Master Legendary
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 550
- 786
Ni kuhusu umoja wa kitaifa katika Matukio kama haya ya kitaifa.
Niliona limetokea kwa Lowassa nature ikalirekebisha ila nashangaa tena kwa Mwinyi limejitokeza tena.
Naona Mama anapambana sana kuhusu 4R ila wasaidizi wake inaonekana hawako tayari au bado wanaishi katika ulimwengu wa hofu.
Mzee Mwinyi ndiyo Muasisi wa Mageuzi ya Demokrasia,nilitegemea katika Msiba huu Vyama vya Upinzani navyo vipewe nafasi ya kuzungumza katika Ratiba ila sijaliona hilo.
Msiba umekuwa wa upande mmoja kwa Maana ya Serikali na Chama chake wakati kiuhalisia sivyo ni msiba wa kitaifa na ungetumika vizuri kuonyesha na kuimarisha umoja wa kitaifa.
Ukimuangalia Rais anatamani sana Taifa liwe moja ila inaonekana kuna shida sehemu ndiyo maana utekelezaji wa Dhamira yake unakutana na Vihunzi vingi sana.
Sijui ni kwanini!