T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 13,804
- 46,726
Una uhakika PSU iko chini ya TISS au umedhania. Sina hakika kama sisi tunaziunganisha, nilitumia comparison na nchi nyingine nyingi ambazo hutofautisha sana hivi vitengo hasa hizi ambazo hazijakomaa kiusalama na kiutawala. Nchi nyingi hazichanganyi ili mmoja akiharibu mwingine arekebishe.Sasa PSU si wapo chini ya TISS? Hata kazi za TISS huzijui? Moja kati ya kazi zao ni VIP protection, ni kama jeshini au polisi kuna mgawanyiko wa kazi, wengine trafiki, wengine wapelelezi na wengine kutuliza ghasia. Vivyo hivyo kwa TISS wapo undercover informers, walinzi wa viongozi, deep covers nk.
Refer jaribio la mapinduzi nchini Uturuki dhidi ya Erdogan mwaka 2016. Presidential guard yao ilikutwa na washiriki 300 kati ya watu 2500 kwenye regiment wakati intelligence agency yao ndio ilizima mapinduzi. Hata wanamapinduzi walishambulia HQ za usalama wa taifa baada ya mkuu wa usalama kupata briefings mapema ikabidi wanamapinduzi watekeleze jaribio masaa matano kabla walipojua wameshtukiwa na hawana control uko.