uchumi zinaelekeza kutoza ada ndogo kwa rasilimali isiyoisha na kutoza ada kubwa kwa rasilimali inayoisha. Kwa mfano watalii wanapaswa kutozwa ada ndogo kwa sababu hawapunguzi chochote kuja kutembelea Tanzania, na sekta ya madini/gesi zinapaswa kutozwa ada kubwa kwa sababu zinapungua kadri zinavyotumika (ipo siku zitaisha).

Rasilimali ambazo zikitumika zinaisha zinapaswa kuwa na ada kubwa, na zile ambazo zikitumika haziishi ada yake inapaswa kuwa ndogo. Simba wa mikumi hawezi kufa kwa kuangaliwa na watalii milioni 1 au kupigwa maelfu ya picha, wala mlima Kilimanjaro hauwezi kudidimia kwa sababu watalii wengi wameupanda. Kwahiyo ada ya utalii inapaswa kuwa ndogo (affordable).

Lakini ilivyo kwa sasa ni vice versa. Rasilimali zinazoisha kama gesi na madini zinatozwa ada ndogo na zile zisizoisha kama utalii zinatozwa ada kubwa. Rais anapaswa kushauriwa vzr zaidi ktk hili.

#Pili; Si kweli kwamba tukipata watalii wachache wanaolipa ada kubwa mapato yetu yataongezeka kama alivyosema Rais Magufuli. Mapato yangeongezeka kama tungepata watalii wengi wanaolipa ada ndogo si watalii wachache wanaolipa ada kubwa. Kanuni za uchumi zinaeleza kuwa biashara nzuri ni ile yenye faida ndogo lakini ina wateja wengi, na sio yenye faida kubwa lakini ina wateja wachache.

Ndio maana Bakhresa anauza juice na maandazi lakini anawazidi wanaouza magari. Hii ni kwa sababu Bakhresa anapata faida ndogo kwa watu wengi tofauti na wauza magari wanaopata faida kubwa kwa watu wachache. Bakhresa anaweza kupata faida ya sh.200 tu kwa kila juice lakini akauza juice milioni moja kwa siku. So akapata faida ya milioni 200 daily. Muuza magari anaweza kupata faida ya milioni 10 kwa kila gari lakini akauza gari 1 tu kwa siku. Kwa hesabu hii Bakhresa amemzidi muuza magari kwa milioni 190 kila siku.

Kwahiyo kama tukitaka kufanikiwa ktk sekta ya utalii kodi ya VAT iondolewe. Hii itafanya kupata watalii wengi watakaolipa ada ndogo hivyo kupata mapato makubwa, kuliko sasa hivi ambapo tunapata watalii wachache wanaolipa ada kubwa na hivyo kuambulia mapato madogo.

Na athari zake zimeanza kuonekana kwa sababu idadi ya watalii imepungua maradufu tangu gharama zilipopandishwa. Wengi wamekimbilia Kenya. Hakuna mtalii anayeweza kulipa mamia ya dola kumuona Simba Tarangire wakati nusu ya pesa hiyo anaweza kuitumia kumuona Simba mbuga ya Tsavo nchini Kenya. Hii si dalili nzuri kwa ustawi wa uchumi wetu. Nitaeleza vizuri kwenye #JamboLeo ya jumanne July 26.

Malisa G.J
MALISA UCHUMI ULISOMEA WAPI NA NI CHUO GANI HICHO?
MASWALA YA GAS NA MIKATABA YA MADINI NDIO HUJUI KABISA WEWE UNACHOJUA NI KUANDIKA... WANGEONGEZA TOZO KWENYE GAS NA MADINI BADO MGESEMA WANA KIMBIZA WAWEKEZAJI...

NI WAZI HUJUI NA WENGI HAMJUI KINACHO ENDELEA KWENYE HIYO GAS...
tuelezee unachojua mkuu
 
We kijana wewe, mbona nasikia eti Tembo wetu wanaisha kwa kasi ya ajabu? Sasa si ni bora walipe ada kubwa tu ili wakiisha tuwe tumepiga Mpunga mrefu..
Mkuu, kwani watalii ndio wanaowaua tembo? Ngoja nihakiki vyeti vyangu kwanza, nitarudi
 
Back
Top Bottom