Hotuba ya Rais Samia Suluhu kwa Taifa Desemba 8, 2021 kuelekea miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika

Kuelekea Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akilihutubia Taifa leo tarehe 08 Desemba, 2021, Ikulu Jijini Dar es Salaam



Ndugu wananchi nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, saa chache zijazo tunaadhimisha miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika sasa Tanzania Bara. Umuhimu wa siku hii katika historia yetu ni wa kipekee, kwani Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tuliyonayo leo isingeweza kuzaliwa Aprili 26, 1964, kama kusingelitanguliwa na Uhuru wa Tanganyika na baadaye Mapinduzi ya Zanzibar. Mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa chachu ya kufanikisha muungano adhimu, na kupelekea Taifa letu kuwa la amani na mshikamano.

Katika harakati za kutafuta Uhuru Mwalimu Nyerere alikuwa na wenzake 16. Ninasikitika kwamba watu wote 17 walioshiriki kupigania Uhuru wametangulia mbele ya haki. Hakika wangetamani sana kuiona siku ya leo.

Kwa mujibu wa takwimu zetu za idadi ya watu, Watanzania 2,520,559, sawa na asilimia 4.3 ya Watanzania wote milioni 59 waliopo sasa, ndio waliokuwa wamezaliwa kabla ya Disemba 9, 1961. Sisi ambao tumepata bahati ya kushuhudia siku ya Uhuru na kuadhimisha miaka 60 ya uhuru, huenda tusipate bahati hii ya kuadhimisha makumi kama haya mengine.

Mafanikio mengi tumeyapata tangu kupata uhuru wa nchi yetu, mafanikio hayo si tu yatahitahitaji muda mrefu kuyaelezea bali pia kupata kurasa nyingi ili kuweza kuyaandika.
Mafanikio ya Miaka 60 ya Uhuru

1. Kufanikiwa kuulinda uhuru au uhuru wetu na mipaka yake​
2. Kujenga umoja wa kitaifa na mshikamano uliozaa na kulea amani na utulivu tulionao​
3. Kuimarisha uchumi wetu na kupunguza umasikini kulikotuwezesha kutoka kwenye kundi la nchi maskini na kuingia kwenye kundi la nchi za uchumi wa kati wa chini​
4. Kuongeza upatikanaji na kuboresha huduma za jamii kwa wananchi​
5. Kujenga heshima ya nchi yetu na ushawishi kikanda na kimataifa​
6. Kuimarisha Demokrasia na Utawala wa Sheria​

Jeshi letu limekuwa na weledi katika ulinzi wa mipaka yetu, katika kipindi cha miaka 60 ya Uhuru wetu, hatujapoteza eneo letu na ni fahari kwa kuwa na jeshi lenye utii na uzalendo kwa Taifa letu.

Kama lipo eneo ambalo tumefanikiwa zaidi ni kuboresha maisha ya wananchi. Tumeweza kuongeza upatikanaji wa maji maeneo mbalimbali ya mijini na vijijini.

Wastani wa pato kwa mtu kwa mwaka 1961 lilikuwa ni shilingi 776 na kwa mwaka 2020 ni shilingi 2,653,790. Jambo hili linaongeza hadhi yetu machoni pa jumuiya ya kimataifa na kutuondolea unyonge.

Kutokana na kukua kwa Uchumi katika nchi yetu Usafiri wa anga si suala la anasa wala starehe hivyo kufufuliwa au kuimarishwa kwa shirika letu la ndege ATCL ni jambo la lazima. Tumeishanunua ndege 12 na malipo ya ndege nyingine 5 yamekwishafanyika

Tanzania inakadiriwa kuwa na makabila zaidi ya 120, lakini pamoja na tofauti zote hizo tumeweza kuwa na Taifa moja na kuweza kuunganishwa na lugha ya Kiswahili. Si kitu rahisi.

