Tumwesige senior
JF-Expert Member
- Jan 28, 2013
- 5,879
- 10,394
Na jamaa huwa wanafunga ma koni makubwa kwenye misikiti sijui yana watts ngapi yale utaskia swalaaa swalaaa swalaaaaaaaaa
Na jamaa huwa wanafunga ma koni makubwa kwenye misikiti sijui yana watts ngapi yale utaskia swalaaa swalaaa swalaaaaaaaaa
Hizo siyo kelele ni alarm ya kuwaita wahusika wafike eneo husika.Kuna watu huku mkuu wanaendekeza sana kelele. Yaani wanapiga kelele mara tano kwa siku. Watu wanakatishwa usingizi kila siku
Ina maana wao wanalazimishwa na hawajuhi wajibu wao?Hizo siyo kelele ni alarm ya kuwaita wahusika wafike eneo husika.
Video iko wapi?Sisi majirani karibu na msikiti wa kunduchi Beach eneo la Mtakuja, tunapenda kutoa malalamiko yetu kuhusu kelele kubwa kutoka msikiti huo uliopo mtaa wa Mbudya. Ibada katika msikiti huu huanza kuanzia saa 10 alfajiri, na sauti inayotumika ni kubwa kupita kiasi cha kuwasumbua wakazi wa eneo hili, hasa nyakati ambazo watu wanahitaji kupumzika.
Hali hii si ya kawaida, na imekuwa chanzo cha usumbufu mkubwa kwa wakaaji. Sauti inabaki kuwa kubwa hata mchana, jambo linaloathiri utulivu wa majirani. Tunatambua na kuheshimu uhuru wa kuabudu kama haki ya msingi, lakini ni muhimu kutekeleza ibada bila kusababisha usumbufu kwa wengine.
Kumekuwa na juhudi kadhaa za kuwasihi viongozi wa msikiti huu kupunguza kiwango cha sauti, ikiwa ni pamoja na mazungumzo ya ana kwa ana na hata barua rasmi kutoka kwa uongozi wa mtaa. Hata hivyo, juhudi hizi hazijazaa matunda kwani bado tatizo linaendelea na uongozi wa msikiti haujaonyesha ushirikiano.
Tunaomba serikali sikivu na mamlaka husika kuingilia kati ili kuhakikisha kwamba ibada zinaendelea bila kelele kubwa zinahathiri utulivu was wakaaji wa mtaa huu. Dini inatufundisha kuishi kwa utulivu na kujali wengine.