Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 2,515
- 4,230
Habari wakuu,
Kuna baadhi ya watu maarufu na wasiokuwa maarufu kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakionyesha chuki za wazi dhidi ya awamu ya tano pamoja na viongozi wake. Mbaya zaidi walifika hatua ya kutaka kusahaulisha 'Legacy' na kazi kubwa sana iliyofanywa na awamu ya tano.
Kwa siku kadhaa wakosoaji hao wameshuhudia wimbi kubwa la ujambazi, ubadhirifu, uzembe kwa baadhi ya viongozi, hali ya uchumi kuzidi kudorora, Matumizi mabaya ya rasilimali za umma, hakuna miradi mipya iliyoibuliwa zaidi ya kukamilisha ile ya awamu ya tano na mengineyo mengi ndani ya muda mfupi.
Hakuna uongozi usiokuwa na mapungufu lakini ni wazi kwamba uongozi wa awamu ya tano ulifanya mambo makubwa sana yaliyowagusa Watanzania wa hali zote. Mapungufu ya awamu ya tano yalikuwa na nafuu kuliko mapungufu ya awamu yoyote ile na haya yanaanza kujidhihirisha pia katika awamu hii. Asilimia 100 ya waliokuwa wanapinga juhudi za awamu ya tano japo hawapo tayari kukubaliana na ukweli lakini wengi mioyoni mwao wanajutia na wanatubu baada ya kuanza kujionea utofauti ila wanaogopa kukiri na kuomba msamaha.
Kwa haya machache tunayo kila sababu kama taifa kuwaombea msamaha kwa Mungu na kwa jamii wale wote waliokosoa awamu ya tano kwa nia mbaya ili kuondosha laana ambayo kama taifa itaweza kuipata.