Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 12,152
- 44,110
Tanzania na Afrika kiujumla kwenye ulinzi wa viongozi wetu bado tuko kishamba na kizamani. Ulinzi wa viongozi wetu umejaa mbwembe na ujinga wa kizamani sana. Hatujui kutofautisha kati ya ulinzi na mbwembe, au walinzi na wapambe au kulinda na kuzongazonga. Sisi bado tunaamini wapambe ndio walinzi, kuzongazonga ndio kulinda!
Mifumo ya kisasa ya ulinzi kidunia kwa viongozi imebadilika sana, sisi bado tunaamini ulinzi ni kujaza wapambe kibao kumzunguka rais, huku tukisahau wabambe hao hao sio watu salama sana kwa rais, adui anaweza kupenya na kuwa miongoni mwa wapambe hao hao!
Ngoja twende kwa mifano.
-Rais akiwa kwenye himaya yake (eneo lililoandaliwa na kikosi chake cha usalama kabla ya rais kuwepo eneo hilo), hakuna sababu ya wapambe au walinzi kumsogelea karibu hata mita mitano. Wakae mbali kabisa.
-Rais akiwa Ikulu, hakuna sababu ya walinzi au wapambe kumsongasonga.
-Rais akiwa eneo la kiitifaki chini ya protokali mahususi (mfano bungeni, kwenye mikutano ya wakuu wa nchi, dhifa za kitaifa na kimataifa nk) hakuna sababu ya wapambe kumzonga zonga.
-Rais akiwa amezuka mtaani katika ziara binafsi ya kijamii 'iliyotengenezwa' hapaswi kuzungukwa na wapambe.
Mifano ni mingi, na wajuzi watakuwa wamenielewa, kama mtu huwezi kuelewa hilo basi jaribu kutazama namna wakuu wa nchi zenye vitisho vikubwa vya kiusalama wanavyolinda viongozi wao. Tazama USA, UK, Israel, Germany, France, Spain nk. utaelewa ninachokisema.