Sisi majirani karibu na msikiti wa kunduchi Beach eneo la Mtakuja, tunapenda kutoa malalamiko yetu kuhusu kelele kubwa kutoka msikiti huo uliopo mtaa wa Mbudya. Ibada katika msikiti huu huanza kuanzia saa 10 alfajiri, na sauti inayotumika ni kubwa kupita kiasi cha kuwasumbua wakazi wa eneo hili, hasa nyakati ambazo watu wanahitaji kupumzika.
Hali hii si ya kawaida, na imekuwa chanzo cha usumbufu mkubwa kwa wakaaji. Sauti inabaki kuwa kubwa hata mchana, jambo linaloathiri utulivu wa majirani. Tunatambua na kuheshimu uhuru wa kuabudu kama haki ya msingi, lakini ni muhimu kutekeleza ibada bila kusababisha usumbufu kwa wengine.
Kumekuwa na juhudi kadhaa za kuwasihi viongozi wa msikiti huu kupunguza kiwango cha sauti, ikiwa ni pamoja na mazungumzo ya ana kwa ana na hata barua rasmi kutoka kwa uongozi wa mtaa. Hata hivyo, juhudi hizi hazijazaa matunda kwani bado tatizo linaendelea na uongozi wa msikiti haujaonyesha ushirikiano.
Tunaomba serikali sikivu na mamlaka husika kuingilia kati ili kuhakikisha kwamba ibada zinaendelea bila kelele kubwa zinahathiri utulivu was wakaaji wa mtaa huu. Dini inatufundisha kuishi kwa utulivu na kujali wengine.
Sijausoma hata ujumbe wenyewe. Kichwa cha habari tu kinatosheleza.
Nchi hii inaongozwa kwa mujibu wa sheria na au desturi.
Moja ya haki ya kidemokrasia ni desturi ya wengi ktk eneo fulani la utawala, mf mtaa, kitongoji, kata na kuendelea ambapo jamii ya wengi ktk eneo hilo hutunga Sheria (Wengi Hushinda). Ndio maana tuna uchaguzi kuanzia ngazi ya mtaa.
Kama Watanzania tunaishi kwa utofauti wa kitamaduni ambao unakaribisha na kukubali watu kutoka mazingira yote ya kijamii, kisiasa, kidini, kikabila na kieneo.
Watu wote wako huru kufuata dini yao na tamaduni zao za asili bila kusahau kuwa kuna utamaduni za wengi ktk eneo hilo.
Na kwamba ili kuepusha mfarakano usio wa lazima wachache wanapaswa kufungwa na kuzuiliwa mara tu tamaduni zao zinapokinzana na tamaduni za wengi za eneo hilo. Katika hali kama hiyo je eneo unaloishi wazawa wengi ni watu wenye tamaduni inayounga mkono adhana au inayohisi ni kelele.
Ili kuweka utaratibu mzuri zaidi wa kisheria ndio maana mara zote naunga mkono, kuundwa kwa utawala wa Serikali za majimbo yenye uhuru zaidi wa kujiamulia mambo yao wenyewe. Si tu kwa Zanzibar bali pia Tanzania Bara kwa hatima yetu vizazi vyetu. Kama Tanganyika ingekuwa na mfumo wa Serikali za majimbo yenye uhuru zaidi wa kujiamulia mambo yao wenyewe ukweli mfumo huu tulionao wa Serikali ambapo mji mkuu uko chini ya utawala wa jamii minority, ukweli tusinfekuwa na vurugu za mabucha ya nguruwe manzese.
Kwa sababu si tu sheria za Serikali za mitaa zinakataza kuuza uchafu huu maeneo ya jamii ambapo wengi ni hawatumii bidhaa hiyo bila ya shaka ingawa wengi wa watendaji wa Serikali wanatumia bidhaa hiyo lkn kiutawala wao ni minority.