#COVID19 Kuna haja ya Serikali kulazimisha Watumishi wa Umma kuchanja chanjo ya UVIKO-19

Abdalah Abdulrahman

JF-Expert Member
Aug 29, 2019
222
201
Watumishi wa umma ndio wanaowahudumia wananchi,kasi ya ugonjwa wa uviko-19 inaweza kupungua kwa serikali kuwalazimisha watumishi wa umma kuchanja.

Hii itasaidia
1. Watumishi kuto ambukizana
2. Watumishi kuto ambukiza wananchi
3. Wananchi kuto kuwaambukiza watumishi

Nchini Kenya idadi ya wananchi wliochanja ni kubwa ukilinganisha na Tanzania,licha ya idadi kuwa kubwa masharti magumu yamewekwa kwa wananchi wasiochanja ikiwepo kusafiri na kupata huduma zingine.

Tanzania haitakiwi kuweka masharti magumu,njia nyepesi ni kuhakikisha kila mtumishi anapata chanjo,baada ya watumishi wote kupata chanjo tunaenda kwa watoa huduma kwa serikali,na baadae kwa wananchi
 
Watumishi wa umma ndio wanaowahudumia wananchi,kasi ya ugonjwa wa uviko-19 inaweza kupungua kwa serikali kuwalazimisha watumishi wa umma kuchanja...
Usafiri wa daladala sio mali ya umma wala watumishi wake (dereva na kondakta) sio watumishi wa umma, lakini wanakutana na abiria tofauti kwa kiwango kikubwa kuliko watumishi wengi wa umma wanavyokutana na watu
 
Kwanini serikali inakataa wajibu endapo litatokea tatizo??
Kukataa wajibu ni jambo la kisheria,kila dawa ina madhara yake na ni wazi kuwa hii kinga ina athari zake ambazo serikali haiwezi kukugaranti kuwa madhara yake itahusika.
 
Back
Top Bottom