Katika kipindi cha miaka 60 ya uhuru, tumeweza kufikia uchumi wa kati mapema hata kabla ya lengo la kufikia uchumi huo mwaka 2025, hali hii inatuondolea unyonge kimataifa na kutuondolea unyanyapaa.

Tumeweza kuunganisha mikoa kwa barabara za lami, na kazi ya kuunganisha makao makuu ya wilaya kwa barabara inaendelea.

Wakati tunapata uhuru tulikuwa na meli 6 na sasa tuna meli 14 zinazofanya kazi katika Ziwa Nyasa, Victoria na Tanganyika.

Wakati tunapata uhuru nchi yetu ilikuwa inazalisha megawati za umeme 17.5 tu, lakini sasa tunazalisha megawati 1909, huku tukiwa na matarajio ya kuongeza megawati nyingine 2,115 tutakapokamilisha ujenzi wa Bwawa la Nyerere [JNHPP].

Wakati tunapata uhuru tulikuwa na walimu wa shule za msingi 36 lakini sasa tuna walimu wa shule za msingi 281,728".

Tumerudisha fursa ya watoto watoro na waliopata changamoto mbalimbali kurudi shule.

Tumepiga hatua kwenye eneo la elimu ya juu kwani kwa sasa tuna vyuo vikuu 30, vya serikali 18 na 12 vya sekta binafsi na vyuo vishiriki 17.

Kilicho dhahiri katika sekta ya afya, ni ule uwezo wa kutoa huduma za kibingwa ambazo zamani hazikuwepo na tulikuwa tukilazimika kupeleka wagonjwa nje ya nchi na hivyo kutumia fedha nyingi za kigeni.

Umri wa kuishi kwa Watanzania umeongezeka kutokana na uboreshaji na upatikanaji wa lishe na kuondoa udumavu, wakati tunapata uhuru wastani wa umri wa kuishi kwa Watanzania ulikuwa ni miaka 37 na sasa ni miaka 67.

Tanzania imeendelea kuimarika, nguvu ya kushawishi imeendelea kukua na kuaminika ikiwemo Watanzania kuongoza taasisi mbalimbali za Kimataifa. Tulikuwa na balozi mbili tu mwaka 1961 na sasa tuna balozi 44. Diplomasia yetu inapanuka na inaendelea kung’ara duniani.

Tangu kurejea kwa mfumo wa vyama vingi tuna vyama vilivyosajiliwa 19 na 17 vinavyoomba usajili wa muda, na tumekuwa na mfumo bora na imara wa kuweka viongozi madarakani ambao unaheshimiwa na kuaminiwa.

Tumekuwa na mfumo imara wa utoaji haki kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu kwa kuzingatia msingi wa kuwa binadamu wote ni sawa na hakuna aliye juu ya sheria.

Tutunze mazingira yetu kwa uchungu mkubwa ili turithishe kwa watoto na vizazi vyetu nchi ambayo ni ya neema kama ilivyokuwa kwetu.

Dira yetu ya maendeleo kufikia 2025 inaelekea kumalizika ambapo tunatarajia kukua kwa uchumi kwa asilimia 8. Tunapoangalia mbele tunakwenda kuandaa dira ya miaka 25 ijayo (2025-2050) ambayo itaelekeza kukua kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Ndugu wananchi, kabla sijamaliza ninayo kila sababu ya kuwashukuru na kutambua mchango wa viongozi wetu ambao wao na awamu walizoziongoza wametufikisha kwenye haya makubwa tunayoshuhudia leo.

Wale waliotangulia mbele ya Haki tuombe mwenyezi Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi, Amen. Daima tutawakumbuka na kuenzi michango yao adhimu kwa Taifa hili

Tuna kila sababu yakujivunia maendeleo tuliyoyapata katika kipindi cha miaka 60, hatujafikia kilele cha matamanio yetu lakini tulipofika si haba.

