Mi nachoona ni angepiga kimya...maana tunatangaza utalii huku rais anasema (indirectly) kuwa kama mmesusa hakuna anayejali...
Kodi walipe na hakuna haja ya kurudia rudia kutangaza hili...wanaweza wasije si sababu ya gharama ila sababu watanzania hawajali ujio wao...akati nchi nyingine zinawapigia magoti...
BIASHARA ushawishi
Nadhani inabidi kuangalia suala zima kwa upana wake
Tukiangalia kodi tu tutakuwa tumejidhulumu
Watalii wanatengeneza sekta nzima ya Utalii inayohusiana na sekta nyingine.
Kwa mfano, sekta ya usafiri na huduma. Je, ni watu kiasi gani wanaajiriwa katika sekta hizo na kupitia wao serikali inafaidika vipi kwa kodi zao?
Nitoe mfano, kuna nchi nilikuwa 'on transit'. Nilifikiwa na watu wakinishawishi niende kuangalia vivutio vya nchi yao. Niliwaambia sina visa ya kuingia.
Waliniambia hilo niwaachie wao, haikupita nusu saa temporary visa mkononi, usafiri nje na kuondoka mara moja.
Sikulipia visa, hata hivyo kwa muda tuliokuwa huko tulitumia pesa za viingilio , wengine kununua 'souvenir' chakula n.k.
Hii maana yake, sekta yao ya usafiri ilipata kitu, sekta ya huduma ilipata kidogo, sekta ya bishara kidogo n.k.
Ukiangalia ajira zilizopatikana na kodi inayotokana na ajira hiyo, gharama za visa au kodi zilikuwa nothing
Tunahitaji watalii wengi ili kupitia kwao wa 'inject' dola katika uchumi wetu kuanzia kwa wapagazi hadi serikali kuu.
Hii kauli ya wakitaka waje au wasipotoka wasije si ya kibiashara au kidiplomasia
Kuna nchi nyingi duniani za kutembelea, biashara ya utalii ina ushindani mkubwa sana.
Kinachotakiwa ni lugha yenye kuvutia, mikakati yenye maana na endelevu
Hili si la ubabe ubabe,sisi tupo katika 'receiving end' tusiigeuze hiyo kuwa 'losing end'