Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Naunga mkono juhudi za Rais kuongeza wigo wa pato la taifa, lakini anahitaji wachumi wazuri kumshauri kwa sababu kuna mambo anapotoshwa. Mojawapo ni hili la watalii. Rais amesema ameongeza ada ya watalii (VAT) na asiyetaka asije. Anasema ni heri kupata watalii wachache wanaolipa ada kubwa kuliko watalii wengi wanaolipa ada ndogo. Kuna mambo mawili Rais kapotoshwa;
#Mosi, kanuni za uchumi zinaelekeza kutoza ada ndogo kwa rasilimali isiyoisha na kutoza ada kubwa kwa rasilimali inayoisha. Kwa mfano watalii wanapaswa kutozwa ada ndogo kwa sababu hawapunguzi chochote kuja kutembelea Tanzania, na sekta ya madini/gesi zinapaswa kutozwa ada kubwa kwa sababu zinapungua kadri zinavyotumika (ipo siku zitaisha).
Rasilimali ambazo zikitumika zinaisha zinapaswa kuwa na ada kubwa, na zile ambazo zikitumika haziishi ada yake inapaswa kuwa ndogo. Simba wa mikumi hawezi kufa kwa kuangaliwa na watalii milioni 1 au kupigwa maelfu ya picha, wala mlima Kilimanjaro hauwezi kudidimia kwa sababu watalii wengi wameupanda. Kwahiyo ada ya utalii inapaswa kuwa ndogo (affordable).
Lakini ilivyo kwa sasa ni vice versa. Rasilimali zinazoisha kama gesi na madini zinatozwa ada ndogo na zile zisizoisha kama utalii zinatozwa ada kubwa. Rais anapaswa kushauriwa vzr zaidi ktk hili.
#Pili; Si kweli kwamba tukipata watalii wachache wanaolipa ada kubwa mapato yetu yataongezeka kama alivyosema Rais Magufuli. Mapato yangeongezeka kama tungepata watalii wengi wanaolipa ada ndogo si watalii wachache wanaolipa ada kubwa. Kanuni za uchumi zinaeleza kuwa biashara nzuri ni ile yenye faida ndogo lakini ina wateja wengi, na sio yenye faida kubwa lakini ina wateja wachache.
Ndio maana Bakhresa anauza juice na maandazi lakini anawazidi wanaouza magari. Hii ni kwa sababu Bakhresa anapata faida ndogo kwa watu wengi tofauti na wauza magari wanaopata faida kubwa kwa watu wachache. Bakhresa anaweza kupata faida ya sh.200 tu kwa kila juice lakini akauza juice milioni moja kwa siku. So akapata faida ya milioni 200 daily. Muuza magari anaweza kupata faida ya milioni 10 kwa kila gari lakini akauza gari 1 tu kwa siku. Kwa hesabu hii Bakhresa amemzidi muuza magari kwa milioni 190 kila siku.
Kwahiyo kama tukitaka kufanikiwa ktk sekta ya utalii kodi ya VAT iondolewe. Hii itafanya kupata watalii wengi watakaolipa ada ndogo hivyo kupata mapato makubwa, kuliko sasa hivi ambapo tunapata watalii wachache wanaolipa ada kubwa na hivyo kuambulia mapato madogo.
Na athari zake zimeanza kuonekana kwa sababu idadi ya watalii imepungua maradufu tangu gharama zilipopandishwa. Wengi wamekimbilia Kenya. Hakuna mtalii anayeweza kulipa mamia ya dola kumuona Simba Tarangire wakati nusu ya pesa hiyo anaweza kuitumia kumuona Simba mbuga ya Tsavo nchini Kenya. Hii si dalili nzuri kwa ustawi wa uchumi wetu. Nitaeleza vizuri kwenye #JamboLeo ya jumanne July 26.
Malisa G.J