Mafanikio tuliyoyapata kwa miaka 60 yamebebwa na utawala wa sheria na utawala bora. Tumekuwa na mfumo bora unaoheshimiwa wa kuweka viongozi madarakani kupitia chaguzi zinazofanyika kila baada ya miaka mitano

Tutembee kifua mbele na kujisifu, wala tusijifuje na kujipa unyonge na kwa vyovyote vile kwani mambo tuliyoyafanikisha kwa miaka 60 ni mengi na makubwa kuliko yale yaliyofanyika nchini wakati wa ukoloni. Tusilinganishe tu kina tulichofikia, na tukasahau kutazama urefu wa kina tulichoanzia.

Kwa maneno haya niwatakie tena kila la kheri katika kusherekea Uhuru wa Tanzania Bara

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Afrika

Nawashukuru sana kwa kunisikiliza, Kazi Iendelee

Asanteni Sana.

Aliyeelewa hotuba ya Rais Samia Suluhu kwa Taifa Desemba 8, 2021 kuelekea miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika tafadhali?​

 
Watoa comments wengi kwenye huu uzi ni Kanda ya Ziwa na Kaskazini. Wote Wana maumivu na Mama
 
Nilikuwa zangu kwenye mishe za maisha, nilipoona wito wa watu kutakiwa kumsikiliza nikaharakisha sana shughuli zangu ili niwahi nijue Jambo.
Nimesikiliza na nimeangalia Ila mbona sijaelewa? Hii ndio kuhutubia taifa? Mbona hotuba ipo shallow sana?
Au saa 4 Kuna nyingine tusubiri?
Hadi sasa najuta kupoteza muda wangu
Mdau mmoja hapa JF kaandika: Bora hagaya angelala tu; hotuba yake ni utopolo mtupu
 
Jpm alikuwa anahutubia taifa akiwa field anakagua maendeleo na watu wakikuwa kila kona unasikia wametune viredio vyao wanamsikiliza mwamba akitema madini!

Huu ujinga wa kujifungia ikulu na kusema eti ndio unahutunia taifa mwishowe unaambulia aibu kama hivi.
 
Jpm alikuwa anahutubia taifa akiwa field anakagua maendeleo na watu wakikuwa kila kona unasikia wametune viredio vyao wanamsikiliza mwamba akitema madini!

Huu ujinga wa kujifungia ikulu na kusema eti ndio unahutunia taifa mwishowe unaambulia aibu kama hivi.
Haaaa JPM alikuwa kisanga anautubia taifa akiwa ground yaani kwenye mauzinduzi wa miradi
 
Nilikuwa zangu kwenye mishe za maisha, nilipoona wito wa watu kutakiwa kumsikiliza nikaharakisha sana shughuli zangu ili niwahi nijue Jambo.
Nimesikiliza na nimeangalia Ila mbona sijaelewa? Hii ndio kuhutubia taifa? Mbona hotuba ipo shallow sana?
Au saa 4 Kuna nyingine tusubiri?
Hadi sasa najuta kupoteza muda wangu
Umesema hujaelewa, halafu unasema ipo shallow. Ulijuaje ipo Shallow bila kuelewa?
 
Worse speech ever! Si angeandika tu kwenye Twitter why atusumbue kumsikiliza wengine kwa majirani halafu hajazungumzia mambo nyeti yanayolokabili Taifa Sasa?
Me nasema mama kajitahidi Sana yaani wembamba wa reli TREN inapita, nachomaanisha hotuba fupi lakini imebeba maneno yaliyoshibaaa
 
Tumefundishwa historia tu
Hotuba ya Chongolo, mchana ilihusu takwimu za kihistoria, hotuba ya usiku nayo imejikita kwenye takwimu za kihistoria! Kwani wanatoka vyama tofauti? Au kuna mmoja kachukua script ya mwenzake?Why all these! Au ndio wale waserikali wanavuruga wamemtumia Chongolo?Where is wayfoward?
 
Back
Top Bottom